Mbunge ataka mafisadi kujivua gamba Krismasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge ataka mafisadi kujivua gamba Krismasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 27, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"][TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]VIONGOZI na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi, wameshauriwa kutoitumia Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Krismasi) kama siku ya kihistoria na badala yake waitumie kujivua magamba. “Krismasi ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu. Ni vizuri nasi viongozi na wanasiasa tukaitumia kuzaliwa upya na kwa wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wakazaliwa upya kwa kujivua magamba,” alisema Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe. Aliyasema hayo jana wakati akitoa salamu zake za sikukuu hiyo kwenye Ibada ya Krismasi aliyohudhuria katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) mjini hapa.

  Alisema historia ya nchi itaendelea kuenziwa kutokana na sera nzuri za CCM ambayo hata hivyo inakwaza na kudondoshwa na baadhi ya watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu wao
  ipasavyo. Alisema CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi, lakini katika mazingira yasiyo ya haki, Serikali imekuwa ikilitazama kwa jicho la upendeleo kundi moja la wanasiasa kwa kuwaongezea posho bila kuzingatia mahitaji ya Watanzania wengine wakiwemo wenye chama.

  “Kimsingi sipingi hata kidogo posho za wabunge kuongezwa, lakini ni muhimu tunapofanya hivyo wafanyakazi wengine wa umma wakaboreshewa mishahara na kuongezewa posho,” alisema. Alisema wakati wanasiasa wakiongezewa posho, baadhi ya viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanazidi kukaidi wito unaowataka wao wenyewe kuwajibika jambo linaloendelea kuharibu sifa ya chama. Alisema kama Serikali itaboresha maslahi ya watumishi wengine wa umma kwa kuzingatia hali halisi ya sasa na watuhumiwa wa ufisadi wakajivua magamba, chama hicho na Serikali yake watakuwa wamezaliwa upya.

  Alisema Tanzania inazo rasilimali nyingi na kama kukiwepo na uadilifu na zikatumika kwa kuzingatia mahitaji ya taifa, matatizo mengi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayowakabili
  Watanzania walio wengi yatapungua. Alisema hali ya mambo ndani ya CCM na Serikali yake sio nzuri kwa kuwa wapo baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali wanaofanya kazi walizopewa chini ya kiwango kwa lengo la kumkwamisha Rais Jakaya Kikwete.

  Habari Leo
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"][TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: right"][/TD]
  [TD="class: kaziBody, align: center"][/TD]
  [TD="class: kaziBody, align: left"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, width: 47%, align: right"][/TD]
  [TD="class: mainStory, width: 3%, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hii single haina radha tena watafute nyingine ya kuwafanya waaminike mbele ya umma
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Binafsi anafanya anachokiamini, kwa sababu wengine wanaimba wimbo tu bila kucheza, yeye haoni aibu hata kumkodolea macho ****** anapofanya mambo kinyume. Jamaa anajitahidi ila tu anakosa wenzake wakusimama pamoja, na hivyo kwa vyo vyote wanamwona kama msaliti.
   
Loading...