Mbunge apewa siku 3 atoe ushahidi wa magari 777 ya washawasha, adai taarifa alizipata JamiiForums

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Mbunge Apewa Siku 3 Atoe Ushahidi wa Magari 777 ya Washawasha .

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amempa siku tatu Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (CHADEMA) awasilishe mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, maelezo ya utetezi dhidi ya madai aliyotoa bungeni kuhusu Serikali kununua magari ya washawasha 777.
Ndugai alitoa amri hiyo kutokana na mwongozo ulioombwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni juzi akitaka Lyimo athibitishe au afute kauli yake juu ya madai hayo wakati serikali imenunua magari 32.

“Hata kwa akili ya kawaida haiwezekani Serikali ikaagiza magari yote hayo 777 ya washawasha. Ninachokumbuka mimi Waziri huyu aliwahi kusema hapa bungeni kuwa magari hayo 777 ni idadi ya magari yote ya aina mbalimbali yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya polisi,” alisisitiza Ndugai.

“Sasa nakutaka uniandikie rasmi majibu vizuri kuhusu kauli yako hii, nakupa siku tatu uwe umeniletea na baadaye nitaipeleka taarifa yako kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, ili kujadili suala hili kwa mapana,”alisisitiza Ndugai.

Awali mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Ndugai alimpatia mbunge huyo nafasi ya ama kufuta kauli yake hiyo au aithibitishe kabla ya hatua za kikanuni za Bunge hazijachukuliwa dhidi yake.

Lyimo alikataa kufuta kauli hiyo na kudai kuwa anao uthibitisho juu ya idadi hiyo ya magari aliyoitamka na kusisitiza kuwa amenukuu taarifa za idadi hiyo kupitia taarifa iliyotolewa na mtandao wa Jamiiforum pamoja na taarifa za Hansad za Bunge.

“Mheshimiwa Spika mimi ni mtu mzima siwezi kwenda kwa hisia za watu, ni kweli jana niliombewa mwongozo bahati mbaya sikuwepo ndani ya Bunge. Nathibitisha kauli yangu na wala siifuti kwa kuwa nina uhakika na idadi ya magari niliyoisema,” alisisitiza mbunge huyo.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) ya Bunge, mbunge hatasema uongo endapo chochote atakachokisema ndani ya Bunge atakuwa amekirejea kwenye chombo cha habari au taarifa za Bunge.
 
Safi sana
Wabunge walizidi kuropoka ovyo
Hawa Jadili vitu vya muhimu kazi yao kusema uongo wapate umaarufu

Kama huna ushahid usiseme kitu wabunge wetu wengi vichwa maji wote wa CCM mpaka wilaya upinzani wengi wao hawajui wanakosea sijui kama zile semina huwa zinazokuwa zinaeleweka
 
Huo ni mkenge waliingizwa na jk na wakaingia wazima wazima,ha ha ha,yule baba alikuwa na mbinu za hali ya juu..

Hivi kweli washawasha 777 utazificha wapi zisionekane?
 
Ninachofurahia kumbe Suzan na wabunge wengine wapo JF 24/7 hivyo hata yale tunayoeleza kuhusu KUB yatarekebishwa.
 
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amempa siku tatu Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) awasilishe mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, maelezo ya utetezi dhidi ya madai aliyotoa bungeni kuhusu Serikali kununua magari ya washawasha 777.

Ndugai alitoa amri hiyo kutokana na mwongozo ulioombwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni juzi akitaka Lyimo athibitishe au afute kauli yake juu ya madai hayo wakati serikali imenunua magari 32.

“Hata kwa akili ya kawaida haiwezekani Serikali ikaagiza magari yote hayo 777 ya washawasha. Ninachokumbuka mimi Waziri huyu aliwahi kusema hapa bungeni kuwa magari hayo 777 ni idadi ya magari yote ya aina mbalimbali yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya polisi,” alisisitiza Ndugai.

“Sasa nakutaka uniandikie rasmi majibu vizuri kuhusu kauli yako hii, nakupa siku tatu uwe umeniletea na baadaye nitaipeleka taarifa yako kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, ili kujadili suala hili kwa mapana,”alisisitiza Ndugai.

Awali mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Ndugai alimpatia mbunge huyo nafasi ya ama kufuta kauli yake hiyo au aithibitishe kabla ya hatua za kikanuni za Bunge hazijachukuliwa dhidi yake.

Lyimo alikataa kufuta kauli hiyo na kudai kuwa anao uthibitisho juu ya idadi hiyo ya magari aliyoitamka na kusisitiza kuwa amenukuu taarifa za... idadi hiyo kupitia taarifa iliyotolewa na mtandao wa Jamii forum pamoja na taarifa za Hansad za Bunge.

“Mheshimiwa Spika mimi ni mtu mzima siwezi kwenda kwa hisia za watu, ni kweli jana niliombewa mwongozo bahati mbaya sikuwepo ndani ya Bunge. Nathibitisha kauli yangu na wala siifuti kwa kuwa nina uhakika na idadi ya magari niliyoisema,” alisisitiza mbunge huyo.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) ya Bunge, mbunge hatasema uongo endapo chochote atakachokisema ndani ya Bunge atakuwa amekirejea kwenye chombo cha habari au taarifa za Bunge.
 
Unajua hawa wabunge hawataki kwenda na wakati
Wakati huu sio ule wa kuropoka na kupata sifa hata kama unacho kiropoka ni Ugoro na uongo.

Wa jaribu kujenga hoja za maana
Naona Lema pole pole ana anza kupunguza kuropoka na kufuata Nini watanzania wana hitaji
 
Mbona serikali na Ndugai wanalikuza hili jambo bila sababu za msingi na kupoteza muda wa Bunge kujadili mambo mengine. Ndugai anakiri kwamba alimsikia waziri akisema jumla ya magari ya polisi yaliyonunuliwa ni 777. Susan amesema serikali imenunua magari 777 ya washawasha. Sasa ni muhimu serikali ikafahamu, malalamiko ya msingi, hata kutoka kwa askari wenyewe ni uhaba wa magari ya kuwarahisishia polisi kazi, sasa katika hayo magari 777 ambayo Ndugai anakiri kumsikia waziri akisema, idadi kubwa ni magari ya kuwarahisishia kazi polisi, au ni yale ya washawasha na yale ya kindavandava? Ninaposema ya kuwarahisishia kazi polisi namaanisha kuwawahisha kwenye matukio mbalimbali, au doria za kawaida.
 
Ingekuwa live tungeweza kuona na kusikia exactly alichosema sasa hizi za kuelezwa tu mbunge ametakiwa kujieleza tunaona ni uonevu tu na inatufanya wananchi tuzidi kuichukia serikali
 
Safi sana
Wabunge walizidi kuropoka ovyo
Hawa Jadili vitu vya muhimu kazi yao kusema uongo wapate umaarufu

Kama huna ushahid usiseme kitu wabunge wetu wengi vichwa maji wote wa ccm mpaka wilaya upinzani wengi wao hawajui wa nakosea sijui kama zile seminar huwa zinazokuwa zinaeleweka
Kiherehere cha nini wewe kikongwe?Si usubiri kwanza Lyimo athibitishe kwa ushahidi kama ni uongo ama ukweli ndo uongee kauli hizo.
 
Back
Top Bottom