Mbunge 'amvaa' Dkt. Hosea mkutanoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge 'amvaa' Dkt. Hosea mkutanoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, May 24, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mbunge 'amvaa' Dkt. Hosea mkutanoni

  23 May 2009 17:19

  Na Mwandishi Wetu Saturday,

  MBUNGE wa Jimbo la Kishapu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Bw.Fredy Mpendazoe juzi 'alimvaa'Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Dkt. Edward Hosea kwa madai kuwa taasisi yake imedorora kutokana na upungufu uliomo ndani katiba ya nchi jambo linalohitaji marekebisho ya haraka.

  Akichangia hoja kwenye Semina ya Wabunge kuhusu rushwa iliyofanyika Dar es Salaam, Bw. Mpendazoe, alisema kutokana na madaraka makubwa ya Rais kikatiba, anaweza kuteua marafiki zake ambao mamlaka husika kama TAKUKURU haziwezi kuwagusa inapobidi.

  Alishauri wateule wa Rais kwa nafasi kama TAKUKURU, Usalama wa Taifa na Tume ya Maadili ya Viongozi, waidhinishwe kwanza na Bunge na Rais afanye kazi ya uteuzi tu.

  Alitoa mfano wa Mkurugenzi wa TAKUKURU kushindwa kuwashughulikia baadhi wateule wa Rais kwenye sakata la Richmond na kueleza kuwa hicho ni kielelezo mojawapo cha madhara ya madaraka makubwa ya Rais Kikatiba na kusisitiza Katiba irekebishwe.

  "Rais anamteua kuanzia DC hadi Jaji Mkuu. Maana yake ana nguvu dhidi ya mihimili mingine ya dola na kikatiba hawezi kuhojiwa kwa jambo lolote analofanya au maamuzi yake. Kwa Mfano maamuzi ya Bunge juu ya Richmond hayajatekelezwa yote, inaleta utata, mfano TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa rushwa wakati Bunge liliona kiongozi wa TAKUKURU hakueleweka kwa taarifa yake ya Richmond" alisema, Bw. Mpendazoe.

  Baada ya maelezo hayo, Dkt. Hosea aliyekuwa Mwenyekiti wa Semina hiyo aliinuka na kuhoji"Unataka niteuliwe na nani? Usizungumzie haya," alisema Dkt. Hosea huku akimwamuru mbunge huyo kukaa chini.

  Katika hoja yake, Bw. Mpendazoe, alisema mfumo mzima wa sasa wa Serikali umetokana na katiba ambayo ina upungufu mkubwa unaohitaji marekebisho. Alisema hata Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuzungumzia suala hilo na kubainisha kuwa Katiba ya sasa inampa Rais madaraka makubwa yanayoweza kumfanya dikteta.


  Mbunge huyo pia alikemea rushwa kwenye kura za maoni za vyama vya siasa na chaguzi za jumuiya za vyama. Alisema katika hilo, TAKUKURU inajitahidi kuchukua hatua lakini inashindwa kwasababu ni chombo cha Serikali na Serikali hiyo inatokana na chama cha siasa.

  "CCM inashindwa kuchukua hatua mfano kama mhusika ni Waziri au Mjumbe wa Kamati Kuu au Halmashauri Kuu na ni kiongozi kwenye Serikali. Mapendekezo yangu nikuimarisha TAKUKURU iwe huru isiegemee chama tawala pia kuwe na Tume huru ya uchaguzi.

  Alisema tatizo kubwa linalochangia rushwa kuota mizizi nchini ni jamii kukumbatia jambo hilo na kutochukua hatua dhidi ya walioonekana kuhusika nayo.

  "Albeilt Einstern alisema; Ulimwenguni pamekuwa mahali pa hatari sana kuishi lakini haitokani na uovu unaofanyika bali inatokana na wale wanaouona uovu ukitendeka na hawachukui hatua dhidi ya uovu huo."

  Alisema kumekuwa na tuhuma mbalimbali zinazowakabili watu kuhusu rushwa, Serikali inapochelewa au inapokuwa haichukui hatua kwa muda mrefu, inachochea rushwa zaidi.


  Source: Majira

  Siyo nia yangu kubandika text kutoka gazetini ila hii habari imenigusa mno na tunataka wabunge wenye mtazamo kama huu.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Magezi,

  Hii habari imekaa vizuri sana. Nilipojiunga na JF, niliuliza juu ya madaraka ya Rais. Nikaambiwa nisome katiba na baada ya kusoma, nikakuta Rais ana madaraka ya kutisha. Wengi wameshasema juu ya hili la uteuzi kuwa hawa wateule wa Muheshimiwa wawe wanapitiwa na bunge. Hili ni la kuvalia njuga.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyu mbunge ni wa kumfuatilia, in this instance ameonyesha courage ambayo inahitajika nchini Tanzania.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sinema hizi tumeshazizoea..sterling yuleyule na picha ni ileile.
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  hakuna courage yoyote huyu kadandia basi kwa mbele hiyo ni janja ya nyani kula hindi bichi;uchaguzi umekaribia
   
 6. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hizi kelele za chura zitamtoa nyoka pangoni siku moja. Naamini moto ukiendelea hivi, basi mabadiliko ya kweli yatakuja very soon. Tusiache kupiga kelele jamani. Wabunge kama hawa na wengine wengi wanaojitokeza hadharani kukemea rushwa, ufisadi na maovu mengine, wanatupa imani kwamba kuna siku haya mambo yatafikia ukomo. It takes great courage kumface Hosea uso kwa uso na kusema kwamba taasisi yake imedorora. Not from a CCM MP. Angekuwa ni Silaa au Zitto, nisingeona issue, lakini anapokuwa ni MP wa CCM, basi lazima tumpe credits zake. Well done Mpendazoe.
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  First lady, vyovyote vile lakini jamaa kamkoma nyani live! Bravo Mpendazoe, we need more of you!
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  It is unfortunate that Mpendazoe is a marked legislator among those whom the " papas " want to eliminate in the coming general elections! Hata hivyo maneno yake ni ya hekima ambayo intelligent Tanzanians should embrace. Tatizo letu kubwa liko kwenye katiba na kama nilivyowahi kuandika huko nyuma kama kweli tunataka mapinduzi ya kimaendeleo nchini mwetu ni lazima tupigane kufa na kupona constitution yetu iwe revisited because it is not cast in Stone! Vinginevyo hawa wahuni watakuwa wanatumia hovyo maliasili ya nchi yetu bila kuthibitiwa.
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yes they can eliminate him from their chama cha mafisadi, but if he stand firm and did his home work to serve his wananchi this term, he can join another party, or stand as mgombea binafsi if that will be allowed and throw them away!

  Haka ka ugonjwa kakuogopa kutemwa na chama cha mafisadi ktk kura za maoni kamewaharibu wabunge wengi wa Chama Cha Mafisadi tulio wategemea kwamba wange fanya jambo kuiadabisha na kuisaida serikali!

  Matokeo yake wamebaki kupiga meza na kushangilia ujambazi ulio wazi!, Lakini Mungu atasaidia tu wadanganyika waamuke na kuwa wajibisha coming 2010!
   
Loading...