Mbunge amrushia Spika bomu la machozi

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,375
3,655
Mbunge wa upinzani kutoka nchini korea ya kusini amemrushia spika bomu la machozi baada ya bunge hilo kupitisha hoja ya biashara huria kati ya nchi hiyo na marekani
 
Ndiyo hivyo, jamaa alizidiwa na hasira!! Hali hewa ilichafuka kila mtu kivyake. Keshaonyesha njia!
 
Mbunge wa upinzani kutoka nchini Korea ya kusini amemrushia Spika wa bunge bomu la machozi, baada ya bunge hilo kupitisha hoja ya biashara huria kati ya nchi hiyo na Marekani.

Mbunge huyo wa upinzani aliyefahamika kwa jina la Kim Sun-dong alionekana kukasirika mara baada ya Bunge hilo kupisha hoja hiyo iliyokua imetawala bungeni kwa muda mrefu. Habari zinaeleza kwamba alirusha bomu hilo dakika chache baada ya kura za kupitisha hoja hiyo ya kufanya biashara huria kati ya nchi hiyo na Marekani.

Baada ya bomu hilo ambalo lilielekezwa katika kiti cha Spika wabunge wote walionekana kupata taabu ya kudhurika na moshi huo wa bomu na aliyeadhirika zaidi ni Spika wa Bunge hilo ambaye alishindwa kuvumilia kabisa baada ya tukio hilo. Habari zilizidi kusema kwamba Spika alilazimika kuamuru mbunge huyo awekwe chini ya ulinzi na walinzi waliokua eneo hilo la bunge kutokana na kitendo hichocha uvunjifu wa amani. Baada ya tukio hilo wabunge walishindwa kuvumilia na kuanza kutoa machozi huku wengine wakitoka nje ya ukumbi huo wakiwa wanapiga makelele. Tusubiri Bunge linalokuja hapa kwetu Tanzania.
 
jamani haya sio mambo ya kufurahisha eti,ni bunge la aina gani hilo mbunge anaweza kuingia na bomu bungeni,mbona hiyo ni kashfa kwa vyombo vya ulinzi na usalama!
 
ibara ya 10 kifungu cha 2 cha katiba mpya kiweke namna ya kumtupia spika wetu kiti labda kitendo hiki ndio kipaumbele chetu kwa sasa
 
mods, tunaoomba uweke kifungu cha Jf cha kutupiana kiti hapa Jf endapo member mmoja ataona inafaa kutupa kiti kwa yule ambaye wanatofautiana msimamo kama kule korea. katika mjadala huu ningeshawatupia viti wawili
 
kwa hiyo mbunge huyu alikuwa tayari analo bomu kibindoni, alishapanga kutekeleza!.....this is aden rage ccm..type kupanda na bastola jukwaani!
 
kwa hiyo mbunge huyu alikuwa tayari analo bomu kibindoni, alishapanga kutekeleza!.....this ia aden rage ccm..type kupanda na bastola jukwaani!

this is Dr slaa chadema type alipokutwa katikati ya spika kule Arusha akiwa na bastola na risasi 17
 
Back
Top Bottom