Mbunge aliedai Wahudumu wa ATCL hawana mvuto aomba Radhi Bungeni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1573720206898.png

Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Mhe. Husna Mwilima leo Bungeni ameomba radhi shirika la Ndege ATCL na Watanzania waliokwazika na kauli yake aliyosema Bungeni tarehe 7/11/2019 kwa kusema Wahudumu wa Ndege ya ATCL (Air hostess) hawana mvuto.

“Nataka nitanie kidogo, hizi ndege zetu zinafanya kazi nzuri lakini mle ndani hebu tuangalie wahudumu tunaowaajiri, tuangalie wahudumu ambao hata akigeuka abiria wanasema kweli tuna Air Hostess, sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta Air Hostess mfupi, hana mvuto,” Alitoa Kauli hiyo Alhamisi Novemba 7, 2019 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo bungeni jijini Dodoma.

Leo November 14, 2019 ameomba radhi bungeni na kusema; “Nilitoa ile kauli lengo lilikuwa ni kuboresha shirika letu la Ndege la ATCL, kwa kuwa ile kauli yangu iliwaboa sana Watanzania hasa wanawake nitumie nafasi hii kuomba radhi Watanzania hasa wanawake wenzangu"

-Mpekuzi-
 
Binafsi nilishamsamehe tangia siku ya kwanza kwani najua ni kawaida Wanawake huendeshwa na emotions, shida ni Wanaume ambao wako kama yeye, hao ndo hushindwa kuwaelewa, huyo ni Mwanamke inawezekana hata sababu ikawa ni wivu tu labda alipanda ndege akazinguana na mfanyakazi mmoja akafura na kusema aliyosema, Wanawake siyo watu stable, nashangaa watu wanavyowatanguliza mbele kwenye mapambano yao.
 
“Nilitoa ile kauli lengo lilikuwa ni kuboresha shirika letu la Ndege la ATCL, kwa kuwa ile kauli yangu iliwaboa sana Watanzania hasa wanawake nitumie nafasi hii kuomba radhi Watanzania hasa wanawake wenzangu"
Mwenyewe ana uzuri gani amenenepeana kama kitimoto, halafu kavaa wigi! Rangi ya mdomo utadhani naniliu bhana! Go to hell
 
Tusichojua ni kwamba ropoka ropoka yetu ya maneno

ulimwengu wa roho yanakuaga hapo juu yanaelea tu

mwanao/mjukuu yatampata tu kama hautotubu kweli kweli

ukayafuta.
 
Kurzweil, Tulijua tu sijui awa viti maalumu wanapatikana kwa vigezo gani.
Hilo neno maanake utamkuta mbunge ana maziwa hayo makuuubwa huku kichwani akili ya kufikiri ni kipi Cha kuongea na kipi so Cha kuongea kichwani hakuna, sijui hivi vyama vya siasa vinatumia vigezo gani kuwachagua.
 
Hapa tunaona jinsi wananchi walivyo na uwezo wa kuwajua viongozi wabovu na wazuri, huyu mama wananchi walimkataa lakini 'mamlaka' zikalazimisha ndiye awe mwakilishi wao.
Sasa jiulize ni wabunge wangapi au watendaji wengine ambao wanafanya maamuzi lakini ni type ya huyu!
 
Tunakuelewa ulitaka wahudumu wa wenye 'derierre' ya kiafrika ila kwenye ile fani hiyo hawafai maana hata kupishana kwenye aisle ingekuwa taabu.
 
Huyu bibi ametumika kimwili kwa kigezo cha uzuri sasa anataka watoto wa watu nao wawe vivutia macho wakaburudishe wateja kama yeye alivyo burudisha mpaka akafika hapo alipo fika maskini, uzuri nae ni mwanamke na nadhani amezaa mabinti, awapeleke sokoni hao wakaburudishe wateja huko... Hawa ndio wabunge wa ccm na hizo ndizo kero za wana jimbo lake??? Hao wanajimbo hata robo hawapandi ndege..msweee.
 
WANASEMA MTU MZIMA AKIOMBA RADHI ANASAMEHEWA

YANAYOENDELEA N UMBEA
NASHAURI NA KF MTOE YALE MAPOST MH AMEJITAMBUA ALIPOKOSEA ATUITAJI KUYAONA TENA
AHSANTENI
Screenshot_20191114-153508.png
Screenshot_20191114-153433.png


YALIOPITA SINDWELE TIGANGE YAJAYOOO
 
Back
Top Bottom