Mbunge Abood akabidhi hundi ya Tsh. 1,000,000/- kwenye Kongamano la Women Suporting Women 2023

Oct 8, 2023
37
17
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Mhe. Abdulaziz M Abood, 22/10/2023 Amekuwa mgeni rasimi kwenye kongamano la Women Supporting Women 2023 lililoandaliwa na Moro Super Women Present.

Mhe. Abood alipokelewa kwa shamlashamla, ndelemo na vifijo. Baada ya mapokezi msafara uliingia ndani na mgeni rasimi alifika meza kuu na kuketi, ziliendelea ratiba mbalimbali ikiwemo michezo na burudani kutoka kwa wakina mama hao. Baada ya michezo ulifika wakati wa risala kusomwa wakati wa risala Mhe. Abood alikuwa makini sana kuisikiliza, risala ilikuwa na vipengeli baadhi kama vile; malengo ya kikundi na changamoto za kikundi.

1) Malengo - Malengo ya kikundi ni pamoja na kujikwamua kibiashara kwa kukopeshana, kushauliana na kupeana furusa za biashara, kutembelea mashuleni ili kutoa Elimu ya afya kwa mabinti na nk.
2) Changamoto - Changamoto kubwa ni ukosefu wa mtaji wa kutosha ili kuweza kukopeshana wao kwa wao.

Mhe. Abood alipokabidhiwa risala alianza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uzima na afya waliyonayo, pili alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitiada zake za kuwaletea maendeleo Wananchi.

Mhe. Abood akijibu risala yao kwanza amewapongeza kwa uthubutu waliyonao na kuwasihi waongeze juhudi, Mhe Abood amekabidhi hundi ya Tsh 1,000,000/- (milioni moja) ili kuwaongezea mtaji kwenye mfuko wao.

Baada ya kumaliza risala Mhe. Abood amepata muda wa kuzungukia biashara za wajasiliamali walizokuja nazo kwaajili ya kuonyesha biashara zako kwenye kongamano hilo, aidha Mhe Abood alinunua biashara zote za wajasiriamali lengo ikiwa ni kukuza mitaji ya wajasiriamali hao.

Vilevile Mhe. Abood aliwapa ofa wajasiriamali hao ya kutangaza biashara zao bure bila malipo yoyote kwenye vyombo vya habari vya Abood Media yote ikiwemo Radio (Abood FM), Television (Abood TV na Mnitandao ya kijamii kama (Abood Media TZ) hii yote ikiwa sehumu ya kuwaungamkono wajasiriamali hao.

20231022_203523.jpg
IMG_20231022_150212_745.jpg
 
Kaka Ishengoma najua umeandika ili kumpromote boss wako Abood ila nakusihi ukiwa humu usiige tabia za Lucas Mwashambwa na kundi lake, wanajidhalilisha sana humu.
 
Machache kati ya mengi ya ku-take note:-

1. Kongamano la Women Support Women.
2. Mh. Abood (Mbunge wa Moro) alialikwa.
3. Kuwasaidia Wanawake wajasiliamali. alichangia kiasi cha tshs. Million moja
4. Alinunua bidhaa zote zilizoletwa na wajasiliamali.
5. Pia alitoa ofa kwa wajasiliamali kutangaza bidhaa bure katika vyombo vyake vya habari.

Hongera kwa wajasiliamali na kongole kwake Mh. ABOOD kwa kuwajali wajasiliamali, this is the win win situation.
 
Back
Top Bottom