Mbu wa Muhimbili

Mbu wa Muhimbili

Nakumbuka kipindi kile enzi za Ngozye alijaribu kupiga dawa lakini wapi..usiombe iwe siku yenu ya usafi class yaani ile asubuhi kuna mbu unaweza jaza gunia za kilo 100 mbaya zaidi ukifika forest hasa kule kitengo mawe mbu wanapiga misumali hadi mchana
nimecheka balaa
 
Kuna wakati niliwahi kuwaza kuwa kuwa tuchimbue na kuzamisha kina cha mto 1. Msimbazi tuunganishe na Bahari kupitia pale Salender Bridge, tujenge ukuta pale daraja la salender lenye Geti, maji yakija (kujaa) tuyaruhusu kuingia na ya kiondoka (kupwa) tunafunga turbine ya umeme hapo na tunafungulia maji yanaanza kuzungusha turbine na tunapata umeme rafiki kabisa.
2. Pia tunaweza kuyafungia huku huku juu bila kuyaruhusu maji hayo wakati wa kupwa , sasa mto uliosafishwa na wenye kina ukatumika katika utalii kwa kuweka boti humo watu wanazunguka kutoka salender, muhimbili, jangwani...tunaweza tukatanua hilo bonde mpaka kigogo...! NA hapa serikali ikapata ela ya kuboresha miradi ya maendeleo kwa watanzania wote.
3.Twaweza pia, kuhakikisha maji taka yote tunayapitisha kwenye bomba moja kubwa na yakamwagwa kilindini huko bahari, na hakuna mtu wala kiwanda kutupa taka kwenye mto huo bira kupitia bomba hili. sasa tukiwa na maji ya mto safi tunaweza kufuga samaki humo, tukawa na uhakika kabisa wa kitoweo safi.

Kupanga ni kuchagua.
Kesho saa tatu asubuhi nakuomba ufike ofisini kwa RC tafadhali ukiwa umejipanga vizuri kufafanua hii idea yako,ukifika ni PM
 
Hawa wa hapa Muhimbili ni kama wamekuwa biologically modified kama sio specie tofauti na nyingine.

Mbu anatoboa hadi turubai..!!
Nawajua hao mbu ogopa usikutane nao siku wameamua kula bata yani kunywa damu za visitors sio wagonjwa yani mbu ananyanyua jinsi mwenzie ananyonya then anampa mwingine
 
Kesho saa tatu asubuhi nakuomba ufike ofisini kwa RC tafadhali ukiwa umejipanga vizuri kufafanua hii idea yako,ukifika ni PM
Asante kwa wito na nashukuru kwa kuona umuhimu wa idea hizi.

Bahati mbaya sana niko mbali na maeneo hayo siwezi kufika kwa muda huo. Hata hivyo, idea hizi sijaziwekea haki miliki bali haki miliki ipo mikono mwa serikali ya nchi yangu Tanzania maana nataka tunufaike watanzania wote. Kwa maelezo hayo, ideas hizi ziko huru kufanyiwa kazi tu na wataalamu wa serikali yetu ya Tanzania pekee. Maana nadhani ideas zote tatu wakikabidhiwa wahusika (wataalamu) kwenye wizara za ujenzi, nishati na mazigira(wazo la 1); wizara za utalii,mazingira, ujenzi na uchukuzi (wazo la 2), na wizara za uvuvi, ujenzi na mazingira (wazo la 3) wanaweza kabisa kufanyia kazi haya wakishirikiana na RC.
 
Nawajua hao mbu ogopa usikutane nao siku wameamua kula bata yani kunywa damu za visitors sio wagonjwa yani mbu ananyanyua jinsi mwenzie ananyonya then anampa mwingine
Halafu mbu wale hatari wana act kufa kama mbung'o( tsetsefly) ukijitingisha...kisha wana nyanyuka wanaendelea na kazi!!!
 
Back
Top Bottom