Mbowe; wengine tuna masikio ila hatujasikia ulichosema

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,338
4,672
Nitatumia mchanganyiko Wa mantiki mbalimbali ili nieleweke.Ni kweli Magufuli anayo historia ya kuchukua maamuzi ambayo baadaye huleta athari.Umezitaja athari sitaki kuzirudia.CDM muliwahi kuitisha maandamano sehemu mbalimbali nchini yenye lengo la kukomboa watu kifikra.Kuwapa Uhuru Wa kuhoji kwa ajili ya maisha mapana ya nchi yetu.Hiyo ilikuwa sura moja ya matokeo.Sura nyingine ni kwamba baadhi ya waandamanaji walipoteza maisha.Hata huo Uhuru hawakufaidika nao! Hawakuonja matunda yaliyodhamiriwa.

CDM tulimwacha Dr.Slaa kwa sababu tulimpata ndugu yetu Lowasa atusaidie kwenye mpango Wa kuokoa Taifa letu toka mikononi mwa Majahili CCM.Hiyo ilikuwa sura moja.Nyuma ya sura hiyo Dr.Slaa "akapotea" physically japo tunaye kiasi Fulani kwa njia za kisasa za mawasiliano.Je,hiyo inawafanya CDM kuwa chama cha hovyo na kinachopaswa kutoaminiwa?

Mungu aliumba mema.Akampa mwanadamu Uhuru Wa kujiamulia mambo(free will).Uwezo Wa kuchenjua mema na mabaya.Hiyo ilikuwa sura moja ya mpango na utekelezaji wake.Nyuma ya sura hiyo mwanadamu aka-opt kukubali pendekezo la Shetani kwamba mwanadamu anao uwezo Wa kuwa sawa na Mungu kwa kila kitu(causally uncreated Creator).Je,Mungu kwa uamuzi huo Wa kumpa mwanadamu free will haifai?Amepoteza credibility?Je,Mungu sasa ni mwenye historia ya maamuzi angamizi kwa wanadamu?


Yesu akaja kutuokoa.Akazaliwa na mwanadamu mwanamke.Hiyo ilikuwa sura moja ya mpango na utekelezaji wake.Nyuma ya sura hiyo watu wakampokea kama binadamu mwenzao tu na asiye na lolote.Vijana wenzie wakamwona kama "msela" mwenzao tu tena "mpiga fungi" mzuri tu maana alijumuika nao kule harusini Kana tena kwa kuongeza chupa za bia baada ya zile zilizokuwa zimeandaliwa na Kamati ya harusi kuishia.Zaidi ya yote wakamuua.Lakini pia akawa amesababisha familia za baadhi ya Mitume kama Petro,Paulo, Yohane na wengineo kuparaganyika na kuacha wajane baada ya hao Mitume kuuawa.Je,Kwa matokeo haya Yesu Kritu haifai kusikilizwa na kuaminiwa tena kwa lolote?

Sasa Ndugu yangu Mbowe unajaribu kutuambia nini juu ya Magufuli? Kwamba ile barabara iliyokuwa inajengwa ikapelekea Serikali kudaiwa fidia kubwa ilikuwa mahususi kwa matumizi ya Magufuli? Kwamba ile Meli aliyoikamata na kisha ikatugharimu ilikuwa inavua samaki kwenye Bahari ya Magufuli? Kwamba watu waliofukuzwa na Vyeti feki walikuwa wanatumikia familia ya Magufuli?

Mimi na baadhi ya watu tuna masikio ila "hatujakusikia sawa sawa"! Kwamba katika chaguzi zilizopita mlikuwa munamusaidia Odinga wakati huo huo alikuwa rafiki yake Magufuli na haikuwa nongwa.Na wakati huo huo Magufuli alikwisha kutusababishia hasara za Fidia ya Barabara na Meli na haikuwa nongwa! Kwamba leo Odinga ameendelea kufanya ushirika na Magufuli akiwa Raisi sasa ni nongwa na mumemuhama na sasa "mshikaji" wetu ni Uhuru Kenyata! Uhuru kazaliwa leo? Kwamba tulimsapoti Odinga kwa sababu ambazo leo hazina mashiko tena? Kwamba tunamsapoti Uhuru kwa sababu Odinga ana ushirika na Magufuli ambaye sasa ana "laana" za vilio vya Vyeti feki na kuzuia Makanikia na hivi mkiendelea kumsapoti hiyo laana itamfuata Odinga na hivi hataweza kushinda uchaguzi?

Nina maswali mengi sana! Lakini nihitimishe tu hivi: siasa hizi ni siasa za namna gani? Je, unaposema ni heri wengine wenu mpotee lakini lazima Taifa lipone unamaanisha nini?Kwa nini kama kuna uwezekano tusipate matokeo yote mawili chanya kwa wakati mmoja? Kwamba Taifa lipate faida kwa kumupinga Magufuli na wakati huo huo asipotee mtu? Ikiwa wengine "wataondoka" kama ulivyosema ili kuponyesha Taifa,CDM itakuwa imejitofautisha vipi na Magufuli na maamuzi yake magumu yenye historia ya kuliumiza Taifa?Hebu naomba Unifanye masikio yangu yasikie na yasikie.
 
Usimuhusishe Mungu na mambo ya siasa ndugu yangu.tena koma kabisa hiyo tabia usiirudie nakusihi kwa sauti ya upole tu,si busara hata kidogo
 
inawezekana ulikuwa na hoja nzuri lakini umejichanganya sana kwenye andiko lako.
pia kumbuka tunao viongozi waliojipachika uwezo wa Mungu.
 
Usimuhusishe Mungu na mambo ya siasa ndugu yangu.tena koma kabisa hiyo tabia usiirudie nakusihi kwa sauti ya upole tu,si busara hata kidogo


Wewe mwenzangu maudhui uliyoambulia katika hoja yangu ni kwamba mimi nimemuhusisha Mungu na yasiyomhusu? Wewe wala usikonde na ukapata vidonda vya tumbo bure kwa kunionya acha Mungu aifanye hiyo kazi mwenyewe.Onyo lako linaweza lisiwe na makali sana kama la kutoka kwa Mungu mwenyewe.Kufuru iko wapi katika mfano wangu uliomhusisha Yesu na Mungu? Sijapata shida maana wewe unasoma maandiko Matakatifu kama Novel.
 
inawezekana ulikuwa na hoja nzuri lakini umejichanganya sana kwenye andiko lako.
pia kumbuka tunao viongozi waliojipachika uwezo wa Mungu.

Nisaidie kujichanganya kulikotokea.Kama nilivyosema katika hoja yangu kuwa kila jambo lina pande mbili katika matokeo yake.Unafanya ukilenga upande chanya ila upande hasi lazima utokee kwa namna Fulani.Na ikitokea hivyo upande hasi uchukuliwe kama fursa na sio kikwazo.Yumkini kuna udhaifu katika mawasilisho ya hoja yangu lakini maudhui ni mema.Na udhaifu huo umekuwa fursa kwako kuibuka.Bila hiyo sura ungeibukaje?
 
Maamuzi ya mbowe kumfukuza Dr slaa yana mpango gani??, na hili la kumpa heche sumu kisa amempinga Masha kuwa mgombea EAL linafaida gani??
 
Chadema yamewafika shingoni, nawashauri siku nyingi wakitaka kufanikiwa wampe wema ukatibu mwenezi au achukue nafasi ya mashinji ambaye kapwaya sana. Wema mambo ya kueneza anayaweza
 
Back
Top Bottom