MUSSA ALLAN
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 18,925
- 13,280
CCM nanyi toeni tamko kuwa hamtaiba kura za wapinzani...
Kiongozi ambae anawaza kwa kutumia miguu ni Freeman Mbowe,amekua kila mara akisema kura hazita ibiwa lakini baada ya matokeo ana mtuma Dr Slaa aseme kura zili ibiwa
CCM nanyi toeni tamko kuwa hamtaiba kura za wapinzani...
CCM nanyi toeni tamko kuwa hamtaiba kura za wapinzani...
Kamanda, nadhani umesahau kuwa CHADEMA kupitia Red Brigade huwa wanakesha nje ya vituo vya kuhesabia kura mpaka matokeo yatangazwe, na huko ndani kwenye uhesabuji CHADEMA wana mawakala wao!..
Kama kura zinaibiwa na majini, sawa, ila kwa namna ya kibinadamu hakuna kura ya CHADEMA iliyowahi kuibiwa!
Mkuu makamanda mwaka huu hawatoki, kila mara wanajidai wanaibiwa kura, lakini sasa wameshajifunga wenyewe kuwa kura hazitoibiwa tena, kwahiyo Single ya kuibiwa kura ndio imefia hapa, tunasubiri waje na kisingizio kingine cha kushindwa!
Umeshasema ni wapinzani, hakuna aliyewahi kuja na ushahidi unaojitosheleza kuwa kura ziliibiwa, wengi wao ni porojo tu baada ya kukataliwa na wananchi.Mkuu si CDM pekee wanaolalamika kuibiwa kura bali imetokea kwa CUF na hata NCCR Mageuzi kipindi kile cha Lyatonga...
Halafu uzoefu unaonesha kuwa majimbo yote ambayo wapinzani huwa wakali na wizi wa kura huwa wanafanikiwa...
Wewe jichekeshe tuu, style itakayo tumika ni kama ile uliyoiona kutumika leo kule Monduli ya kumtoa mtu kwa nguvu ambaye hakuchaguliwa na kumweka aliyechaguliwa kwenye kiti huku Polisi wakishuhudia. Au kama yale ya Migombani Segerea na kwingineko kama kile kipigo cha pale Land Mark hotel ambako mwenyekiti wa kuchonga alipokuja kuapishwa aliishia kujificha kama Gadaffi kwenye Kalavati na kurudi kwake kavaa shati vipande vipande.
Kama mmeamua kuwa hamtoki bali kwa mabavu basi mtaona itakavyo kuwa.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kimejipanga kuhakikisha katika uchaguzi Mkuu hawaibiwi kura.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati akizindua mafunzo ya Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha chama hicho (Red Brigade), kwa vijana 200 wa Kanda ya Kati pamoja na Kikosi maalum cha Karate.
Katika uchaguzi huu hatutaki kulalamika tena kwamba tumeibiwa kura na tutahakikisha tutaomba kura kwa wananchi na tutazilinda, alisema Mbowe.
Alisema endapo watakubali kuibiwa kura maana yake hawapo tayari kuongoza. Mbowe aliwataka vijana hao wa Brigade kutokukilinda
chama peke yake bali pia kiwe chachu ya ulinzi kwa jamii inayowazunguka kwenye maeneo yao.
Alibainisha kuwa Chadema kitaendelea kutoa mafunzo ya ulinzi kwa vijana nchi nzima. "Vijana hawa lazima wajenge moyo wa kujitolea, chama kilijengwa na watu wenye moyo huo ambao baadhi walipata madhara mbalimbali ikiwamo kupoteza maisha, alisema Mbowe.
Alisema wajenge sifa ya kuwa wakombozi wa Taifa na malipo mengine siyo lazima walipwe hapa duniani bali watapata kwa Mungu
CHANZO: NIPASHE.
=======================================================================
Mbowe amekuwa akiwaaambia wafuasi wa CHADEMA kila uchaguzi ukaribiapo kuwa hakuna kura zitakazoibiwa, lakini uchaguzi unapopita tu, na CHADEMA kushindwa kwa kishindo, Wimbo wa kuibiwa kura unaanza tena.
Mbowe sasa uwahakikishie wafuasi wako kwa dhati kabisa kuwa mwaka huu hatutasikia ngonjera za kuibiwa kura baada ya uchaguzi.