Mbowe: Tutashika dola kirahisi 2015

mwanakijiji ameshakuwa mmarekani,anarusha smart bombs tokea cleveland,ohio,anaogopa vita ya ardhini!!

Hauwezi ukajipa jukumu la kuangalia wenzako wanafanya nini alafu ukakosa cha kukosoa.
 
Mchambuzi:
Unapotoka unaposema Chadema inavuna wanachama 5Mil wa CCM, kwani wanachama na mashabiki wengi wa Chadema, hawaijuhi na wala hawajawahi kuwa CCM na kwa mpango ni kuwa Chadema ina Recruit vijana waleo, kizazi cha 90's ambacho hakijuhi CCM ni nini zaidi ya kuwa CCM ni Janga.
Labda cha kuwashahuri Chadema ni kuhakikisha elimu ya kutosha inafika kwa hawa vijana kwa ajili kuhakikisha siku ya kupiga kura wote wanajitokeza kupiga na kulinda.
 
Kwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?

Mzee Mwanakijiji najua kuwa wewe si mvivu wa kufikiri, kwa msingi huo, tohoa tafadhali kwa ulinganifu wa matukio kufikia hatua ya kuaminiwa ama kutokuaminiwa ya wamarekani/kimarekani na yetu nitakayoyateua:-
1) Ni baada ya Gen. Collin Powel "mwafrika" kuwathibitishia pasipo shaka "wazungu" wa marekani kwamba waafrika wanaweza alipoweza kwa mafanikio makubwa kuwa rubani mahiri hatimaye kukabidhiwa na Bush senior kuchora raketi ya vita vya ghuba,

2) harakati za kuzingua zilizofanywa na shonza, mwampamba & co. ndani ya harakati wakiwa miongoni mwa wanaharakati kuudai uhuru unaohitajika zaidi sasa kuliko wakati mwingine, huku wakifanya kazi za malware kuderail move ya ukombozi wakiwa embeded fighter wa jeshi la upinzani (ccm)

kama umenielewa vizuri mifano yangu ukiisha kuijadili tupe fikara zako, ni muda gani tuutumie kumchunguza askari wetu kabla ya kumuamini kumkabidhi Arsenal ama angalau B52 ashambulie kwa mfano kanda ya kati.

n.b adui (ccm) ana majeshi ya kukodi nayo ameyatapakaza haiyumkini miongoni mwetu.
 
Last edited by a moderator:
Katika wakati mgumu kama huu cdm inabidi kuangalia ni jinsi gani inapunguza madaraka toka kwa viongozi waliopo kama kina Mnyika. Wakati huo huo ijipange kuona ni jinsi gani inatafuta viongozi wapya na wakaandaliwa kwa namna ambayo hawatakuwa na madhara katika mchakato wa kuendea kushika Dola.

Wako wanachama ndani ya chama na ni wa muda mrefu tu. Hao wapikwe kwa kozi kwa maandalizi ya kufikia lengo. Hii tayari imeshakuwa ni pigo kwa ccm hivyo umakini ni muhimu mno.
 

Mchango mzuri sana, CHADEMA, CCM chukueni hii mjenge juu yake. Hapo tutakuwa na kampeni nzuri sana
 
ndiyomkuusana naomba tofauti ya sera za majimbo na sera za CCM za upelekaji madaraka mikoani; uanzishwaji wa serikali za mitaa na kitu wanachoita "D by D"
 

Ukisoma gazeti la Mtanzania la Jana utabaini propagander inayopigwa na watu wa CCM dhidi ya Serikali inayotawala ni kali zaidi ya inachoweza kufanya CDM, the war within CCM kwa sasa imefika kwenye hatua mbaya, hii inaifanya CDM kushika nchi huku wanakunywa chai
 
Hizi kauli wanasiasa wa Afrika wamezoea sana kuzitumia ili baada ya uchaguzi wapate justification ya kusema wameibiwa kura. Yaani leo anatoa kauli kuwa ana uhakika wa ushindi halafu baada ya uchaguzi akishashindwa anatumia yake ya awali kuthibitisha kuwa alishinda ila ameibiwa kura. Kwa vile wafuasi wengi hawakai chini kuchuja, wanabeba maneno hayo na kuamini kuwa chama chao kimedhurumiwa.
Hii ni sawa na wale fanatics wanaoamini kuwa Wilbroad Slaa alishinda uchaguzi wa mwaka 2010, ukiuliza vigezo wanatumia kauli za huyohuyo mwanasiasa!!!!
 
nyie ccm mjiulize kama 2010 mligawana kura na wapinzani tena hazikutosha nye kwa hii miaka mitano mmeboreshaje maisha ya watanzania mpaka muje kukubalika tena..? nyi mkishindwa uchaguzi hamtakubali kuachia madaraka kwa fikra zenu mgando mlizonazo!
 
wanachofanya cdm ni sahihi kabisa, bado mapema, baadhi ya watu hawaaminiki na kadiri muda unavyokwenda ndivyo watu watazidi kujuana zaidi. Hebu fikiria wangekuwa wameshapewa nafasi nzito akina shonza ingekuwaje mbele ya safari? Na akina shonza wako wengi tu ndani ya upinzani. Hatua kwa hatua tutafika.
 
Vyeo vinavyotolewa kwa kujuana kuna vetting gani?Yale yale ya rubbe stamp tu.
Wakati mwingine watu msiishie tu kulalamika na kupiga majungu mitandaoni.
Mtu hajaonesha jitihada zozote za kukipigania chama, naye anataka apewe madaraka from nowhere.
Ndo yale yale ya akina Shonzi et al.
 
Kwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?

MM ni heri hao wenye nyadhifa tayari wanajulikana kuliko kuweka watu wapya,unaweza kuta umejaza
wasaliti"
 
Mkuu Mchambuzi you are right in one way, wrong in another.

Kampeni zote, yaani ku-recruit wanachama wapya (ikiwemo kuchukua wale wa ccm ili kuidhoofisha) na kuelimisha wale swing voters ili waiamini chadema inabidi ziende sambamba. Na nina imani ndicho wanachokifanya chadema kwa sasa.

Kwa muda uliobaki sasa kufikia 2014/2015 huwezi ukaenda na kampeni moja moja kwani muda utakuwa hautoshi. Afterall unapofanya mkutano mahali popote unakuwa na watu wa aina zote hizo mbili ulizozitaja kwa hiyo ni vema kupiga ndege wawili kwa jiwe moja.

Kuchukua wanachama wa ccm ni muhimu kwani ni mahesabu ya ki-accounting yaani una credit kwako na ku-debit kwa adui yako. Wakati huo huo unabeba na wale wanachama ambao ni swing voters. Hii ni muhimu sana.

Unapokuwa na wanachama wengi unakuwa umeongeza wigo wa watu wa kukusemea, yaani kutangaza itikadi yako kwa wengine ambao ni "undecided". Hili ni muhimu sana.

Unapofika uchaguzi unakuwa na kazi ya ku-brush kidogo tu kwani kazi kubwa inakuwa imeshafanyika huko mitaani.

Kutegemea ku deal na swing voters pekee ni hatari kwani hawa wengi wao huwa wanabadilika kutegemea na upepo unavyovuma.
 
Ni vizuri kujua nia ma dhumuni ya chama chochote cha siasa Duniyani ni kutaka kuchukua au kuongoza Doula. Hivyo Mbowe ana haki zote kutamka hivyo kwani ndio dhumuni lao la kuunda chama chao.

lakin uhalisia inabidi ajipime je itawezekana?

Tombe mola tuone 2015.
 
Ni kweli dola siku hizi zinashikwa kirahisi
$1 , $10, $100 zote zinapatikana kirahisi .
 
MM ni heri hao wenye nyadhifa tayari wanajulikana kuliko kuweka watu wapya,unaweza kuta umejaza
wasaliti"

Mpaka lini?
Kila mzazi anapenda mtoto wake wa kike abaki bikira mpaka wakati anaolewa, sio rahisi kiivyo. Jukumu la kukilinda chama lipo mikononi mwa wanachama na si viongozi peke yao ni vizuri kuwa na imani na wenye chama kuwa hawawezi yumbishwa na mamluki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…