Mbowe: tunajiandaa kuchukua nchi

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2][/h]


Na Hellen Mwango



30th April 2012











Mbowe(46).jpg

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kinajipanga kuchukua dola mwaka 2015 na kwamba ndoto ya Watanzania iko karibu kutimia kutokana na tishio la hali ngumu ya maisha inayosababishwa na mfumuko wa bei za vyakula nchini chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kadhalika Chadema kimesema ili kuikamata dola mwaka 2015, chama hicho kina mkakati mkubwa wa kusisitiza nidhamu kwa wanachama wake wote nchini itakayowapa imani wananchi wakati wa kushika dola.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam.

Alisema ajenda kubwa ya mkutano huo ni kujipanga kuhusu namna ya kushika dola mwaka 2015 sambamba na nidhamu kwa wanachama wote itakayowapa imani Watanzania wakati wakiwa madarakani.

Alisema serikali iliyopo madarakani ina matumizi makubwa ya anasa na kusababisha upungufu wa fedha huku wananchi wakilia kwa ugumu wa maisha.

“Ndugu wajumbe ajenda kuu ya mkutano huu tunajipanga namna ya kushika dola mwaka 2015 pamoja na kuimarisha nidhamu katika chama ili wananchi wawe na imani na sisi... hali ya wananchi ni mbaya sana, mfumuko wa bei ya vyakula haukamatiki uko juu na wanashindwa kumudu maisha kutokana na serikali iliyoko madarakani kujali matumizi ya anasa ya vigogo wake,” alisema Mbowe.

Alisema serikali ya CCM imechanganyikiwa na inashindwa kutimiza majukumu ya msingi, ikiwemo kuwatimizia wananchi mahitaji ya msingi pamoja na kupunguza mfumuko wa bei.

“CCM watupishe Chadema tuingie Ikulu kuwatumikia wananchi, mara ya pili sasa Baraza la Mawaziri linavunjwa tangu Rais Kikwete aingie madarakani. Watupishe jamani,” alisema Mbowe huku akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.

MAUAJI YA WANACHAMA

Akizungumzia mauaji ya wanachama wa chama hicho kwa sababu ya kuwa mstari wa mbele kulinda haki na kwamba mauaji hayo yametokana na nguvu ya dola kuingilia kati.

“Katika chaguzi ndogo zilizofanyika Igunga, umeya wa Manispaa ya Arusha mwaka jana na sehemu mbalimbali nchini wamekufa wanachama wetu 16, na mpaka sasa hakuna aliyechukuliwa hatua yoyote za kisheria ... sisi Chadema tunasema CCM wapo kwenye jumba la vioo kwa hiyo wasianze kutupa mawe nje,” alisema.

Aliongeza: “Godbless Lema amepoteza ubunge kihuni japo mahakama ni chombo cha kutenda haki na tuna imani nayo, lakini tuko tayari kurudia uchaguzi na tutashinda tena Jimbo la Arusha Mjini kwa kura za aibu ... heri mtu ufe umesimama kuliko kufa umepiga magoti kwa aibu.”

KATIBA MPYA

Kuhusu Katiba Mpya, Mbowe alisema wabunge wa chama hicho waliibua suala hilo, lakini awali walibezwa na kutukanwa kwa sababu haikuwa ajenda ya CCM ya kubadili Katiba, lakini mwisho wa siku serikali ilikubaliana nao.

Alisema chama hicho kitatoa maelekezo kupitia vipeperushi kwa wanachama wake nchi zima vitakavyoeleza madai gani ya msingi wanayotaka yaingie kwenye katiba mpya.

“Kuhusu Katiba Chadema tutajadili tunavyotaka pamoja na kutoa elimu ya kutosha ili tuwe na sauti moja ikiwemo kupiga vita rushwa na sio kwa maelekezo ya Rais Kikwete,” alisema Mbowe.

NIDHAMU KATIKA CHAMA

Alisema wapo waliokuwa wanachama wa chama hicho ambao wamewavua uwanachama kwa utovu wa nidhamu wakiwemo madiwani na viongozi wengine na kuwa ikibidi hata wabunge wakifanya utovu wa nidhamu chama hicho hakiogopi mtu kitawachukulia hatua kali ili wakishika dola serikali yao iwe na maslahi kwa wananchi.

DK. SLAA AMSIFU SABODO

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibroad Slaa, alisema wafanyabiashara wakubwa nchini wanafanya shughuli zao kwa maelekezo ya CCM tofauti na mfanyabiashara Mustapha Sabodo ambaye ni mwanachana wa CCM, lakini anakisaidia Chadema kwa uwazi bila kuogopa mkono wa serikali kutokana na kufanya biashara halali.

Alisema Sabodo ni sehemu ya mafanikio ya Chadema kutokana na kuchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha na kupata wabunge wengi kwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

“Tunamshukuru Mzee Sabodo kwa kutusaidia mara kwa mara katika chaguzi kuanzia ule wa mwaka 2010 hadi wa Arumeru Mashariki wa mwaka huu hadi sasa ametuachangia Sh. milioni 450 visima 210 katika majimbo yote yaliyoko chini ya Chadema,” alisema Dk. Slaa.

Naye Sabodo aliyehudhuria mkutano huo kama mgeni mualikwa, alisema alichotoa Chadema ni asilimia moja ya yale aliyoyafanya kwa CCM na kwamba katika miaka 50 ambayo amekisaidia chama tawala hajawahi kupewa heshima kubwa na kuambiwa asante kama walivyofanya Chadema.

“Sijasema CCM wabaya, lakini wanapofanyiwa mazuri wanapaswa washukuru kama mlivyofanya ninyi Chadema, naamini vyama hivi viwili ni sawa na mtu na binamu yake... pia nataka kuahidi kwamba nitahakikisha najenga ofisi ya makao makuu ya Chadema yenye hadhi badala ya ile mnayotumia sasa,” alisema Sabodo.

Aidha katika mkutano huo, baadhi ya wajumbe walishindwa kuhudhuria kutokana na kuwa na udhuru mbalimbali, akiwemo Edwin Mtei, Bob Makani na Zitto Kabwe ambao walikuwa na matatizo ya kiafya, wakati Tundu Lissu na Profesa Abdallah Safari walikuwa nje ya Dar es Salaam kushughulikia kesi mbalimbali zilizopo mahakamani.





CHANZO: NIPASHE
 
Zitto Kabwe ni mzima wa afya sema yeye hakubaliani na picha haziendi na Dokta Slaa, hataki kabisa kukutana nae kwenye kazi.
 
Kuna wafanya biashara wengi wenye imani ya kuchangia Chadema katika harakati za ukombozi kama Mfanya biashara marufu MzeeSABODO lakini tatizo kubwa lililopo ni vitisho vya mali zao.


Kumbuka kuwa kuna book specel la Wafanya biashara wakubwa kulazimishwa kuchangia Chama Tawala cha ccm, na kama hukufanya hivyo basi unapokea viticho kuwa Contena yako ikifika Bandarini tutaicherewecha kuitowa na kama muna bizaa zakuharibika au kucherewa kuza kazi kwako.


Sasa hii inasababisha kutumazwa ki-democrasia na kutokuwa na mamuzi, jambo jengine ni vigogo kutuma watu wao kila bada ya kipindi kwenda kukushanya pesa kwenye wafanya biashara wakubwa kama vile kuna shea yao.


Sasa hii inatufanya wafanya biashara tuingiwe na woga kusaidia chama tukitakacho kutokana na mbinyo wa vitisho.
 
Kama Arusha ni nchi basi mtaichukua lakini sio Tanganyika,

Hilo halitatokea kamwe abadan!
 
Zitto na Dr Slaa picha haziendii?

Haziendi mkuu,
Kwanza ni tofauti kubwa sana ya kiitikadi baina yao.

Zitto ana busara na hakurupuki katika kufanya maamuzi pia wote wanataka urais hapo ndio sehemu nyingine ugomvi ulipo.

Umeelewa?
 
Back
Top Bottom