MBOWE mnatuharibia chama, chama kinazidi kupotea

MBOWE mnatuharibia chama, chama kinazidi kupotea

mayange

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
701
Reaction score
198
Mimi nasema tena kuwa mimi nimwanachama hai wa CHADEMA, Nimemsema mh. Mbowe kwakuwa yeye ndiye mwenyekiti wetu na mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, haya yanayoendelea kukishushia heshma chama hayaoni? Dr. Slaa naye kama katibu wa chama hayaoni?.

Ni aibu kubwa sana taasisi kubwa kama hii yenye watu makini kiasi hiki kupambana na mtu mmoja tena mwisho wake tunaishia kupata aibu.

Kwani faida yetu sisi wananchi na wanachama mkimmaliza Zitto Kabwe kisiasa ni ipi?

Hapo awali mmetengeneza migogoro wenyewe kwa kumjengea tuhuma zisizo na ushahidi kama taarifa kutoka makao makuu ya chama kuhusu nyendo za ZZK toka mwaka 2008 kwa kupokea pesa toka CCM, mbona hamjatuletea ushahidi wa uhakika nasi tukajihakikishia?

Matokeo yake kila mmoja ameona utofauti wa CHADEMA ya mwaka 2013 na CHADEMA ya mwaka 2014.
Kwenye hili swala la leka dutigite, NSSFna TANAPA mmefanya uchunguzi wa kutosha na mkapata uhakika na mlichopeleka bungeni?

Tunataka ushahidi hapa ili na wananchi tujihakikishie sio mnatuletea propaganda za kijinga hapa na kuanza kuaminisha watu.

Nimesoma ufafanuzi wa Zitto mwenyewe, NSSF na TANAPA nimesikitika sana kuona kuwa maelezo haya kama ni ya kweli basi CHADEMA ndio itazidi kupoteza mvuto.

Nashindwa kuwaelewa na hawa washabiki wanaoshinda humu JF wakishabikia ujinga bila hata kufikiri ilimradi Mbowe kasema.

Watu wanabaki kuchangia changia ujinga wao humu Jf hata katika ujenzi wa chama hawaonekani wakidhani ndio ukomavu wa chama kumbe ndio wanazidi kukibomoa chama.

Mnajifanya wanachama wa CHADEMMA kwa kutetea hata ujinga wa baadhi ya viongozi ndio mnazidi kukimaliza chama, mfano huyu huyu ZZK alipoongelea kidogo habari za Mbowe wengi wenu mlianza kulalamika kwanini aongelee habari za Mbowe.

Sasa ZZK sio binadamu kama alivyo Mbowe au kiongozi mwingine anayeweza kuumia anapozushiwa na kuchonganishwa kwa wananchi?

Mashabiki nawashauri acheni kupumbazwa.
 
Ni kweli hakuna mwanachadema kama huyu jamaa wanachadema karibia wote kwanza hawana historia ya kuhoji jambo lolote lililofanywa na Mbowe au Slaa haijalishi jambo hilo ni jema au la hovyo

Xaxa huo ndo ukanjanja wenyewe na nchi yetu haiitaji wanachama bendera kama nyny xo hata kama mbowe au huyo slaa akiongea pumba nyiye mwasapoti tu xaxa nyiye watu au...
 
sio mwanachama kwa hoja ipi? Au nawe ndio wale washabiki mnashabikia na kutuhumu mwenzenu bila ya hata kufikiria? Mbona mnakuwa wajinga kiasi hiki? Mnatuharibia chama.

usifananishe CDM na hicho chama chenu cha wasaliti,Koma kulitumia jina la CDM kuwafurahisha mabwana zako waliokutuma.
 
Xaxa huo ndo ukanjanja wenyewe na nchi yetu haiitaji wanachama bendera kama nyny xo hata kama mbowe au huyo slaa akiongea pumba nyiye mwasapoti tu xaxa nyiye watu au...

peleka pumba zako lumumba au leka tutigite
 
Ni kweli hakuna mwanachadema kama huyu jamaa wanachadema karibia wote kwanza hawana historia ya kuhoji jambo lolote lililofanywa na Mbowe au Slaa haijalishi jambo hilo ni jema au la hovyo

hahahhaaaaaaaaaaaaaaaaa mbona unawatoa akili wenzio kiasi hicho
 
kipotee tu kwani sisi kinatuhusu nini..hizi thread nyingine pelekeni chadema blog.
 
Jamani wachangiaji wote wanakuja kutukana tu, naomba hata mmoja angalau aje kupinga kwa hoja.
 
Mnajiita makamanda. Kamanda gani anayekimbia vita? Au mnatumia tuu maneno bila kuyatendea haki
 
Back
Top Bottom