BONGOLALA
JF-Expert Member
- Sep 14, 2009
- 16,507
- 11,887
Mbowe: Mabomu yamerushwa na Polisi kwa maagizo ya Serikali
Amesema hivyo na ushahidi wa video upo, silaha 3 zilihusika.
Source: ITV
Amesema hivyo na ushahidi wa video upo, silaha 3 zilihusika.
Source: ITV
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema polisi wanahusika na milipuko katika mkutano wa CHADEMA na kuua watu watatu.
Mh Mbowe amesema ana ushahidi na picha za video za tukio hilo.
Mh Mbowe alisema hayo akihojiwa na ITV.
Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Aikaeli Mbowe (Mb) na Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema wamedai kuwa wana ushahidi wa kutosha juuya tukio la bomu katika Mkutano wa Kampeni wa CHADEMA-Arusha.
Akihojiwa na BBC, Mbowe amesema kuwa wao wana ushahidi wa kutosha ambao hatahivyo hawatautoa kwa vyombo vya ndani vya kiuchunguzi. Amesema kuwa wako tayari kushirikiana na vyombo vya kiuchunguzi vya kimataifa katika kuona ukweli wa tukio husika.
Naye Lema,akihojiwa na VOA, amesema kuwa wana ushahidi wakutosha ikiwemo video iliyopatikana siku ya tukio inayomtanabaisha mhusika watukio hilo la bomu.
Ukweli utajulikana tu. Nami niko njiani kwenda Arusha kufanya kinachonipasa kama mtanzania wa kawaida. Hatuwezi kukaa tukifungwa mikono yetu huku tukishuhudia wapendwa wetu wakiangamia. Mambo haya yatakoma sasa!