Mbowe, Lowassa Zitto &Co. Wazungu wenu wamewaonyesha njia ya Demokrasia!

Vipi chama kilichotawala zaidi ya miaka 50 lakini wananchi wake bado ni maskini wa kutupwa kinastahili kuendelea kutawala kweli? Kwa nini kiongozi wake asijiuzulu pia?
 
Je maoni ya waliomweka hapo yakoje na mawazo yake yakoje. Maana Cameroon amejiuzulu baada ya kile alichokua anakiamini kushindikana.na uchaguzi ulikuwa huru na haki je uchaguzi wa hapa ukoje?

Uchaguzi wa huru na haki ni relative, hata huko Uingereza ukienda ukaongea na watu kuna ambao pia watakuwa na malalamiko ya namna moja au nyingine jinsi mwenendo mzima ulivyokwenda, lkn hili la kujiuzulu kwa demokrasia ya kizungu huwa halina mjadala na wala halijadiliki, huwa Kiongozi akishindwa ni automatic anajiuzulu na wala hamuulizi Mwanachama wala Kiongozi yoyote yule, hivyo kama ulitaka kusema Mbowe anashindwa kujiuzulu kwa sababu ya Wanachama kutokumtaka kufanya hivyo hilo siyo kweli na hapo yuko kinyume kabisa na demokrasia ya Kizungu!
 
..aliyejiuzulu ni waziri mkuu aliyekuwa madarakani. Unaweza kumlinganisha na Raisi wa Tz.

..sasa kwanini mtoa mada haulizi kwanini Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, hawakujiuzulu baada ya kushindwa ktk utekelezaji wa ahadi walizitoa?

Napingana na hoja yako hasa hapo kwenye red. David Cameroon hajajizulu kwa sababu ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyotoa, ingekuwa ni ahadi basi angeshajiuzulu kitambo maana aliahidi kupunguza idadi ya raia wa EU wanaokuja UK kutoka kwenye malaki kufikia kwenye elfu kumi. Hili halikuwezekana kwa sababu ya sheria za EU.

Sababu ya David Cameroon kujiuzulu ni baada ya wananchi wa UK kukataa aina UK kuwa chini ya mamlaka ya EU kwa maana hiyo inatoa 'defination' mpya kabisa ya UK, kwa maneno rahisi wamekataa aina ya nchi anayoitaka yeye Cameroon.

Kama tungetumia misingi hiyo ya UK na Cameroon basi Freeman Mbowe alitakiwa kujizulu mara baada ya wananchi kukataa manifesto ya chama chake ambayo kimsingi inaeleza aina ya Tanzania aliyotaka kuijenga. Mbowe amekipeleka chama chake kwenye uchaguzi mkuu mara 3 na mara zote wananchi wamemkataa lakini bado yupo!
 
Kila siku mnaimba hapa demokrasia, demokrasia, mara sijui Tanzania hakuna demokrasia kama Ulaya, haya Waziri Mkuu wa Uingereza anajiuzulu kwa sababu ameshindwa kutimiza kile ambacho alikiahidi Chama chake/ kambi yake, sasa Mbowe unajiuzulu lini?
Kwa maana umeiongoza chadema chaguzi tatu mfululizo na umeshindwa zote lkn bado wewe ni Mwenyekiti wa Chama na kama hilo halitoshi wewe bado ni KUB vipindi viwili mfululizo ingawaje hakuna uchaguzi uliyowahi kushinda!

Usijifanye hujui. Kwenye KILA uchaguzi, kinachoweka wazi wa nani anayeshinda na nani anayeshindwa ni WAHESABU KURA, sio WAPIGA KURA!

Ili mradi CCM inamiliki dola, na ndiyo inayosimamia Tume ya Uchaguzi ya Taifa (yenye viongozi wanaoteuliwa na Rais, Mwenyekiti wa Chama Tawala), HAITATOKEA chama chochote kile cha upinzani kushinda uchaguzi, kwa ngazi ya Urais! HATA KIDOGO!

Kama mnabisha, iachieni Tume ya Uchaguzi ya Taifa iwe HURU kabisa, tuingike kwenye kinyang'anyiro cha kura tukiwa na uwanda sawia... Polisi wasimamie usalama, sio vitisho na virungu kwa wagombea wa vyama pinzani na wanachama wao.

Waachieni Watanzania WAWE HURU kuchagua nani aongoze NCHI YAO!

#MwishoWaUbayaMnaujua
 
Uko nje ya Mada, hapa hoja ni kwamba ni kwa nini Mbowe hajajiuzulu kama Wazungu ili hali ameongoza chaguzi tatu na ameshidwa zote?
Hilo la kuiba kura au sijui kuibiwa kura mnalijua ninyi tu lkn Wasimamizi wa AM, SADC, Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Ulaya (EU) pmj na USA wenyewe wamesema uchaguzi wa Tanzania ulikuwa huru na wa haki, hivyo kwa kifupi Dunia inajua kwamba tulifanya uchaguzi uliokuwa huru na haki na aliyeshinda, kashinda kihalali hayo mengine yote jiambieni huko kwenu Kishumundu!
 
..aliyejiuzulu ni waziri mkuu aliyekuwa madarakani. Unaweza kumlinganisha na Raisi wa Tz.

..sasa kwanini mtoa mada haulizi kwanini Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, hawakujiuzulu baada ya kushindwa ktk utekelezaji wa ahadi walizitoa?
Mwisho waliondoka hawakubaki kuruhusu demokrasia. Hapo ndo tofauti na hao. Hata akishindwa X100 yumo tu.

Na sahizi utasikia wakitangaza kung'oana kwa sababu uchaguzi wa ndani umekaribia.
 
Napingana na hoja yako hasa hapo kwenye red. David Cameroon hajajizulu kwa sababu ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyotoa, ingekuwa ni ahadi basi angeshajiuzulu kitambo maana aliahidi kupunguza idadi ya raia wa EU wanaokuja UK kutoka kwenye malaki kufikia kwenye elfu kumi. Hili halikuwezekana kwa sababu ya sheria za EU.

Sababu ya David Cameroon kujiuzulu ni baada ya wananchi wa UK kukataa aina UK kuwa chini ya mamlaka ya EU kwa maana hiyo inatoa 'defination' mpya kabisa ya UK, kwa maneno rahisi wamekataa aina ya nchi anayoitaka yeye Cameroon.

Kama tungetumia misingi hiyo ya UK na Cameroon basi Freeman Mbowe alitakiwa kujizulu mara baada ya wananchi kukataa manifesto ya chama chake ambayo kimsingi inaeleza aina ya Tanzania aliyotaka kuijenga. Mbowe amekipeleka chama chake kwenye uchaguzi mkuu mara 3 na mara zote wananchi wamemkataa lakini bado yupo!

Mkuu, kula 5
 
Kila siku mnaimba hapa demokrasia, demokrasia, mara sijui Tanzania hakuna demokrasia kama Ulaya, haya Waziri Mkuu wa Uingereza anajiuzulu kwa sababu ameshindwa kutimiza kile ambacho alikiahidi Chama chake/ kambi yake, sasa Mbowe unajiuzulu lini?
Kwa maana umeiongoza chadema chaguzi tatu mfululizo na umeshindwa zote lkn bado wewe ni Mwenyekiti wa Chama na kama hilo halitoshi wewe bado ni KUB vipindi viwili mfululizo ingawaje hakuna uchaguzi uliyowahi kushinda!

Sasa mbona hapa hamtaki kuiiga demokrasia ya Wazungu? Au demokrasia ya Wazungu nzuri pale mnaponufaika?

Tayari tunamsikia fisadi Lowasa anataka kuwania tena uraisi mwaka 2020 huku akiimba demokrasia ingawaje alishindwa uchaguzi na isitoshe hakuna kikao chochote kilichompitisha kugombea uraisi 2020, je hiyo ni demokrasia?

Vile vile Zito Kabwe ambaye umekua ukipayuka sana siku za hivi karibuni kuhusu demokrasia na umeenda mbali zaidi na kumtuhumu Magufuli wetu kwamba hafwati demokrasia kama unavyoielewea wewe yaani demokrasia ya kizungu, mbona wewe (Zito) haukujiuzulu kama Kameruni (Waziri Mkuu wa Uingereza) au Wazungu wengine wafanyavyo pindi vyama wanavyoviongoza vinaposhindwa Uchaguzi?

Zito Kabwe amekiongoza Chama chake cha ACT kwenye Uchaguzi ameshindwa vibaya sana siajabu haijawahi kutokea ktk Historia ya Dunia hii Kiongozi anayejinasibu kama Zito kwamba yeye ndiyo yeye anashindwa hata kupata Mbunge mmoja zaidi ya yeye mwenyewe hivyo kidemokrasia ina maana Zito Kabwe ni failure na hapaswi hata kuwa kiongozi, kwa maana ameshindwa kutushawawishi Watanzania tupigie kura Wabunge wake, vipi hapo demokrasia? Au ikifikia hapo inakuwa wale ni Wazungu na sisi ni Waafrika?

Lisu, Baregu &Co. mko wapi kuhusu hili?
FUNZO tunalolipata ni kusikiliza na kufuata maamuzi ya wananchi. Uingereza hawakung'ang'aniza matakwa viongozi au chama kilichoko madarakani
 
CCM wanachofanya ni shindanisha wagombea wao wa urais kwa uwazi na yeyote anayepata nafasi ya kukiwakilisha chama katika nafasi ya urais na kushinda inakuwa ni automatic election kwa nafasi ya mwenyekiti wa CCM.

Hivi katiba ya ccm inasemaje kuhusu hilo unaloliongea?
 
Huyu ndie kijana mwenye akili zaidi huko lumumba !!
Akili za buku 2
 
Kila siku mnaimba hapa demokrasia, demokrasia, mara sijui Tanzania hakuna demokrasia kama Ulaya, haya Waziri Mkuu wa Uingereza anajiuzulu kwa sababu ameshindwa kutimiza kile ambacho alikiahidi Chama chake/ kambi yake, sasa Mbowe unajiuzulu lini?
Kwa maana umeiongoza chadema chaguzi tatu mfululizo na umeshindwa zote lkn bado wewe ni Mwenyekiti wa Chama na kama hilo halitoshi wewe bado ni KUB vipindi viwili mfululizo ingawaje hakuna uchaguzi uliyowahi kushinda!

Sasa mbona hapa hamtaki kuiiga demokrasia ya Wazungu? Au demokrasia ya Wazungu nzuri pale mnaponufaika?

Tayari tunamsikia fisadi Lowasa anataka kuwania tena uraisi mwaka 2020 huku akiimba demokrasia ingawaje alishindwa uchaguzi na isitoshe hakuna kikao chochote kilichompitisha kugombea uraisi 2020, je hiyo ni demokrasia?

Vile vile Zito Kabwe ambaye umekua ukipayuka sana siku za hivi karibuni kuhusu demokrasia na umeenda mbali zaidi na kumtuhumu Magufuli wetu kwamba hafwati demokrasia kama unavyoielewea wewe yaani demokrasia ya kizungu, mbona wewe (Zito) haukujiuzulu kama Kameruni (Waziri Mkuu wa Uingereza) au Wazungu wengine wafanyavyo pindi vyama wanavyoviongoza vinaposhindwa Uchaguzi?

Zito Kabwe amekiongoza Chama chake cha ACT kwenye Uchaguzi ameshindwa vibaya sana siajabu haijawahi kutokea ktk Historia ya Dunia hii Kiongozi anayejinasibu kama Zito kwamba yeye ndiyo yeye anashindwa hata kupata Mbunge mmoja zaidi ya yeye mwenyewe hivyo kidemokrasia ina maana Zito Kabwe ni failure na hapaswi hata kuwa kiongozi, kwa maana ameshindwa kutushawawishi Watanzania tupigie kura Wabunge wake, vipi hapo demokrasia? Au ikifikia hapo inakuwa wale ni Wazungu na sisi ni Waafrika?

Lisu, Baregu &Co. mko wapi kuhusu hili?

Wewe akili zako hazina tofauti na huyu Mbunge wako

Hiyo msg ilitakiwa kupelekwa kwa CCM, wameahidi maisha mazuri kwa Watanzania tangu napata akili mpk leo hali ni ile ile, Ulimwengu anasema tunarudi nyuma miaka 50........nadhani kwa kushindwa kuwapa Watanzania maisha bora kwa wakati wote huo CCM ndio walipaswa wakae pembeni ili kuona wengine watalifanyia nini Taifa.......hata Zanzibar tu ingetosha kuonesha tofauti ya fikra na uongozi wa Nchi.
dah.. mkuu.. tkea uhuru no changes!!!???..,, nafkiri uko mbali kidogo... ishu n kwamba.. mabadiliko yapo, ila hayaendan na resources zilizopo... zatumika nyingi bila maslah y kitaifa,
 
Kwa nini unakwenda nje ya Mada? Hii Mada haihusu Zanzibar na uchaguzi wake kwani tayari kuna Mada nyingi kuhusu hilo hapa JF unaweza kutembelea huko kama ukipenda, hapa naongelea Demokrasia ya Kizungu, kwamba kiongozi akishindwa uchaguzi basi anajiuzulu kwa maana hana jipya tena na kupisha wengine, sasa kwa nini Mbowe ambaye ameongoza chadema chaguzi tatu mfululizo ameshindwa zote bado Mwenyekiti wa chadema? Yaani anakwenda kuiongoza chadema kwenye Uchaguzi wa nne ana lipi jipya? Je hakuna wengine?

Fisadi Lowasa amegombea Uraisi ameshindwa, leo bado miaka 5 uchaguzi mwingine ufike tayari anasema yeye 2020 anaingia Ikulu ni nani amempa nafasi ya kugombea Uraisi kupitia chadema?

Zito kabwe ameshindwa kunadi wagombea wake kama kiongozi wa Chama na ameshindwa vibaya hivyo maana yake ni kwamba Watanzania hatuna imani naye ni kwa nini hajajiuzulu kama Wazungu wanavyofanya?
Nakujibu kwa sababu hujielewi kuwa ni mjinga na mpumbavu kumbe hata maudhui ya unachokiandika hukijui?
 
Ruhusuni referendum Zanzibar.
Nyinyi kweli nimeamini ni wa dijitali. Yaani mkisikia kipya tayari msharukia na kuacha mengine yote? ndo maana hata NS anawadharau sana, madume mazima hovyo eti mnazibwa midomo.
 
Hiyo msg ilitakiwa kupelekwa kwa CCM, wameahidi maisha mazuri kwa Watanzania tangu napata akili mpk leo hali ni ile ile, Ulimwengu anasema tunarudi nyuma miaka 50........nadhani kwa kushindwa kuwapa Watanzania maisha bora kwa wakati wote huo CCM ndio walipaswa wakae pembeni ili kuona wengine watalifanyia nini Taifa.......hata Zanzibar tu ingetosha kuonesha tofauti ya fikra na uongozi wa Nchi.
Na wanaoendelea kimaisha wanatoka nchi gani sio kila kitu unasubiri uletewe chakalika unaposhindwa unapigwa tafu sio mtaan kwenu mtalo umeziba unasubir serikal ije kuzibua
 
Nyinyi kweli nimeamini ni wa dijitali. Yaani mkisikia kipya tayari msharukia na kuacha mengine yote? ndo maana hata NS anawadharau sana, madume mazima hovyo eti mnazibwa midomo.
Sasa ndio umecomment nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom