Mbowe, Lowassa Zitto &Co. Wazungu wenu wamewaonyesha njia ya Demokrasia!

Kila siku mnaimba hapa demokrasia, demokrasia, mara sijui Tanzania hakuna demokrasia kama Ulaya, haya Waziri Mkuu wa Uingereza anajiuzulu kwa sababu ameshindwa kutimiza kile ambacho alikiahidi Chama chake/ kambi yake, sasa Mbowe unajiuzulu lini?
Kwa maana umeiongoza chadema chaguzi tatu mfululizo na umeshindwa zote lkn bado wewe ni Mwenyekiti wa Chama na kama hilo halitoshi wewe bado ni KUB vipindi viwili mfululizo ingawaje hakuna uchaguzi uliyowahi kushinda!

Sasa mbona hapa hamtaki kuiiga demokrasia ya Wazungu? Au demokrasia ya Wazungu nzuri pale mnaponufaika?

Tayari tunamsikia fisadi Lowasa anataka kuwania tena uraisi mwaka 2020 huku akiimba demokrasia ingawaje alishindwa uchaguzi na isitoshe hakuna kikao chochote kilichompitisha kugombea uraisi 2020, je hiyo ni demokrasia?

Vile vile Zito Kabwe ambaye umekua ukipayuka sana siku za hivi karibuni kuhusu demokrasia na umeenda mbali zaidi na kumtuhumu Magufuli wetu kwamba hafwati demokrasia kama unavyoielewea wewe yaani demokrasia ya kizungu, mbona wewe (Zito) haukujiuzulu kama Kameruni (Waziri Mkuu wa Uingereza) au Wazungu wengine wafanyavyo pindi vyama wanavyoviongoza vinaposhindwa Uchaguzi?

Zito Kabwe amekiongoza Chama chake cha ACT kwenye Uchaguzi ameshindwa vibaya sana siajabu haijawahi kutokea ktk Historia ya Dunia hii Kiongozi anayejinasibu kama Zito kwamba yeye ndiyo yeye anashindwa hata kupata Mbunge mmoja zaidi ya yeye mwenyewe hivyo kidemokrasia ina maana Zito Kabwe ni failure na hapaswi hata kuwa kiongozi, kwa maana ameshindwa kutushawawishi Watanzania tupigie kura Wabunge wake, vipi hapo demokrasia? Au ikifikia hapo inakuwa wale ni Wazungu na sisi ni Waafrika?

Lisu, Baregu &Co. mko wapi kuhusu hili?
Nadhani mafunzo ni mawili. La kwanza ni hilo la kujiuzulu na kama ulivyosema uko sahihi. Lakini kubwa kabisa, ni KUHESHIMU MAONI NA MATAKWA YA WANANCHI kuhusu Matokeo ya Kura. Hakuna ubabaishaji hakuna ujanja ujanja kama ulioko huku Afrika. Wananchi wakiamua kile walichopigia kura kinatoka kama kilivyo. Sote tunakumbuka maoni ya Wananchi yalivyofanyiwa Figisu figusu. Kwa kweli tunayo mambo ya kujifunza inapofika suala la nchi zetu hizi na yale wenzetu wafanyayo huko Ulaya.

Wazungu ni watu smart na watabaki hivyo milele. Hakuna mizengwe wala longolongo. Afrika ipo shida kubwa na ndiyo maana HATUENDELEI!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom