Mbowe,Lissu , wammnyooshea mikono juu Zitto Kabwe

Mbowe,Lissu , wammnyooshea mikono juu Zitto Kabwe

Status
Not open for further replies.

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,062
Reaction score
3,280
Zitto bado ni Lulu ndani ya Chama .

Sinema ilianza kabla ya Kikao cha bunge kufunguliwa jioni . , ndani ya Bunge Zitto alionekana kuzungukwa na wabunge kibao wa CDM na CCM...

Part two ni pale Makofi yakutosha aliyopigiwa Zitto wakati anatoka nje... duuh nikajiuliza .. huyuanayepigiwa makofi kiasi hichi ai ndio yule alikua anaitwa msaliti .... na hao hao si ndio walikiri kutoshirikiana nae kwa lolote

Mwishoni nilichikiona ni...

'' Akili ndogo kushindani na akili kubwa '' hakuna lingine .

Hakuna mtu CHADEMA mwenye uwezo wa kujenga hoja za nchi zaidi ya Zitto .

Upinzani bado ZZK anahitajika kufikisha upinzani mahali pake .
 
Kiukweli walifanya kazi nzuri sana jana
 
....chadema haiangalii sura kama ccm. kwetu maslahi ya taiga mbele na mambo mengine baadae...

Note: kusoma report hats darasa la tatu anaweza...
 
Hizi mada lengo lake ni kutaka watu kutukanana tu humu .......nchi inapokuwa vitani inakuwa ni Watanzania kuilinda nchi dhidi ya yeyote na si CDM,CCM au kundi lolote ......Issue ya IPTL si issue ya chama au vyama .......acheni kuvuruga dakika hii tunayotaka kuwajibishana ......... ndio maana unamuona hata Rage (CCM) yupo na Zitto kwenye hili ..........
 
mtu yoyote makini hawezi kuwa mchoyo wa pongezi.
tunajali hoja za maana na tija.
ukitoa hoja za maana na zenye tija lazima upongezwe,
ukifanya madudu lazima ukosolewe.

Na hitaji tu CDM watambue kua Zitto ni mtu wa muhimu kwao ,kwa namna moja ama nyingine , walitumuonea tu kumfuta uwanachama na mambo mengine kwa hoja isyokua na mashiko . Ni muda sasa wa Viongozi wa CDM kujirudi ,bado ni mtu wa mujimu saana kwenye Chama
 
Chadema wamelazimika kuishangilia tu kwani hawana jinsi.lakini bado inawauma zitto kupata ujiko
 
Nyie watu ndio mnaharibu Zitto kwa sababu ya sifa hizi za ki-pumba-vu !.

Eti hakuna anayeweza kujenga hoja CDM nzima kama yeye !. Na yeye alivyo wa ajabu nadhani huwa anaamini upuuzi kama huu na matokeo yake ndio maana aliweza kujiona kwamba yeye alikuwa zaidi ya Chama !

Zitto pamoja na kamati yake wamefanya kazi nzuri kwenye hii issue ya Escrow, na watu wengi ikiwa ni pamoja na mimi ninalikubali hilo na hata mimi ningekuwa hapo Bungeni ningempigia makofi....Actually ingeshangaza kama CDM wasingempigia makofi !. Mbona huwa wanawapigia wabunge na viongozi wa CCM pale wanapoongea hoja zenye mashiko ? Sasa kitu gani cha ajabu wao kumpigia Zitto !

Hata hivyo hiyo haibadilishi ukweli kwamba Zitto hafai kuendelea kuwa CDM !. Akaendeleze chama chake cha ACT alichokianzisha yeye pamoja na msaliti mwenzake Kitila !


Zitto bado ni Lulu ndani ya Chama .

Sinema ilianza kabla ya Kikao cha bunge kufunguliwa jioni . , ndani ya Bunge Zitto alionekana kuzungukwa na wabunge kibao wa CDM na CCM...

Part two ni pale Makofi yakutosha aliyopigiwa Zitto wakati anatoka nje... duuh nikajiuliza .. huyuanayepigiwa makofi kiasi hichi ai ndio yule alikua anaitwa msaliti .... na hao hao si ndio walikiri kutoshirikiana nae kwa lolote

Mwishoni nilichikiona ni...

'' Akili ndogo kushindani na akili kubwa '' hakuna lingine .

Hakuna mtu CHADEMA mwenye uwezo wa kujenga hoja za nchi zaidi ya Zitto .

Upinzani bado ZZK anahitajika kufikisha upinzani mahali pake .
 
Kwani Zito alijenga hoja au alikuwa anasoma kile kilichoandikwa na kamati nzima? Nadhani kamati ilikuwa na watu zaidi ya kumi kutoka CCM na vyama vingine vya upinzani.
 
Kwa hiyo mtu akifanya jambo zuri asisifiwe?, hizi akili za kushikiwa mnapata wapi?

Hapo lazima ugundue kuwa pana chuki kubwa ya kikabila /kikanda /kiimaani.

Na pana hawa viumbe wa Mwenyezi Mungu baadhi yao hawatobadilika maana imo damuni mwao.
 
Mtoa mada wewe ni mpuuzi.
Mathalan, wangemzomea ungekaa kimya?
Na je wasingempongeza wakauchuna tu ungekaa kimya?
All in all unawashwa na unatabia za uswahili, hukosi la kusema.
 
Ndo hapo ujue CHADEMA siyo chama cha KINAFIKI. Mtu akifanya vizuri anapongezwa na akiboronga hamna kuleteana UNAFIKI unapigwa za uso pia.

LIVE LONG CHADEMA...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom