Mpangawangu
JF-Expert Member
- Mar 5, 2014
- 887
- 965
JESHI la Polisi Nchini lipo mbioni kumkamata Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kudaiwa kutorosha mabilioni ya fedha kwenda nchi mbalimbali za Bara za Asia.
Uchunguzi uliofanywa na JAMVI LA HABARI, umebaini kwa kiasi kikubwa uchunguzi uliokuwa unafanywa na Kitengo cha Uchunguzi wa Fedha kilicho chini ya Wizara ya Fedha (FIU) kimekamilika huku Polisi ikitarajia kuanza kuchukua hatua zaidi.
Taarifa ilizozipata gazeti hilo kutoka FIU, ilisema tayari kila kitu kimemalizika na kilichobaki ni suala hilo, kulipeleka Polisi kwa ajili ya kuchukua uamuzi zaidi wa jambo hilo.
"Tumemaliza kila kitu na kilichobaki ni Polisi, lakini mie sio msemaji wa suala hilo, ungezungumza na watu wa FRAUD kutoka Polisi, ambao watakupa nafasi nzuri ya suala hilo, ambalo ni kubwa sana,''alisema.
Hata hivyo, Gazeti hili liliwasiliana na mmoja wa askari wanaoelezwa kulishikiria suala hilo, Salum Kisai, ambapo alisema yeye sio msemaji na kumtaka mwandishi awasiliane na Kamanda wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ZCO Costastine Massawe na kukata simu.
"Embu wasiliana na ZCO mie sio msemaji wa suala hilo,''alisema na kukata simu.
Mbowe, ambaye alisafirisha fedha hizo mwanzoni mwa mwezi wa Agosti, mwaka huu baada ya kuamisho mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake hivi karibuni bila kuwa na vielelezo vya kufanya hivyo na kutakiwa kukamatwa na kumfikisha katika vyombo vya dola.
Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mbunge wa Hai na mfanyabiashara mwenye makampuni mengi hapa nchini, amefanya uhamisho huo wa fedha kwa kutumia kampuni isiyofahamika sana ijulikanayo kwa jina la Aretra World Wide Limited na imethibitika kwamba amefanya uhamisho huo wa fedha kwa kumtumia mtu anayeitwa Junaid Ali, ambaye ni Meneja wa Mahusiano ya Wateja wa Benki ya Noor ya Falme za Kiarabu mwezi huo.
Taarifa zaidi zinathibitisha kwamba, Kwa kumtumia Ali, Mbowe aliagiza fedha hizo zipelekwe katika akaunti tatu tofauti ambazo zote ziko nje ya Tanzania.
Kampuni hizo na kiasi cha fedha kilichopelekwa ni Puku Hong Kong Limited iliyotumiwa dola 230,555 (shilingi milioni 461), TanChin Trading Co. Limited iliyotumiwa dola 302,614 (shilingi milioni 605) na Hong Kong Da Web International Tradings Limited iliyotumiwa dola 489,860 (shilingi milioni 980). Jumla ya fedha zote zilizohamishwa ni zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Makampuni yote yaliyotumiwa fedha yana ofisi zake nchini Hong Kong na yote yamefunguliwa akaunti katika benki maarufu ya HSBC.
Junaid Ali ambaye amepewa maelekezo ya kufanya malipo hayo ni mtaalamu wa masuala ya kufungua makampuni yanayojulikana kama offshore ambayo mara nyingi hutumiwa na wafanyabiashara kufanya malipo pasipo kujulikana na watu.
Taarifa zinaendelea kusema kwamba makampuni ya namna hii hufunguliwa katika nchi zenye usiri mkubwa kwa watu wanaohifadhi fedha na ndiyo maana wakati wa sakata la ununuzi wa rada, Andrew Chenge na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Idris Rashid, walitumiana fedha kupitia akaunti zao zilizo katika nchi zinazoongoza kwa kuwa na makampuni mengi ya namna hii.
Akimwandikia Junaid, Freeman Mbowe alisema; "Tafadhali, nakuomba na kwa haraka, ufanye uhamishaji wa fedha kutoka katika benki yako na kwenda kwenye akaunti zifuatazo; Puku, TanChin na Hong Kong Da Web," aliandika Mbowe.
Katika barua hiyo ambayo JAMVI LA HABARI imefanikiwa kuona nakala yake, Mbowe ameitambulisha kampuni yake kwa anuani ya S.LP 293816, iliyopo katika jengo la World Trade Centre, Mtaa wa Sheikh Zayed, Dubai falme za kiarabu.
Kwa kuwa kampuni hiyo ya Mbowe ni offshore, gazeti hili limeshindwa kufahamu ni kiasi gani cha fedha Mbowe amehifadhi au ameweka kwenye akaunti hiyo na chanzo cha mapato hayo ni kipi kwa vile biashara zake nyingi anafanya hapa nchini, ingawa ameanza kujitanua kimataifa.
Sambamba na hilo , uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba Mbowe alitakiwa kupokea kiasi cha dola 330,000 (shilingi milioni 660) takribani sawa na fedha aliyoihamishia TanChin Hong Hong, kutoka kwa wafadhili wa chama hicho waliopo nchini Japan.
Kwa mujibu wa mawasiliano baina ya viongozi wa juu wa Chadema na wafadhili hao wa kijapani kupitia kwa mtu anayefahamika kwa jina la Naomi pamoja na Mchungaji Mariko Morikubo, Chadema ilikuwa ichangiwe fedha za kijapani (Yen), milioni 40 ambazo ni sawa na dola 330,000 kabla ya mwisho wa Julai mwaka huu.
Ndani ya CHADEMA, ni viongozi wakuu watatu ndiyo wanaonekana kushiriki katika mazungumzo hayo; Mbowe, Slaa na Reginald Munisi ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho.
Mpaka sasa haijafahamika mara moja ni kwa nini Mbowe amehamisha kiasi kikubwa namna hiyo cha fedha na kukipeleka nje ya nchi na kwamba imeendelea kutia mashaka kama kuna kodi halali ya serikali imekatwa katika muamala huo.
Wakizungumza na gazeti hili lilipotaka kujua mtazamo wao kuhusu kinachoitwa 'utumbuaji majipu wa Magufuli' wananchi kadhaa wamesema hicho nacho ni moja kati ya kipimo kikubwa cha uimara wa serikali ya Magufuli na kwamba kama ataweza kumkamata Mbowe basi ataonekana kweli amedhamiri kulikomboa taifa letu na kuthibitisha msemo kwamba sheria ni msumeno.
Abdallah Hussein, mkazi wa Kichangani Morogoro amesema, ili nchi yoyote inayofuata na kuheshimu utawala wa sheria ni lazima watu wote waishi misingi na utaratibu wa nchi hiyo, Hussein amesisitiza ikiwa Mbowe ameweza kufanya hivyo na kama hatua haitachukuliwa dhidi yake, basi kuna uwezekano mkubwa wa wanasiasa wengine kutumia uanasiasa wao kufanya biashara halali na haramu kujinufaisha.
"Hebu ona hii,mtu kama mbowe anaweza kusafirisha zaidi ya bilioni mbili kiharaka haraka hivyo, unatarajia kuna uhalali hapo? ,nani amekagua hizo hela na kuthibitisha ni halali na hazina madhara wala viashiria vya rushwa?"
Ameendelea kushangaa na kuonyesha taadhari ya hali ya juu na kumtaka Rais Magufuli kuhakikisha anaendelea kutumbua majipu na kusisitiza kwamba asimuangalie mtu yeyote usoni na kwamba ni lazima sasa vyombo vya dola vikachukua nafasi yake na kuthibitisha uhalali wa fedha hizo .
Taarifa ambazo gazeti hili linazo zinasema kwamba kitengo cha udhibiti wa Fedha FIU kinaendelea kulishuhulikia suala hilo na kwamba inatarajiwa hatua kuchukuliwa wakatio wowote kutoka sasa.
Mara kadhaa Mbowe amekaririwa kama mtu anayetetea sana uwepo wa utawala wa sheria na kwamba amekuwa akiilaumu serikali na taasisi nyingine zisipofuata sheria, jambo ambalo yeye pia anakabiliwa nalo hivi sasa,.
Ikiwa FIU watakamilisha uchunguzi wao haraka kama inavyotarajiwa, jeshi la polisi litakuwa na wajibu wa kumkamata na kumfikisha mahakamani kwa tuhuma za usafirishaji fedha isivyo halali.
Chanzo: Gazeti la JAMVI LA HABARI