Mbowe kuhudhuria shauri lake Mahakama Kuu

A Father

JF-Expert Member
Nov 11, 2012
1,206
373
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imekubali ombi la Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe la kumruhusu Mbowe kuhudhuria shauri lake la Kikatiba alilolifungua dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Shauri hilo namba 21 la mwaka 2021 linasikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu John Mgeta, Steven Magoiga na Leila Mgonya ambapo litatajwa Agosti 30, 2021.

Katika kesi hiyo, Mbowe anapinga hatua ya kushtakiwa kwa kosa la ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kuhusiana na mashtaka hayo, huku akieleza maneno ya vitisho anayodai kupewa na Polisi.

Sambamba na madai hayo Mbowe anadai haki zake kukiukwa kwa kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilisha kuwajulisha Nduguz zake na Wakili wake, pia Mbowe anadai kuwa wakati alipokwa ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa Afisa wa Polisi.


Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakikmu Mkazi Kisutu, July 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine ambao walikuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka jana 2020.

 
Back
Top Bottom