Mbowe: Katika kila ukombozi yupo anayevishwa taji

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,526
41,040
"Moyo wangu wamtukuza Bwana na Roho yangu inafurahia Mungu Mkombazi wangu. Maana umewashusha wenye enzi katika viti, ukawakweza wanyenyekevu"

Nimeanza na nukuu hiyo ya Biblia, ambayo ilikuwa ni kukiri kwa Mama yetu Maria juu ya ukuu wa Mungu, na jinsi Mungu alivyo mwaminifu kwao wamchao.

Lakini dhima kubwa ya mada hii ni kutafakari siasa za nchi yetu ambayo bila shaka Mungu kwa huruma yake alitujalia kupewa. Waliopewa ni sisi sote, wanaCCM, wanaCHADEMA, wanaACT, waislam, wakristo, wapagani, wakurya, wasukuma, wachaga, wakinga, wahehe, wamatumbi, n.k.

Sote kwa haki sawa, Mungu alitujalia tuishi hapa, na hata tukiwa ugenini lakini tunajua tuna kwetu, ambapo ni Tanzania.

Wapo waliojitwakia utukufu wa Mungu, wamejimilikisha nchi, na kuwaona wengine ni wapangaji, wao huamua wanachotaka, na ninyi wengine nyote mfuate. Huo ni ushetani, na ukiukubali, maana yake umekubali kumtii shetani.

Wapo walio majasiri ambao wanakataa kuishi kama wapangaji, yaani usiwe na lolote la kuamua usipokuwa watawala.

Leo hii, kama wewe siyo mwanaCCM, basi wewe ni raia mpangaji. Utanyimwa karibu nafasi zote za kuamua yanayokuhusu. Ukiwa na bahati mbaya, unaweza kuondoshwa kabisa, usionekane tena Duniani. Ukibahatika kidogo, basi utafirisiwa, utawekwa mahabusu, utabambikiziwa kesi za uhaini, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, kufanya uchochezi, n.k.

Mbowe yupo ndani, wasaidizi wake kadhaa wapo ndani. Mbowe kabambikiziwa kesi ya ugaidi. Mbowe ambaye hajawahi kuthibitika kufanya jinai yoyote katika umri wake wote wa zaidi ya miaka 50, leo amekuwa gaidi!

Rais Samia alipoingia madarakani, aliwafungulia mashekhe waliotengenezewa kesi za ugaidi, sote tukaamini kuwa anachukizwa na mambo ya kuwabambikia watu kesi, kumbe labda alitaka awe nao wa kwake mwenyewe, kuliko kurithi waoiobambikiziwa na tawala zilizopita. Samia anatengenza wa kwake. Na siyo ajabu tutawapata wa kubambikiziwa uhujumu uchumi, uchochezi, uhaini, n.k.

Utawala wa Tanzania, ni kama viongozi wanashindana kufanya maovu kuliko mema.

Kwa upande mwingine, mahabusu zinatisha, kifo kinatisha, virungu na maji ya washawasha vinatisha lakini siku zote, taji hupatikana baada ya kukubali kuyakabili mateso, na kuyashinda.

Yesu ninayemwabudu kama nafsi ya Mungu aliyebeba ubinadamu, alikuja Duniani kutuonesha tunavyotakiwa kuishi. Aliteswa, akafa, akazikwa, akayashinda mauti, akapewa taji mbinguni ili kuyahukumu makabila yote.

Mandela, alifungwa mara kadhaa, kabla ya kufungwa miaka zaidi ya miaka 20, alivyotoka alichagukiwa kuwa Rais wa Kwanza wa SA isiyo na ubaguzi. Alitawala muhula mmoja tu, lakini mpaka anafariki alikuwa ndiye mtu maarufu zaidi kuliko wanadamu wote waliokuwa wakiishi nyakati zake.

Mahtam Gandhi likamatwa na kuhukumiwa jela miaka 6 na wakoloni kwabuchochezi, lakini mpaka leo, hakuna mtu maarufu kama Gandhi nchini India.

Martin Luther King Jn alifungwa, na leo hii nchini Marekani, ukimwondoa George Washington, hakuna kiongozi ambaye jina lake linaishi zaidi ya jina lake.

Kwenye orodha hii wapo wengi. Na Rais Samia atambue kuwa anaweza kumfanyia chochote shujaa Mbowe, lakini hata kwa vituko vyote, kamwe jina la Samia halitakaa lisikike kama la Freekan Mbowe, wawe wanaishi au hawapo Duniani. Mbowe hapiganii maisha yake maana hela alikwisha kuwa nazo, hapiganii cheo maana kama angetaka, hata leo, angeweza kusema anajiunga CCM, na haraka angepewa cheo, Mbowe anapigania haki ya kila mtu kuwa na umiliki wa nchi tuliyopewa na Mungu. Kazi anayoifanya Mbowe ni kazi takatifu. Na hakika, kwa uhakika, tena wa 100% Mungu hatamtupa, bali atamvidha taji, na kuwapa dhalilisho wale walao njama usiku na mchana, wakiwahadaa Watanzania kwa maneno matamu yaliyojaa unafiki ndani yake.

"Kwa kuwa hupiganii utajiri wako, hupiganii ukuu wako, bali unapigania watu wa nchi niliyowapa kuwa ja maamuzi ya maisha yao, nimekubariki wewe na kazi yako"

Wakati tukilaani ufedhuli unaofanywa na watawala, kila mmoja kwa namna alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu, tupiganie haki ya Mbowe, haki ya kila mtu, na zaidi ni haki ya nchi yetu kuwa na katiba nzuri tuliyoitengeneza wenyewe, na siyo tuliyotengenezewa na watawala.

Nyati ni wakubwa sana, na kama wangekuwa na umoja, haki hakuna nyati ambaye angeliwa na simba. Wanaliwa kwa sababu ya kutoshirikiana. Nyati akiona mwenzake analiwa na simba, anakaa pembeni, na bila shaka moyoni anasema kuwa, afadhali aliyeliwa siyo mimi, mimi nipo salama. Asichojua ni kuwa baada ya kuliwa yeye, huenda atakayefuatia ni yeye. Vyama vya upinzani vinaweza kufa, lakini nondo wala watu hawawezi kukosa wa kumla.

Kama mpinzani hayupo, atapatikana wa kuliwa humo humo CCM. Na hivi karibuni limedhihirika hilo. Walikuwa wanawabambikia matajiri kodi na kisha kuwafunga, walipoisha, wakawabambikia kodi wananchi wote kwenye miala. Wananchi wa kawaida, mlio wanaCCM endeleeni kufurahia kuwa anayeonewa ni Mbowe, siyo wewe mwanaCCM, lakini mjue siku Mbowe na CHADEMA wasipokuwepo, ndani ya CCM ni lazima wapatikane wa kuliwa.

Ni wakati wa kutafakari na kuamua, naweza nisiwe na ujasiri wa Mbowe, Lisu, Msigwa, Sugu, Lema, Hayati Maalim, Jusa na wengineo, lakini kwa huu woga na udhaifu wangu, nachangia nini katika jitihada za hawa mashujaa wanaotaka sisi wananchi tuongozwe kwa utaratibu wa haki?

Ukishindwa yote, basi jitenge na waovu na washabikiao maovu wala usishikamane nao kwa lolote. Jitenge nao katika maisha ya kila siku, hata katika mambo ya kawaida. Kujitenga au kuhakikisha upo mbali na ibilisi ni jambo la heri hata mbele za Mungu. Kuwa karibu na ushirikiane naye sana na kila mwenye haki na aitafutaye haki.
 
Mimi nimekuelewa,umefanya maombi yakuwaombea watawala wawe wanamwamini Mungu siyo Mali.
 
giphy (3).gif
 
Aksante: Kila mpenda uhuru na haki afanye lolote lile lililochini ya uwezo wake kuitafuta haki na uhuru hata kuwatemea mate watesi.
 
Watawala wamepoteza aibu hadi inaogopesha!!CCM SIO JOKA LA KAFARA HADI LIABUDIWE HIVI!KWANI CCM IKIONDOKA MADARAKANI TANZANIA ITATOWEKA???!!
 
"Moyo wangu wamtukuza Bwana, na Roho yangu inafurahia Mungu Mkombazi wangu. Maana umewashusha wenye enzi katika viti, ukawakweza wanyenyekevu"

Nimeanza na nukuu hiyo ya Biblia, ambayo ilikuwa ni kukiri kwa Mama yetu Maria juu ya ukuu wa Mungu, na jinsi Mungu alivyo mwaminifu kwao wamchao.

Lakini dhima kubwa ya mada hii ni kutafakari siasa za nchi yetu ambayo bila shaka Mungu kwa huruma yake alitujalia kupewa. Waliopewa ni sisi sote, wanaCCM, wanaCHADEMA, wanaACT, waislam, wakristo, wapagani, wakurya, wasukuma, wachaga, wakinga, wahehe, wamatumbi, n.k.

Sote kwa haki sawa, Mungu alitujalia tuishi hapa, na hata tukiwa ugenini lakini tunajua tuna kwetu, ambapo ni Tanzania.

Wapo waliojitwakia utukufu wa Mungu, wamejimilikisha nchi, na kuwaona wengine ni wapangaji, wao huamua wanachotaka, na ninyi wengine nyote mfuate. Huo ni ushetani, na ukiukubali, maana yake umekubali kumtii shetani.

Wapo walio majasiri ambao wanakataa kuishi kama wapangaji, yaani usiwe na lolote la kuamua usipokuwa watawala.

Leo hii, kama wewe siyo mwanaCCM, basi wewe ni raia mpangaji. Utanyimwa karibu nafasi zote za kuamua yanayokuhusu. Ukiwa na bahati mbaya, unaweza kuondoshwa kabisa, usionekane tena Duniani. Ukibahatika kidogo, basi utafirisiwa, utawekwa mahabusu, utabambikiziwa kesi za uhaini, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, kufanya uchochezi, n.k.

Mbowe yupo ndani, wasaidizi wake kadhaa wapo ndani. Mbowe kabambikiziwa kesi ya ugaidi. Mbowe ambaye hajawahi kuthibitika kufanya jinai yoyote katika umri wake wote wa zaidi ya miaka 50, leo amekuwa gaidi!

Rais Samia alipoingia madarakani, aliwafungulia mashekhe waliotengenezewa kesi za ugaidi, sote tukaamini kuwa anachukizwa na mambo ya kuwabambikia watu kesi, kumbe labda alitaka awe nao wa kwake mwenyewe, kuliko kurithi waoiobambikiziwa na tawala zilizopita. Samia anatengenza wa kwake. Na siyo ajabu tutawapata wa kubambikiziwa uhujumu uchumi, uchochezi, uhaini, n.k.

Utawala wa Tanzania, ni kama viongozi wanashindana kufanya maovu kuliko mema.

Kwa upande mwingine, mahabusu zinatisha, kifo kinatisha, virungu na maji ya washawasha vinatisha lakini siku zote, taji hupatikana baada ya kukubali kuyakabili mateso, na kuyashinda.

Yesu ninayemwabudu kama nafsi ya Mungu aliyebeba ubinadamu, alikuja Duniani kutuonesha tunavyotakiwa kuishi. Aliteswa, akafa, akazikwa, akayashinda mauti, akapewa taji mbinguni ili kuyahukumu makabila yote.

Mandela, alifungwa mara kadhaa, kabla ya kufungwa miaka zaidi ya miaka 20, alivyotoka alichagukiwa kuwa Rais wa Kwanza wa SA isiyo na ubaguzi. Alitawala muhula mmoja tu, lakini mpaka anafariki alikuwa ndiye mtu maarufu zaidi kuliko wanadamu wote waliokuwa wakiishi nyakati zake.

Mahtam Gandhi likamatwa na kuhukumiwa jela miaka 6 na wakoloni kwabuchochezi, lakini mpaka leo, hakuna mtu maarufu kama Gandhi nchini India.

Martin Luther King Jn alifungwa, na leo hii nchini Marekani, ukimwondoa George Washington, hakuna kiongozi ambaye jina lake linaishi zaidi ya jina lake.

Kwenye orodha hii wapo wengi. Na Rais Samia atambue kuwa anaweza kumfanyia chochote shujaa Mbowe, lakini hata kwa vituko vyote, kamwe jina la Samia halitakaa lisikike kama la Freekan Mbowe, wawe wanaishi au hawapo Duniani. Mbowe hapiganii maisha yake maana hela alikwisha kuwa nazo, hapiganii cheo maana kama angetaka, hata leo, angeweza kusema anajiunga CCM, na haraka angepewa cheo, Mbowe anapigania haki ya kila mtu kuwa na umiliki wa nchi tuliyopewa na Mungu. Kazi anayoifanya Mbowe ni kazi takatifu. Na hakika, kwa uhakika, tena wa 100% Mungu hatamtupa, bali atamvidha taji, na kuwapa dhalilisho wale walao njama usiku na mchana, wakiwahadaa Watanzania kwa maneno matamu yaliyojaa unafiki ndani yake.

"Kwa kuwa hupiganii utajiri wako, hupiganii ukuu wako, bali unapigania watu wa nchi niliyowapa kuwa ja maamuzi ya maisha yao, nimekubariki wewe na kazi yako"

Wakati tukilaani ufedhuli unaofanywa na watawala, kila mmoja kwa namna alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu, tupiganie haki ya Mbowe, haki ya kila mtu, na zaidi ni haki ya nchi yetu kuwa na katiba nzuri tuliyoitengeneza wenyewe, na siyo tuliyotengenezewa na watawala.

Nyati ni wakubwa sana, na kama wangekuwa na umoja, haki hakuna nyati ambaye angeliwa na simba. Wanaliwa kwa sababu ya kutoshirikiana. Nyati akiona mwenzake analiwa na simba, anakaa pembeni, na bila shaka moyoni anasema kuwa, afadhali aliyeliwa siyo mimi, mimi nipo salama. Asichojua ni kuwa baada ya kuliwa yeye, huenda atakayefuatia ni yeye. Vyama vya upinzani vinaweza kufa, lakini nondo wala watu hawawezi kukosa wa kumla.

Kama mpinzani hayupo, atapatikana wa kuliwa humo humo CCM. Na hivi karibuni limedhihirika hilo. Walikuwa wanawabambikia matajiri kodi na kisha kuwafunga, walipoisha, wakawabambikia kodi wananchi wote kwenye miala. Wananchi wa kawaida, mlio wanaCCM endeleeni kufurahia kuwa anayeonewa ni Mbowe, siyo wewe mwanaCCM, lakini mjue siku Mbowe na CHADEMA wasipokuwepo, ndani ya CCM ni lazima wapatikane wa kuliwa.

Ni wakati wa kutafakari na kuamua, naweza nisiwe na ujasiri wa Mbowe, Lisu, Msigwa, Sugu, Lema, Hayati Maalim, Jusa na wengineo, lakini kwa huu woga na udhaifu wangu, nachangia nini katika jitihada za hawa mashujaa wanaotaka sisi wananchi tuongozwe kwa utaratibu wa haki?
Mbowe amekuwa kama Musa, Joshua na manabii wengine wakubwa. Tumwombee Mungu amlinde katika utume wake kwa watanzania.
 
Kwa hili la katiba nasimama na Mh. Mbowe nihesabiwe....no matter what.
 
Joyce Mukya tunaomba utulie wakati serikali inafanya uchunguzi wake juu ya gaidi Freeman Mbowe
Mijitu mishamba na ya kuja Kama wewe..Lini Tanzania waliwahi kukamata magaidi...ubalozi wa Marekani ulivyolipuliwa walienda vijiweni kuwakamata wavuta bangi..walivyotua CIA na FIB walivyowacheck wakawaambia Polisi waachieni wote..ndani ya masaa 24 wakamkamata yule kijana wa Kinzanzibar boda ya SA..kuwa na akili hao watu wenu wanajua kunyanyasa wanyonge tu...
 
Kiongozi mkuu wa upinzani bungeni,mbunge,mwenyekiti wa chama cha upinzani anakuwa gaidi!??! Kama Osama au?? Hahahahhahaaa doh! Kweli mama anaupiga mwingi chiiii....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom