labda niandike kidogo,
mkuu hilo sibishi. hata mimi kimoyomoyo nasema hivyo hivyo kuwa Prof. angevuta subira kwanza. lakini kinachofanya nimsapoti Prof. ni hii tabia ya Seif iliyojengeka. alichokifanya sasa hivi ni marudio tu. alishakifanya kwa Aboud Jumbe kwa kupeleka maneno kwa mwl. nyerere na matokeo yake sote tunayafahamu kilichomkuta yule mzee. nilifikiri alishajifunza.
Prof. Lipumba ndo muasisi wa ukawa na ndo aliyemkaribisha mzee lowassa kuja ukawa. (na siamini kama kweli kuondoka kwa Lipumba kuna uhusiano wowote na Lowassa, sema tu ilikuwa justifcation, maana ukweli ndo unasemwa sasa hivi) kilichomfanya ajiuzulu ni ile kuzungukwa na seif. yeye anajua wako na seif pamoja kumbe mwenzie anamzunguka. anaenda kwenye vikao yeye akiwa kama kwenyekiti wa ukawa na Dr. slaa katibu anashangaa anapewa habari za chama chake na akina mbowe. hii kiukweli ni dharau ya hali ya juu. kama kuna kitu seif alitaka kwa nini asimuambie Lipumba na wakawa na msimamo wa pamoja kama chama ili kulinda hata kama ni masilahi ya chama? siamini kama kweli Prof. angekataa ukizingatia wamefanya kazi pamoja kwa zaidi ya miaka 20.
ndo maana binafsi na kwa sauti naona anachofanya Prof. ni sawa kabisa hasa kwa aina ya mtu mwenyewe (seif) na tabia zake za ovyo mpaka hata katika umri ule.