Mbowe kafanya mengi mazuri kwa Chadema Kwa nchi yake na kwenye siasa za upinzani ila naona ni muda mzuri na sahihi kwake kuachia ngazi

Tundu Lisu atafungwa speed gavana na Mbowe. Lisu na kelele zake zote hana ujanja wa kumtilia kibesi Mbowe hilo hata wewe unalijua.

Hamna Cha speed gavana. Mbona Jana watu wameongea issues kabla ya Mbowe kuharibu na hotuba yake ambayo ilikuwa personal.
 
Heche! Sio kwamba mbaya ila wanamuogopa na misimamo yake atawaacha njia panda kama jiwe alivyowatosa wenye chama

Sidhani! Wanachadema Wana imani naye. Ni Kama 2020, kamati kuu ilimchagua Nyalandu ila mkutano mkuu ukamchagua Lissu. Wanachama wanajua anaye faa.
 
Mbowe akiondoka CHADEMA is doomed labda asimame imara kuweka Mwenyekiti moderate asitokee kwe kambi ya radicals. Siasa za Afrika ni za kutongoza demu ukitumia nguvu unapotea na hakuna atakaejali mfano mzuri yeye kakaa ndani muda tu nini kilitokea, Rwanda mwandishi mkosoaji amekufa nini kimetokea, Cameroon wana Rais hata hajui yeye ni nani ila maisha yanaenda Museveni kila siku anaua watu. So kwa Afrika lazima ujue kuuma na kupuuliza huku ukijenga uwezo chama chako kauaminika zaidi hasa na vyombo vya dola ila ukitumia nguvu staili za kina Heche, Lissu, Lema and co hupati chochote na unazimishwa tena ikiwa bahati mbaya unazimishwa mazima

Nakataa kabisa ulichosema. CHADEMA hakiwezi kufa kisa Kiongozi wake ni radical. Kwa sasa CHADEMA inahitaji Kiongozi radical la sivyo CCM wataipiga mwishoni. Muulize maalim aliyefanya maridhiano na CCM walimfanyia Nini 2010? 2015? na 2020 walimpiga Hadi virungu. CCM sio wa kuwachekea.
 
Mbowe Muda wake Umefika kikomo
Eti amepoteza billions kazaa je anasahau kuhusu watu Kama lissu wamepigwa Hadi risasi na wengine wamekufa na Kupata Ulemavu wa kudumu.

Kapata pesa nyingi akiwa mwenyekiti wa CDM kuliko alizotoa. Isitoshe CDM sio Bank aanze kuleta vitisho vya hela zake.
 
Mbowe angeondoka kabla hajaaribu zaidi. Wanachama walimlilia alipokuwa ndani, leo katoka anamuona aliyeutangazia Dunia kuwa Mbowe ni gaidi ni mzuri Sana.

Akae pembeni maana sasa ni dhahiri wafuasi wa CDM hatuna imani naye.
 
Ushauri wako ni mzuri Sana. Ni muda Sasa Mbowe akastaafu kwa heshima na kumuachia Lissu au Heche uenyekiti ili kulinda tradition ya CHADEMA. Naona mzee anajaribu kuipeleka CHADEMA kwenye mrengo ambao sio. Utaona tofauti Lissu akikanyaga bongo.
Nashukuru mkuu Kwa kupendrkeza majina,
Ila naona ndani ya cdm kuna haja ya kusimamia na kuiheshimu demokrasia ya ndani Kwa nguvu zote na kuruhusu ushindani wa haki bila mizengwe,.
Kila mwanachama aweze kugom ea nafasi yoyote bila hofu ,
Ukweli mchungu ni kwamba mkiti alitengeneza mazingira ya kwamba kila anayetaka nafasi yake kidemokrasia kabisa ni msaliti

Na hii dhambi akiendelea kubaki kwenye hiyo nafasi inaenda kumtafuna , kama ambavyo ameanza kulauma kwamba anasingiziwa kala asali, maanake ameshaanza naye kuitwa msaliti
 
Ndio maana nasema haya mambo kuna wakati yanahitaji kutumia akili zaidi ya maguvu...

Mbowe kuondoka Chadema ni suala la muda tu, coz alishasema itakuwa this year...

Lakini atakuja nani kuchukua nafsi yake kwangu ndio la msingi zaidi, atakuwa na akili na hekima kama za Mbowe? au kwake ni kushikana mashati tu muda wote kama wanachadema wanavyopenda!..View attachment 2490565

Yes, na alifanikiwa kumtongoza demu, ajabu wengine hawaoni hili! wao ni Mbowe aondoke...kama wimbo!.
Upuuzi mtupu. Walamba asali hamna la kuwasaidia watanzania.
 
Hotuba ilikuwa nzuri na ya kueleweka sema huu uzi umevamiwa na uvccm kuja ku spin Mambo ili mbowe aonekane hafai

Lkn Intel. ya chama ipo makini na imeshalijua hilo mkae kwa kutulia

Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
 
Tangu hotuba ya Washington DC nilimuona Mbowe kabadilika. Anaongelea utaifa kuliko CHADEMA. Nikashangaa, issues za CHADEMA haziongelei anadai yeye anapigania taifa. Nikadhani Furahisha atabadilika kumbe ni Yale Yale. Akija Musoma ajirekebishe please. Musoma mjini ndio Jimbo ambalo CHADEMA Ina wafuasi wengi asiharibu Kama Jana.

Mbowe hapaswi tena kupewa mic kwenye mkutano wa hadhara wa CDM ahutubie. Kama anapigania taifa basi awe anaenda kwenye mikutano ya kitaifa aongee huko.
 
Sidhani! Wanachadema Wana imani naye. Ni Kama 2020, kamati kuu ilimchagua Nyalandu ila mkutano mkuu ukamchagua Lissu. Wanachama wanajua anaye faa.
Hapa demokrsia ya ndani inatakiwa iimarishwe Sana ndani ya chadema iwepo kamati huru wazi na haki ya uchaguzi, Kila mwanachama aone haki ikitendeka,
Kama ambavyo kinapigania tume huru ya uchaguzi lazima waonyeshe mfano mkuu,
Ndicho tunachotamani
 
Naunga mkono hoja Mbowe anahitaji kupumzika hivi sasa mwanaCHADEMA yeyote ana haki ya kuwa mwenyekiti, tusimfanye kama special sana ndiye pekee mwenye sifa za uenyekiti. Uenyekiti ni wa CHADEMA na hivyo ni haki ya kila mwanaCHADEMA.
 
Hotuba ilikuwa nzuri na ya kueleweka sema huu uzi umevamiwa na uvccm kuja ku spin Mambo ili mbowe aonekane hafai

Lkn Intel. ya chama ipo makini na imeshalijua hilo mkae kwa kutulia

Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
Ingawa sio lengo la huu uzi kujadili hotuba ya Mbowe,
Lakini kiukweli baada miaka Saba ya kifungo Cha mikutano, mbowe alipaswa ajielekeze zaidi kwenye dira mpya ya chama chake,
Naamini sio kosa lake ila ni wakati hauko upande wake amefanya mengi so uwezo na nguvu na uono wake umepungua sana

Pia sio kila hoja unafikiria uccm na uchadema
Huu uzi unachangiwa na watu wenye KIU ya kuona mabadiliko ndani ya Chama mbadala na demokrasia ya nchi yetu
 
Tangu hotuba ya Washington DC nilimuona Mbowe kabadilika. Anaongelea utaifa kuliko CHADEMA. Nikashangaa, issues za CHADEMA haziongelei anadai yeye anapigania taifa. Nikadhani Furahisha atabadilika kumbe ni Yale Yale. Akija Musoma ajirekebishe please. Musoma mjini ndio Jimbo ambalo CHADEMA Ina wafuasi wengi asiharibu Kama Jana.
Hapo tumaini letu pekee lililobaki pale chadema ni lisu na kamanda Heche Hwa kwa sasa ndio wenye uwezo wa kukivusha hapa hiki chama
 
Back
Top Bottom