Mbowe aunganishwa kesi ya Slaa, Lissu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe aunganishwa kesi ya Slaa, Lissu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Nov 13, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amepandishwa kizimbani katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria na kukaidi amri ya jeshi la polisi

  Mbowe ameunganishwa na wenzake waliopandishwa kizimbani juzi Dk. Slaa na Lissu ambapo imetimia idadi ya washitakiwa 28 katika kesi hiyo

  Watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kufanya kusanyiko isivyo halali katika viwanja vya NMC, eneo la Unga Ltd, Arusha Novemba 7 mwaka huu .

  Mbowe alipandishwa kizimbani jana katika mahakama hiyo mara baada ya kujisalimisha polisi kwa kutakiwa kufanya hivyo na jeshi hilo kwa kuwa siku ya tukio hakupatikana

  Alisomewa mashtiaka hayo mawili mbele ya Hakimu Devotha Kamuzora na kukana mashitaka hayo na kuwa nje kwa dhamana kwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho na barua ya utambulisho kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kata wanakotoka kutia saini hati ya dhamana ya Shilingi milioni tano kila mmoja.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu itakapotajwa

  Chanzo: Mbowe aunganishwa kesi ya Slaa, Lissu
   
Loading...