Katika mkutano wa leo mbowe ametoboa siri ya mafanikio ya CHADEMA kuwa ni umoja walionao katika uongozi wao huku wabunge wao wakiwa tayari kutumika katika ujenzi wa chama hicho. Amewaomba wameru wasishangae kumuona Nasari akiwa Lindi au Mtwara katika shughuli za ujenzi wa Taifa kwani mbunge wa Chadema ni mbunge wa Taifa. Hayo aliyasema kukiwa na mvua kubwa iliyoendelea katika mkutano wa shukrani kwa Wameru kukichagua Chadema katika viwanja vya Leganga USA leo jioni.
hongera kamanda mbowe kwani nina taarifa ulitumia gari lako kukimbiza gari la ccm lenye kura feki.hii sio kazi ya mwenyekiti wa chama lakini kama mwenyekiti umeonyesha umuhimu wa kuwa front line.
kadiri siku zinavyokwenda leadership credibility kwa Mbowe naona zinaongezeka! Mungu ampe maisha marefu na busara. tz nchi yangu na chdm nyumbani kwangu!
congratulation twas a tough battle and hardwork resilence and strong willpower...in the end you toppled..was a good chase coz for a month we followed each event until the admn forced me to join and not spectate...
Kamanda Mbowe nakuaminia. Njoo LONGIDO ndo kuna mtaji mkubwa wa CCM imekuwa ikisha kila mwaka kwa 84% huku wananchi wake wikiwa na kipato cha sh. 200-500 kwa siku. Ninajua si rahisi watu kuamini hili lakini ndivyo ilivyo vijana wa CDM tuliamua kufanya assessment tukagundua hili. Vijana, Akina mama na Wazee wanafunzi wamechoshwa sana CHADEMA ni kuja kuchukuwa tu. Viongozi wa Chama CCM ni maarufu sana kwa kushinda na tooth pick midomoni wakichokonoa vipande vya minofu ya nyama huku familia zao wakiishia kushinda kwa uji wa chumvi. Kwa kifupi jana walirudi vijijini kwa aibu baada ya kukung'utwa na nguvu umma.