Mbowe atoa tamko: CHADEMA kuisimamisha nchi Machi 25, 2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe atoa tamko: CHADEMA kuisimamisha nchi Machi 25, 2013

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Mar 11, 2013.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Mar 11, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,616
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Muda mfupi uliopita hapa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, ametoa tamko la Musoma, likiwataka Watanzania wote wapenda nchi yao, kujiandaa kwa maandamano makubwa na mgomo wa wananchi yatakayofanyika Machi 25, 2013, nchi nzima, kushinikiza uwajibikaji (kujiuzulu au kufukuzwa kazi) kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa na Naibu wake, Phillip Mulugo, kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne.

  "Yatakuwa maandamano makubwa ya kuisimamisha nchi...tunataka siku hiyo mama ntilie wawe barabarani, watoto waliofeli na wazazi wao wawe barabarani, bodaboda wawe barabarani, wamachinga wawe barabarani, walimu wawe barabarani, wanafunzi walioko shuleni na vyuoni wawe barabarani, askari watuunge mkono.

  "Wazalendo wote watuunge mkono, Machi 25, 2013, Watanzania wawaoneshe watawala kuwa sauti ya wananchi ni kubwa na muhimu kuliko waziri mmoja na naibu wake...tunataka kitu kidogo tu, waziri na naibu wake wajiuzulu, tunataka wawajibike kwa matokeo mabaya ambayo yametuingiza kwenye kitabu cha maajabu ya dunia..., wanaume na wanawake siku hiyo hakuna mtu kubaki ndani.

  "Tutaisimamisha nchi katika majiji manne, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha...nanyi wa Musoma mnataka kulianzisha hapa? Haya Mbunge Nyerere wananchi wako nao wamesema watalianzisha hapa hapa, hawataki kuja Mwanza, kwa hiyo wa Butiama watashuka Musoma, wa Tarime watashuka hapa, wa Serengeti, Bunda na Mwibara, watashuka hapa, yataanzia wapi na kuelekea wapi, mtaambiwa hatua za baadae. Wananchi mjiandae Machi 25, maandamano na mgomo mkubwa," alisema Mbowe.


  2. Wawakilishi wa wananchi Vs the so called Kamati ya Ngwilizi


  Mwenyekiti Mbowe pia ametoa kauli na msimamo wa CHADEMA juu ya kuwepo kwa wito wa kile kinachoitwa kuwa ni Kamati ya Kudumu ya Kinga, Haki na Maadili ya Bunge chini ya uenyekiti wa Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi (Kamati ya Ngwilizi) kuwaita wabunge wa CHADEMA kutokana na kile kinachodaiwa kuwa vurugu zilizotokea bungeni siku ya Februari 4, 2013.


  Msimamo wa CHADEMA ni kwamba, wawakilishi hao wa wananchi hawatakwenda kuhojiwa kwenye hiyo Kamati ya Ngwilizi, kwa sababu za msingi zifuatazo; kamati hiyo haipo, kwa sababu kwa mujibu wa kanuni za bunge, kamati zote za bunge zilimaliza muda wake siku bunge lilipoahirishwa, Februari 8, 2013, baada ya mkutano wa 10 ambao ni nusu ya uhai wa bunge.  "Kwa mujibu wa kanuni ya bunge 113 kifungu kidogo cha 7 kinazungumzia ukomo wa uhai wa kamati za bunge ambao ni wakati wa Mkutano wa 10 wa bunge, yaani nusu ya uhai wa bunge. Hivyo kamati zote, ikiwemo hii ya Ngwilizi, zilishamaliza muda wake. Kanuni ya 113 kifungu cha 10, kinazungumzia position ya Mwenyekiti wa kamati na ukomo wake, Ngwilizi hana mamlaka tena, maana uenyekiti wake ulikwisha kuanzia Februari 8, 2010..."


  "Hivyo wawakilishi hao wa wananchi walioitwa, hawatakwenda, kuhojiwa, kama wanataka kutufukuza ubunge kwa maslahi ya CCM wajaribu waone...hawa ni wawakilishi wa watu, si suala la wabunge wa CHADEMA! Kama inafikia hatua wao wanaweza kufanyiwa vyovyote tu watu wanavyotaka, je mwananchi wa kawaida atapata wapi ya kuzungumza," amesema Mbowe.


  Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa CHADEMA inashangaa kuona wabunge wake leo wanaitwa kuhojiwa na Kamati ya Ngwilizi, kwa suala la vurugu za bungeni, Februari 4, 2013, wakati kamati hiyo hiyo ilishalishughulikia suala hilo hilo na ikatoa hukumu bila kuwasikiliza.


  "Leo ndiyo wamekumbuka kuhahalisha utaratibu mbovu na haramu waliotumia kushughulikia suala hilo...walitunga tuhuma, wakaendesha mashtaka, wakatoa hukumu na wakataja hata wakosaji kuwa ni Lissu, Mnyika, Gekul na Nassar, wakaitangazia dunia nzima, watanzania wote na nchi nzima ikaambiwa kuwa hawa ndiyo wakosaji...wakafanya hivyo bila kuwaita na kuwasikiliza hata siku moja, sasa ndiyo wameona umuhimu wa kuwaita, kwa utaratibu upi? Wanataka kusikiliza kitu gani wakati walishaamua na wakosaji wanajulikana?


  "Wanasahau kuwa kamati hiyo ni sawa na mahakama ya bunge, inapokaa ni sawa na mahakama, sasa kwa taratibu za mahakama, ikishashughulikia suala moja, haiwezi tena kukaa kushughulikia suala hilo hilo ambalo tayari imeshalitolea uamuzi. Tatu wito huu unakiuka katiba ya nchi na sheria...," alisema Mbowe mbele ya mkutano huo wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi wa Musoma na vitongoji vyake.


  Mbunge Vincent Nyerere azuiwa kwenda Kamati ya Bunge


  Wananchi wa Musoma waliohudhuria mkutano huo wa hadhara kwa kauli moja wamemzuia Mbunge wao Vincent Nyerere kuitikia wito wa kuhojiwa na kile kinachoitwa kuwa ni Kamati ya Ngwilizi, wakisema kuwa hiyo ni kinyume na misingi ya demokraia na uendeshaji wa shughuli za bunge.


  Wananchi hao walifikia uamuzi huo baada ya kuhojiwa na Mwenyekiti Mbowe, iwapo katika mazingira hayo (aliyoyaelezea mapema) iwapo wako tayari mbunge wao aitikie wito huo ambao umefikishwa kwake kwa barua ya kipolisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, nao wakasema 'asiende asiende...hatutaki aende...'

  More updates to come...
   

  Attached Files:

 2. M

  MALI MISANGO Member

  #2
  Mar 11, 2013
  Joined: Sep 17, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du,kwani kuandamana ndo suluhu,kimsingi hiyo haitasaidia,kitakachokuja ni raia kuswekwa rumande,je atakaye wapa dhamana ni nani ?Poleni mtakaoandamana mie naaona rundu la dola liko nyuma yao.
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 42,837
  Likes Received: 11,205
  Trophy Points: 280
  Bora tuisimamishe tuu hii nchi maana jk kashindwa kuiongoza yeye anachofanya ni kusafiri tuu!
   
 4. m

  majebere JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,439
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Siasa za matukio, hawa kwisha kazi yao.hamna sera tena, la ufisadi limevunda sasa wamebaki kusubiri matukio ndio wawike.Lissu amebuma Dar,Mnyika amebuma UK,Slaa kaingia mitini,lema amebaki kufoka foka kama muimba rap. M4C wamekosa usafiri baada ya mikweche yao kukwama kenya. Naona mtoa roho anazunguka anga za CDM
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2013
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,588
  Likes Received: 772
  Trophy Points: 280
  Roger that!
   
 6. Yegoo

  Yegoo JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2013
  Joined: Nov 14, 2012
  Messages: 1,303
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Eeen kimenuka tena!
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2013
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,298
  Likes Received: 2,439
  Trophy Points: 280
  Asije akaongea mengi akawatisha polisi, halafu wakatafuta sababu za kunyima kibali.
   
 8. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2013
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,297
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  SI MCHEZO... .
  serikali v/s sauti ya umma
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2013
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,073
  Likes Received: 3,295
  Trophy Points: 280
  Kuna siku watataka jambo gumu toka kwako, na kwa kuogopa 'rundu' la dola utawapa maana watakuwa nyuma yako
   
 10. m

  majebere JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,439
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Waunganishe na yale maandamano ya mnyika.
   
 11. m

  majebere JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,439
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  hilo tamko angetolea Dar kwenye ile nyomi ya lissu
   
 12. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2013
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,588
  Likes Received: 772
  Trophy Points: 280
  Itakuwa jumatatu, waajiriwa watapatikana?
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 805
  Trophy Points: 280
  Hakika hebu kweli watoto siku hizi wanafeli kiasi hicho? Huduma mbovu kila siku, mashuleni!! Mtoto hana msingi mzuri wa elimu toka shule ya awali amekuwa akisoma kwa mateso kukaa kwenye vumbi na chakula hakuna!! Mwishowe akimaliza shule anapata average ya alama D unampeleka shule ya kata hakuna mwalimu!!! Je huyu atafaulu kwa muujiza au ni vipi?
   
 14. M

  Mboko JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2013
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,066
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wewe Gamba huna lolote na huna ujualo zaidi ya kupalilia ajira yako uliyopata kwa kujuana,kumbuka maandamano ni sehemu kubwa sana tena sana ya kufikisha ujumbe,Juzi hapa Irak waliandamana waziri akajiuzulu so kwa nini unamtetea Kawambwa na wenzake who are you by the way let them go out
   
 15. Tony Gwanco

  Tony Gwanco JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2013
  Joined: Jan 22, 2013
  Messages: 5,921
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  umejuaje elimu kwanza we msukuma gani mwoga kama mbwa wa kijijini wasukuma wapo ngangali acha umaruhani
   
 16. m

  majebere JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,439
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  wewe unafikiri alikua anajua itakua jumatatu,mtu mwenyewe alikua amekolea lager.yeye ni kuropoka tu
   
 17. B

  BUMIJA MOSSES Member

  #17
  Mar 11, 2013
  Joined: Dec 5, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 15
  Tupo pamoja, tunasubiri kwa hamu hayo maandamano.

  "Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke"
   
 18. m

  majebere JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,439
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  acha hasira kijana
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2013
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Katika ulimwengu wa watu waliostaarabika kama hapa nchini Tanzania, Dr Kawambwa na msaidizi wake wala hawakuhitaji kusubiri mpaka wasukumwe nje ya ofisi kwa maandamano ya nguvu ya umma.
   
 20. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2013
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,389
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Wazazi wasiotomiza wajibu wao pia wajiuzuru. Na tunahitaji SERA ya CDM ya elimu ndio kiwe ni kigezo muhimu cha kuhitaji attention ya wanachi wote wa Tanzani. Waseme ni mfumo gani wa elimu wanaupendekeza utumike na kama ikishika dola tatizo hili watalitatuaje maana tunahitaji miaka kumi turudi kwenye mstari. Kumbukeni watoto wengi wapo sekondari hawajui kusoma na kuandika na ni ngumu kuwarejesha nyumbani watakosa kura na misaada.
   
Loading...