CCM hivi hamjui kwamba mnavyoendelea kuzuia mikutano yetu kwa kisingizo cha al-shababy na kuwabambikizia kesi za kipuuzi wapinzani, ndivyo mnavyotupa umaarufu mara mbili? Na ndivyo mnavyowazidishia hasira wananchi kwa serikali yenu? Kwa MwanaCCM yoyote mwenye akili anajua kuwa siku zenu zinahesabika, watu uraiani tuna hasira sana.
Waraka wa lema, Naamini unabeba kile kilicho moyoni kwake. Ninaamini jamii ina KIU ya Kutekelezewa kile alichooadika na Kuuamini. Ule waraka usomwe vizuri na serekali na igundue kuwa HAKUNA CHA KUUZUIA USITEKELEZWE .. na Kujaribu kuupigia dana dana .. NI KUONGEZA UMAARUFU kwa upande wasiotaka.
ngoja tuone kama watazuia huo mkutano kwa kisingizio cha allshababu
Ni vema serekali na wanaopinga mahitaji ya Jamii kama yalivyoaninishwa kwenye waraka wa Lema ... wawe makini ... Wakitaka watumie Historia wajaribu kugundua ... Nguvu ya serekali yeyote inaweza vipi kuzuia KIU ya jamii Kutaka Uadilifu na Haki kwenye nyanja kuu za kijamii, kiuchumi, kisiasa na ustawi kwa Ujumla.
Jk na wafuasi wako ujue kuwatenda wapinzani sio kigezo kwamba madarakani hamtaondolewa kuondolewa itabaki palepale na zaidi mnazidi kuwapa umaarufu
BUSARA zote zinaonyesha kuwa, Hakuna haja ya kuleta upinzani pale mtu au kikundi cha watu kweye jamii kinapopigania UTU na HESHIMA zake kwani HIZO ni nguvu kubwa sana kwenye jamii zisizo pingika ..kirahisi. Serekali ingibidi Itumie Busara na Hekima zote kuhakikisha kuwa Jambo hili linawezeshwa na kufanyika salama ...SIO KUWEKA VIZINGITI!!
I thiought Kivuyo anapenda kuwaona wapinzani wametoweka huku nje wawafungie wote so anaenda kufanya nini ? RCO yeye si yuko Arusha na ukweli anaujua kuna shida gani hadi aende gerezani kusema na Lema huko ?Mpwapwa si kasema Lema ana kesi na OCD wake anachunguzwa why tena mhalifu kama walivyo muita Mnaenda kuomba atoke ? Tangia wahalifu wakaombwa kutoka gerezani ? CCM haya mnayo yafanya mnajitakia shida baadaye .
Mkuu Lunyungu, You made a fantastic observation Sir!
Tuliiomba sana serekali watume watu waende gerezani ...waka..RECONCILE.. au wakayamalize na Lema Kwani Kile anachodai Lema though kinaweza kuonekana kama mtu atakavyotaka kukiona.. KINA MSINGI. Hata kama sio Lema atakaye kitekeleza na kukifanyia kazi lakini ..kiukweli kabisa Kwa zama tulizonazo ...TANZANIA UTU NA UBINADAMU kama msingi wa Utendaji kazi, kama sehemu ya Uongozi nk viko chini. Na Sio Lema, Yeyote akaanzisha VUGU VUGU la kuviamsha anaweza kupata wafuasi na watu wa ku m support!
Tukasema Serekali iachane kukimbizana na Lema kama wanafikiri Yeye hana hadhi ya kujenga VUVU VUGU HILO ... Na Serekali ichukue jukumu Hilo!
Tunafikiri sasa Serekali imesikia ushauri, Imekwenda kufanya maongezi ya kuyamaliza ... Na ... BILA SHAKA ... TUTAONA .. YOTE YALIYOANDKWA KWENYE WARAKA WA Hon G LEMA ... yakitekelezwa!
Kwani ni hakika ...UTU NA UBINAADAMU .. Inafika wakati ukadidimia ...na kupotea kabisa ..lakini Mtu makini akiliona hilo na kulifanyia timing ...anaweza kuanzisha vuguvugu lisilopongika .. atakuwa Lema? Tusibiri tuone!!
Lakini CCM na Serekali iliyoko madarakani ...Wanaeweza kuchukua jukumu hilo.. Na kufanya G LEMA kukosa cha kufanya na kumalizikiwa na NGUVU NA UMAARUFU!!
Time is due for this people to surrender,no where to escape.tatizo they never think twice.zaidi they never learn from the mistakes they keep on doing several mistakes.
Josephine ..? You have a great vision Dear!!! ... As far as am concerned ? ...You Just hit the point!!
Its not about G Lema neither CDM ... Its about human dignity, nobility and all about community Credibility .. THESE are Fundamental forces making the sound community ... You can not just come and stop them by whatever means...GUNS and Ammunition ...Stops..The fundamental forces of human and community development? ... A Big Joke..!!!
Ni Jukumu la serakali kusimamia kuwa ustawi wa
Utu na Ubindamu unakuwa na kukomaa sambamba na maendeleao ya
Vitu na mazingira ya jamii. Ustawi huu hauzuiliki kwa nguvu za Sillaha, Mabomu au Ubabe. NGUVU YA UTU... Inaweza kuzima mabomu yote ya NUKLIA duniani kwa sekunde moja.. Itakuwa risasi na maji ya washwasha...? Hata hivyo busara kidogo tu ... kama ambavyo imesha anza kutumika .. Itamaliza hili tatizo ... IHakikishe ..nadni ya Jamii KUNA KUHESHIMIANA, UPENDO, MATUMAINI NA HAKI ZA BINADAMU, hilo likifanyika ....utashangaa ... Dunia haihitaji ..MIJISILAHA na Makundi makubwa ya wanajeshi wamezagaa kila mahali!! ... Kasomeni tena ule ujumbe wa G Lema .. Unalilia hayo ...Msiupuuziee!! Ukilipuka bila kusimamiwa vizuri ... hakuna mtu atakaye taka kuona kitakacho tokea ..Na Kitajutiwa!!
Lema ni kiongozi shujaa mwenye ujasiri wa ukombozi wa mtanzania,tunamsubiri kesho kwa hamu,CCM inaangamiza maisha ya watu kila siku dola ipo juu,vyakula vimepanda,ajira hakuna now days na kama ikitokea wanapeana wao na watoto wao licha ya kuwa vilaza this is not fair at all,if this is not my I country could leave,but I have to fight till the end,and the freedom is coming.
Kwa ukweli kabisa . Mtanzania anahitaji ukombozi wa aina fulani... Sijui G Lema ametoa wapi yale Matamshi kwenye waraka wake na ana mpango gani kweli na kile alicho andika pale ... lakini ..Ule ujumbe ukiachiwa ukawafikia watanzania wakaamua kuutekeleza ... Unaweza kuanzisha vuguvugu ... ambalo Bora lisimamiwe Kwa Busara!!
Lema awe makini sana sana ndani miaka hii 3 maana ameshakuwa target kama Mwakyembe kama wamemkosa huko selo na kale ka sumu basi akae macho!!!!
Dhana aliyonayo MOYONI na hatimaye kuiweka HADHARANI kama Ujumbe kwenye waraka wake ... Ni mshale wa machungu kwa Mpinga Utu na Mpinga haki za Binadamu yeyote. LAKINI.. Fuatia historia ya ustawi na maendeleo ya jamii Kokote duniani. Kama vuguvugu likianza ... Hata wale viongozi wakiondoka kwa namna yeote .. Hakibadiliki Kitu!! Ni Matumaini Watanzania wana hekima na Busara ya kutosha kusimamia jambo hili liende vizuri.
Ukitaka kujua uwezo wa mtu kiakili mwache aongee. nadhani maneno yako yanaashiria uwezo wako wa kufikiri. Naomba waJF wakusamehe kwa kuwa hujui ulisemalo na wasikuhukumu.
Chieth na kuelewa!
Kuna watu wamesoma na wana digirii zote tatu ... na wakaanza tena nyanja nyingine...wakapata digirii tatu ...jumla sita! Unajua nini?? Wakifika nyumbani ... WANA KULA CHAKULA CHA WATOTO NA WANAKUWA WA KWANZA KUINGIA KITANDANI KULALA!!
Utasema hawajasoma hao? Wamesoma, Shule wamepandisha ... Lakini UTU?
SUFURI KABISA... UBINADAMU...?
0% Wanakula chakula cha watoto... AIBU !! Na nikweli ukitaka kuwaelewa vizuri waache waongeee na kuangalia VITENDO vyao...na Tabia zao!
Wasomi hao? Wape kazi ya kuweka mikataba... watakula chakula cha watoto ...kivipi unajua ...anahongwa..ka GX ... anaingia mkataba feki wa mamilioni ya faida kwa mwekezaji kwa miaka mia.. siunaona. Shule ..Kasoma madigirii yote..Lakini kweli ANA UTU NA UBINADAMU Huyo? Yeye kashiba na familia yake lakini jamii nzima ya Kitanzania inakufa njaa ya kila aina. AKILI MINGI lakini UTU NA UBINDAMU 0%. Hawa viogozi hawapooo? Hatutamaliza Kuonyesha udhaifu huu kwa jamii ya Tanznaia kwa Sasa. Ni kweli kabisa UTU na UBINADAMU uko chini sana na hilo halipingiki. Ndio Maana Taka tusitake ..VuguVugu lina kuja...Tunahijati Serekali ilisimamie liwe na AMANI na UTULIVU ... ni VuguVugu la Kurejesha UTU NA UBINADAMU ..soma waraka wa G Lema!!
Hata kama G Lema asingejitokeza kuanzisha vugu vugu hilo ... hakuna namna kwa vyovyote lisingekuja hasa ukitilia maanani kuwa SHINA LA UASISI WA TAIFA HILI NI UTU KUTAWALA KILA NYANJA YA KIJAMII. UTANZANIA NI UTU, UTU hauna DINI, UTU hauna Makabila, UTU hauna ITIKADI, UTU hauna JINSIA, UTU hauna MATABAKA, UTU hauna RANGI ...UTU ni UTANZANIA!!
Sioni ni kwanini CCM na Serekali isichukue jukumu la Kundesha Vuvu Vugu Hili!!!