Mbowe amliza Chami

Mbowe amliza Chami

Huu upuuzi wa Chami unatudhihirishia kuwa ccm ni chama kinachotuumiza watanzania na tunajuta sana kuwa na serikali inayofanya wajibu wake kwa misingi ya siasa za propaganda za kijinga zisizojali tanzania yetu ya kesho.

Tunapaswa kujengewa barabara nzuri kwasababu ni kodi zetu na ni haki yetu na sio kwasababu mbunge wa eneo husika ni ccm au mkazi wa eneo husika ni Anna Mkapa.

Huu ujinga wa ccm ni wa kuukomesha kwa kukiadhibu chama hichi kwa kukikataa kuanzia ngazi ya kata mpaka taifa.
Hatutavumilia ujinga huu kamwe.
Kataa ccm, kataa ushetani na uharamia wa wabunge wa ccm.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hawa ndio aina ya viongozi tuliowachagua

Naona huyu mkuu hapa ameleta wivu wa kike kabisa baadala ya kusema barabara zake zijengwe ka lami anataka watu wote wakose kisa yeye amekosa.

What do you expect from a CCM lad!!
 
Sasa anataka nini mbona watalia wengi tu 2015 cha msingi budget ya mazishi iongezwe wengi watakuwa puzzled na uchaguzi wa 2015 huu mwanzo stroke zitawaua wengi baada ya kupoteza ubunge!!!!
 
CDM ndio dira ya maendeleo bila kuitaja viongozi hawafanyi kazi.
 
hakuna sauti isiyo sikika ,na sauti inayo toka kwa ajiri ya watu haziitwi kelele ........endelea kuongea watasikia.
 
Labda mwenzie anafuatilia,angetakiwa kumuona Mbowe amuulize amefanyaje mpaka amefanikiwa.Labda wamechangishana
 
Walimuibia mgombea wetu wa chadema 2010 waziwazi eti kisa uwaziri, sasa hakuna cha uwaziri wala ilani ya ccm. Kilio chao 2015.
 
Barabara ya Old Moshi inayoanzia barabara kuu iendayo Dar es Salaam kupitia Kiboriloni Primari, kijiji cha Kikarara, kijiji cha Tsuduni hadi kijiji cha Kidia (km 19.8) katika Kata ya Old Moshi Mashariki, pia ni ahadi nyingine ya Rais aliyoitoa wakati wa kampeni za 2010 eneo la Tsuduni na imeingizwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa 2011-2016, alisema Chami.

“Inaelekea ahadi ya barabara hii hata haifahamiki kabisa, kwa sababu hata katika taarifa mbalimbali kwa viongozi wa kitaifa wanaotembelea Kilimanjaro haisikiki. Kumbe nimeona niukumbushe uongozi wa Tanroads mkoa na wa Wizara ya Ujenzi juu ya barabara hii, japo natambua uwapo wa mawasiliano kati ya Mama Anna Mkapa (mzaliwa wa Kijiji cha Kikarara) na Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli juu ya ujenzi wa barabara hii,” alieleza Chami.

Hii barabara ni mfano dhahiri wa chuki na kisasi cha CCM na Serikali yake. Itakumbukwa kwamba ( I stand to be corrected) katika uchaguzi wa mwaka 1995, Mh Dr Augustino Lyatonga Mrema, alipata kura nyingi sana maeneo ya Moshi. Kwa hasira, mkapa alinukuliwa kuahidi kuwa maendeleo hayatafika moshi vijijini, hasa baada ya eneo ambalo mkewe ametoka (barabara tajwa hapo juu) kukataa kumpa kura. Toka hapo, barabara hii imekuwa ikiachwa iharibike na wakati mwingine wanaiwekea moram au kuichimba jambo ambalo limepelekea vumbi kali wakati wa jua na utelezi wakati wa mvua. Katika chaguzi za 2005 inaaminika Chadema ilikuwa na ushawishi mkubwa. Kadhalika 2010. Upepo wa kisiasa haukuwa mzuri kabisa 2010 hasa baada ya wakazi kuikataa ccm kwa kuwa imepuuza kero zao kubwa za maji na barabara. Hapo ililazimika Kikwete mwenyewe kuja na kuwaahidi (kuwadanganya) kuwa barabara hiyo ingejengwa kwa lami! Alifanikiwa kupata kura (inawezekana nyingine ziliibwa kujazilizia) lakini amewasahau wakazi hao, kama kawaida!
 
Hili li jamaa libnafsi sana tena halina sifa ya uongozi. ataishia tu kulalmika mara 2015. Hatakiwi kabisa............ naona sasa anawachefua hata wake waliomwonea huruma baada ya kulambishwa tope kwenye uwaziri. hivi hiyo Phd ina uhalali kweli?
 
uchaguzi ujao hawatakuwa wana ahidi ovyoovyo maana ahadi hewa ndio zinaenda kuiangusha ccm. hizi ni nyakati za kutenda unachokisema na kusema unachokitenda
 
uchaguzi ujao hawatakuwa wana ahidi ovyoovyo maana ahadi hewa ndio zinaenda kuiangusha ccm. hizi ni nyakati za kutenda unachokisema na kusema unachokitenda
 
Back
Top Bottom