Mbowe amlipua JK

Mbowe amlipua JK

Mimi huwa nadhani huwa wanamaanisha 'wananchi wengi' badala ya kusema tu wananchi ili kuepuka maswali ya namba na jinsi zilivyopatika katika context ya wananchi.

Tatizo la wanasiasa wetu wengi pia huwa siyo makini sana katika maana ya kila neno wanalolisema na pale inapotokea watu makini wakagundua mapungufu katika kauli zao, utawasikia wanasiasa wetu wakisema 'wamenukuliwa' kimakosa.

Wanasiasa wengine wanapenda sana kujificha kwenye kauli tata kama hizi as we know, Politics, after all, is the art of persuasion and manipulation!.
Mfano ni wewe mwenyewe umekana kauli zako nyingi na unajikanganya sana
 
Mh Freeman Mbowe
Wednesday, February 5, 2014
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemvaa Rais Jakaya Kikwete, akimtaka kuacha kutafuta huruma ya Watanzania juu ya suala la Katiba na badala yake atumie nafasi hiyo kuwataka wabunge wake kuheshimu maoni ya wananchi.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete juzi kwamba Katiba haiwezi kupatikana kwa ngumi imejaa upotoshaji kwa wananchi.

Katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika mkoani Mbeya, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alimshangaa Mbowe kwa kauli yake kwamba mfumo wa serikali tatu ukikataliwa katika Bunge hilo nchi haitatawalika.

“Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa,” alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mbowe alisema ni vema Rais Kikwete akaacha kuhangaika na wapinzani, badala yake awe tayari kuheshimu mawazo ya wananchi waliyotoa wakati wa kutoa maoni ya Katiba.

Mbowe alisema kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa na mtu anayejaribu kupotosha hoja, kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo.
Alisema kuwa viongozi wa CCM wamekuwa wakilazimisha ajenda ya Katiba mpya kuonekana kama sera yao, jambo ambalo CHADEMA haiwezi kuafiki.

“Katiba ni ya wananchi, si ya chama chochote cha siasa, ndiyo maana hatukubali kuona mawazo ya wananchi yakishindwa kuheshimiwa,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba imefanya kazi nzuri ambapo Rais Kikwete na wabunge wake wanapaswa kuheshimu mchango huo.

Alisema kuwa CHADEMA itahakikisha inashindana kwa hoja katika Bunge la Katiba litakaloketi hivi karibuni na iwapo hilo litashindikana watarudi kwa wananchi ambao ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.

“Wajumbe watakaoshiriki Bunge la Katiba ni 640 ambao hao si waamuzi wa mwisho na kama tutaona kuna suala lolote linaloenda kinyume, sisi tutakachokifanya ni kurudi kwa wananchi kuwaeleza juu ya kilichotokea na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho katika kura ya maoni,” alisema.

Mbowe alisema kuwa hata katika kushindana kwa hoja CCM wanapaswa wasiweke hila, maana wataweza kuchangia mchakato huo kushindwa kufanikiwa.
Alisema kuwa nia ya CHADEMA ni kuhakikisha Katiba nzuri, bora na iliyo ya wananchi inapatikana na si kusababisha vurugu kama ambavyo Rais Kikwete amejaribu kupotosha.
“Hila hiyo imeonekana wazi maana kuna hali ya kutaka kupuuza mawazo ya wananchi na CCM kulazimisha mawazo yao, hilo hatutalikubali na tutapambana…hiyo si mara ya kwanza kupambana katika suala hilo,” alisema.

Mbowe alisema kuwa kuhusu serikali tatu ni muhimu Rais Kikwete akaheshimu mawazo hayo na CHADEMA itashindana kwa hoja juu ya suala hilo ili kuhakikisha mawazo hayo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba yanaheshimiwa.

Katika ziara ya mikutano ya hadhara ya CHADEMA iliyopewa jina la Operesheni M4C Pamoja Daima, Mbowe na viongozi wengine waliionya Serikali ya CCM kutochakachua mchakato wa Katiba, kwani Watanzania hawako tayari kurudi kwenye Katiba ya sasa ambayo alidai imekosa uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema CCM kwa kutumia wabunge wake wakiamua kuhujumu mchakato huo bungeni, yeye na viongozi wenzake watapita nchi nzima kuwataka wananchi wasishiriki kura za maoni na yuko tayari kufunguliwa kesi kwa kudai Katiba mpya.
Posted by Chadema Blogtz at 3:18 AM

Sauti ya umma Ni sauti ya Mungu....Mh Mbowe anasimamia kauli ya Umma ambayo Mh Warioba aliiwakilisha kupitia Rasimu ya Katiba. Hivyo wanaoipinga kauli hii ya umma, Ni wale Tu wanaoongozwa na mkono WA shetwani...na ndio mhimili WA uovu ambao CCM imejishikiza. Kuupinga umma Ni kumpinga Mungu, na mpinzani WA Mungu kwa vizazi na vizazi Ni ibilisi, na CCM inasimama ktk mstari huo muovu ILA itashindwa na kutupwa ktk abyss, yaani shimoni kama shetwani, na ndiko tuendako sasa na CCM hii! Watanzania walishaamua, walishafikia mwisho WA maamuzi Yao. Katiba mpya inayowafaa ndio jibu sahihi. Anayeipotosha, kuipinga au kuihujumu hastahili kuwepo ktk historia ya Tanganyika mpya!
 
hakafu mbona presidaa alisema hadi jumanne majina ya wabunge la katiba atakuwa kashayataja?sasa ishapita siku moja tayari
 
Mbowe angeenda shule asingeongea huu ujinga hapo juu! Shule inasaidia sana, hata uwe na fedha vipi kama hujaenda shule huwezi kuwa na hoja iliyosimama ipasavyo!

kwahiyo elimu yako wewe ndio ya kujiita msalani nyie mliozaliwa kupitia masabuli mna tabu.
 
Lakini kweli kuna mara nyingi waandishi wetu uwanukuu vibaya (au kwa makusudi)...
Yes, lakini tukubaliane mara nyingi sana wanasiasa wetu wengi ni wabovu sana katika kufikiria athari au matokeo ya kile wanachokisema katika jamii na hii inatokana na ukosefu wa taaluma au experiance katika mawasiliano na sheria.

Ukiangalia nchi zilizoendelea ambazo tunataka tuwe kimaendeleo kama wao, utagundua kuwa wanasiasa wengi wazuri kihoja, kimantiki na vision ni wataalam wa sheria, sayansi ya siasa na kiuchumi.

It makes a lot of sense and big difference to our politics.
 
Sauti ya umma Ni sauti ya Mungu....Mh Mbowe anasimamia kauli ya Umma ambayo Mh Warioba aliiwakilisha kupitia Rasimu ya Katiba. Hivyo wanaoipinga kauli hii ya umma, Ni wale Tu wanaoongozwa na mkono WA shetwani...na ndio mhimili WA uovu ambao CCM imejishikiza. Kuupinga umma Ni kumpinga Mungu, na mpinzani WA Mungu kwa vizazi na vizazi Ni ibilisi, na CCM inasimama ktk mstari huo muovu ILA itashindwa na kutupwa ktk abyss, yaani shimoni kama shetwani, na ndiko tuendako sasa na CCM hii! Watanzania walishaamua, walishafikia mwisho WA maamuzi Yao. Katiba mpya inayowafaa ndio jibu sahihi. Anayeipotosha, kuipinga au kuihujumu hastahili kuwepo ktk historia ya Tanganyika mpya!
Wanaopinga wana haki iliyosawa na wale wasiopinga kwa sababu maoni yao kama binadamu hayatofautiani katika macho ya mwenyezi Mungu. Kwani si tunaambiwa kuwa Mungu anawapenda wanae wote na wote kwake wako sawa! Itakuwaje tena wana wa Mungu wawe wanaongozwa na mkono wa shetani wakati Baba yao yupo kila sekunde katika njia zao!.
Matthew 7:1-4,
1 "Do not judge so that you will not be judged.
2 For by the standard you judge you will be judged, and the measure you use will be the measure you receive.
3 Why do you see the speck in your brother's eye, but fail to see the beam of wood in your own?
4 Or how can you say to your brother, 'Let me remove the speck from your eye,' while there is a beam in your own?
 
Mh Freeman Mbowe
Wednesday, February 5, 2014
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemvaa Rais Jakaya Kikwete, akimtaka kuacha kutafuta huruma ya Watanzania juu ya suala la Katiba na badala yake atumie nafasi hiyo kuwataka wabunge wake kuheshimu maoni ya wananchi.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete juzi kwamba Katiba haiwezi kupatikana kwa ngumi imejaa upotoshaji kwa wananchi.

Katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika mkoani Mbeya, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alimshangaa Mbowe kwa kauli yake kwamba mfumo wa serikali tatu ukikataliwa katika Bunge hilo nchi haitatawalika.

“Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa,” alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mbowe alisema ni vema Rais Kikwete akaacha kuhangaika na wapinzani, badala yake awe tayari kuheshimu mawazo ya wananchi waliyotoa wakati wa kutoa maoni ya Katiba.

Mbowe alisema kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa na mtu anayejaribu kupotosha hoja, kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo.
Alisema kuwa viongozi wa CCM wamekuwa wakilazimisha ajenda ya Katiba mpya kuonekana kama sera yao, jambo ambalo CHADEMA haiwezi kuafiki.

“Katiba ni ya wananchi, si ya chama chochote cha siasa, ndiyo maana hatukubali kuona mawazo ya wananchi yakishindwa kuheshimiwa,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba imefanya kazi nzuri ambapo Rais Kikwete na wabunge wake wanapaswa kuheshimu mchango huo.

Alisema kuwa CHADEMA itahakikisha inashindana kwa hoja katika Bunge la Katiba litakaloketi hivi karibuni na iwapo hilo litashindikana watarudi kwa wananchi ambao ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.

“Wajumbe watakaoshiriki Bunge la Katiba ni 640 ambao hao si waamuzi wa mwisho na kama tutaona kuna suala lolote linaloenda kinyume, sisi tutakachokifanya ni kurudi kwa wananchi kuwaeleza juu ya kilichotokea na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho katika kura ya maoni,” alisema.

Mbowe alisema kuwa hata katika kushindana kwa hoja CCM wanapaswa wasiweke hila, maana wataweza kuchangia mchakato huo kushindwa kufanikiwa.
Alisema kuwa nia ya CHADEMA ni kuhakikisha Katiba nzuri, bora na iliyo ya wananchi inapatikana na si kusababisha vurugu kama ambavyo Rais Kikwete amejaribu kupotosha.
“Hila hiyo imeonekana wazi maana kuna hali ya kutaka kupuuza mawazo ya wananchi na CCM kulazimisha mawazo yao, hilo hatutalikubali na tutapambana…hiyo si mara ya kwanza kupambana katika suala hilo,” alisema.

Mbowe alisema kuwa kuhusu serikali tatu ni muhimu Rais Kikwete akaheshimu mawazo hayo na CHADEMA itashindana kwa hoja juu ya suala hilo ili kuhakikisha mawazo hayo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba yanaheshimiwa.

Katika ziara ya mikutano ya hadhara ya CHADEMA iliyopewa jina la Operesheni M4C Pamoja Daima, Mbowe na viongozi wengine waliionya Serikali ya CCM kutochakachua mchakato wa Katiba, kwani Watanzania hawako tayari kurudi kwenye Katiba ya sasa ambayo alidai imekosa uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema CCM kwa kutumia wabunge wake wakiamua kuhujumu mchakato huo bungeni, yeye na viongozi wenzake watapita nchi nzima kuwataka wananchi wasishiriki kura za maoni na yuko tayari kufunguliwa kesi kwa kudai Katiba mpya.
Posted by Chadema Blogtz at 3:18 AM

JK nilikuwa namkubali sana alivyoanza kwenye mchakato wa kutafuta katiba mpya, lakini inaonekana makada wa CCM wamemkalia kooni sn na kuanza kuropoka kama akina Kinana na wenzake.,

Ni vyema angebaki kimya na zaidi akawataka na kuhimiza watu kwenye bunge la katiba wachangie vyema ili kupata katiba itakayowafaa watanzania wote wakiwemo na wasio na vyama., lakini kuja kwenye majukwaa na kutamka chama changu kinataka serikali 2 hapa amefanya ujuha wa hali juu kabisa.,

Sasa kama chama chako kinataka mfumo wa serikali 2 kwanini uliruhusu mchakato wa katiba mpya na serikali 2 zipo sasa?? ilikuwa tuendelee nazo tu, hawa CCM ovyo sana wanaogopa na kutishana tishana hata Rais anakuwa hana mamlaka lazima afuate na kuburuzwa na watu wachache hii nchi bado sn.,
 
Tatizo la Mbowe ni shule.

huhitaji shule kujua tume ya katiba ilichokuwa inakifanya kunahitajika uwazi zaidi kwa kuwa suala linagusa wananchi ambao ndio wameamua serikali tatu , kusimamia hotuba za mwalimu kwa karne hii ni kufilisika kisiasa zilikuwa na mashiko wakati huo sio sasa la msingi si hoja ni kusimamia utashi wa wananchi katiba sio ya ccm ni kwa ajili ya nchi na taifa kwa ujumla wenye ,mamlaka ya kukataa viongozi ni wananchi sauti zao zisipuuzwe idumu tanzania
 
Kila mmwamba ngoma kamba huvutia kwake. CHADEMA watavutia kwao na CCM watavutia kwao pia. Yule atakayeshindwa ndo kashindwa sasa ugomvi wa nini kwenye mchezo. Usitegemee mvuta kamba wa CCM avutie upande wa CHADEMA, CHADEMA hali kadhalika. Upande utakaoshindwa ujipange upya. Hakuna dhambi Raisi Kikwete kuvutia upande wa CCM na Mbowe naye akivutia CHADEMA ndiyo halali yake. Kikwete katoa hoja Mbowe naye anatoa hoja yake. Sasa Mbowe alitaka Kikwete atoe hoja Mbowe? Haiwezekani.
Hoja ya kusema tunataka Katiba ni ya nchi nzima sio ya chama haina mshiko kwa sababu nchi sio ardhi ni watu na watu ndiyo wenye maslahi iwe mmoja mmoja au kwenye vikundi vyao kama vile CCM, CHADEMA CUF NCCR Mageuzi vikundi vya dini NGOs nk. Kupata katiba itakayokuwa haiangalii maslahi ya vyama vya siasa haitawezekana. Hata wanaosema tuwe na muungano wa serikali tatu wanayaona maslahi ndani serikali tatu

Ni kweli unachosema,ila nilitaka uhakika kama mbowe asema neno'NGUMI' .
 
Mwambieni MBOWE aache kulalamika majukwaani, wafunde Wabunge wake waende DODOMA wakiwa na hoja badala ya ujinga ujinga tena.

kama Lisu akitolewa nje ya bunge kisa ANACHANGIA SANA je?nao ni ujinga ujinga?
 
Sina hakika kama umefikiri vizuri ulipoandika maneno niliyowekea rangi .Hotuba za Nyerere zilikuwa zinafichua mambo ya mbele zaidi hata kabla ya karne kufikiwa. Hili halionekani na mimi peke yangu linaonekana hata na wazuoni wengine. Mifano ya aliyoyasema yakaonekana baadaye ni mingi, lakini kwa kukusaidia nitaje michache. Ukiona mtu anakimbilia Ikulu, mwogope kama ukoma. Waliokimbilia Ikulu hatukuwagopa matokeo tumeyaona.
Dhambi ya ubaguzi ukiianza haitakuacha. Mtaendelea kubaguana. Tumeiona Sudani kusini.
Lakini nisikulaumu sana kwa sababu kufikiri vizuri sio jambo jepesi ingawaje kila mtu huwa anafikiri. Lakini hata kama utafikiri vizuri kukumbuka pia ni jambo gumu huwenda unashindwa kuyakumbuka aliyoyasema Nyerere yaliyombele ya wakati hadi sasa. Hata wanaodai serikali tatu ni wale waliokwisha sahau mawazo yake kuwa huo nia aina ya ubaguzi unaotokana na ulevi tu hasa ulevi wa madaraka. Kutaka bendera, wimbo wa taifa kupigiwa mizinga. Nyerere alisema Rais achaguliwe kwa sifa alizonazo na sio kabila lake. Anazo sifa zooote, lakini Ahh! Mkara. Hana sifa hata moja ya kuwa Rais lakini mimi namtaka Seif Sharif Hamad. Kwa nini? Mpemba bwana.
Haya ndiyo yanayofanyika sasa miaka 14 baada ya kifo chake. Nani kapitwa na wakati? Nani kafirisika kisiasa?
huhitaji shule kujua tume ya katiba ilichokuwa inakifanya kunahitajika uwazi zaidi kwa kuwa suala linagusa wananchi ambao ndio wameamua serikali tatu , kusimamia hotuba za mwalimu kwa karne hii ni kufilisika kisiasa zilikuwa na mashiko wakati huo sio sasa la msingi si hoja ni kusimamia utashi wa wananchi katiba sio ya ccm ni kwa ajili ya nchi na taifa kwa ujumla wenye ,mamlaka ya kukataa viongozi ni wananchi sauti zao zisipuuzwe idumu tanzania
 
Yes, lakini tukubaliane mara nyingi sana wanasiasa wetu wengi ni wabovu sana katika kufikiria athari au matokeo ya kile wanachokisema katika jamii na hii inatokana na ukosefu wa taaluma au experiance katika mawasiliano na sheria.

Ukiangalia nchi zilizoendelea ambazo tunataka tuwe kimaendeleo kama wao, utagundua kuwa wanasiasa wengi wazuri kihoja, kimantiki na vision ni wataalam wa sheria, sayansi ya siasa na kiuchumi.

It makes a lot of sense and big difference to our politics.
Wenzetu pia wanasaidiwa na uwazi uliopo. Ukidai umenukuliwa vibaya, chombo hicho cha habari inatia mkanda na kulinganisha kauli yako na madai yako. Huku kwetu mwanasiasa akisema amenukuliwa vibaya anasaidiwa kuficha ukweli na kukazia ukanushaji wake huo.
 
Back
Top Bottom