Mbowe amlipua JK

Mbowe amlipua JK

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
[h=1][/h]
Mh Freeman Mbowe
Wednesday, February 5, 2014
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemvaa Rais Jakaya Kikwete, akimtaka kuacha kutafuta huruma ya Watanzania juu ya suala la Katiba na badala yake atumie nafasi hiyo kuwataka wabunge wake kuheshimu maoni ya wananchi.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete juzi kwamba Katiba haiwezi kupatikana kwa ngumi imejaa upotoshaji kwa wananchi.

Katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika mkoani Mbeya, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alimshangaa Mbowe kwa kauli yake kwamba mfumo wa serikali tatu ukikataliwa katika Bunge hilo nchi haitatawalika.

“Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa,” alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mbowe alisema ni vema Rais Kikwete akaacha kuhangaika na wapinzani, badala yake awe tayari kuheshimu mawazo ya wananchi waliyotoa wakati wa kutoa maoni ya Katiba.

Mbowe alisema kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa na mtu anayejaribu kupotosha hoja, kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo.
Alisema kuwa viongozi wa CCM wamekuwa wakilazimisha ajenda ya Katiba mpya kuonekana kama sera yao, jambo ambalo CHADEMA haiwezi kuafiki.

“Katiba ni ya wananchi, si ya chama chochote cha siasa, ndiyo maana hatukubali kuona mawazo ya wananchi yakishindwa kuheshimiwa,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba imefanya kazi nzuri ambapo Rais Kikwete na wabunge wake wanapaswa kuheshimu mchango huo.

Alisema kuwa CHADEMA itahakikisha inashindana kwa hoja katika Bunge la Katiba litakaloketi hivi karibuni na iwapo hilo litashindikana watarudi kwa wananchi ambao ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.

“Wajumbe watakaoshiriki Bunge la Katiba ni 640 ambao hao si waamuzi wa mwisho na kama tutaona kuna suala lolote linaloenda kinyume, sisi tutakachokifanya ni kurudi kwa wananchi kuwaeleza juu ya kilichotokea na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho katika kura ya maoni,” alisema.

Mbowe alisema kuwa hata katika kushindana kwa hoja CCM wanapaswa wasiweke hila, maana wataweza kuchangia mchakato huo kushindwa kufanikiwa.
Alisema kuwa nia ya CHADEMA ni kuhakikisha Katiba nzuri, bora na iliyo ya wananchi inapatikana na si kusababisha vurugu kama ambavyo Rais Kikwete amejaribu kupotosha.
“Hila hiyo imeonekana wazi maana kuna hali ya kutaka kupuuza mawazo ya wananchi na CCM kulazimisha mawazo yao, hilo hatutalikubali na tutapambana…hiyo si mara ya kwanza kupambana katika suala hilo,” alisema.

Mbowe alisema kuwa kuhusu serikali tatu ni muhimu Rais Kikwete akaheshimu mawazo hayo na CHADEMA itashindana kwa hoja juu ya suala hilo ili kuhakikisha mawazo hayo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba yanaheshimiwa.

Katika ziara ya mikutano ya hadhara ya CHADEMA iliyopewa jina la Operesheni M4C Pamoja Daima, Mbowe na viongozi wengine waliionya Serikali ya CCM kutochakachua mchakato wa Katiba, kwani Watanzania hawako tayari kurudi kwenye Katiba ya sasa ambayo alidai imekosa uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema CCM kwa kutumia wabunge wake wakiamua kuhujumu mchakato huo bungeni, yeye na viongozi wenzake watapita nchi nzima kuwataka wananchi wasishiriki kura za maoni na yuko tayari kufunguliwa kesi kwa kudai Katiba mpya.
Posted by Chadema Blogtz at 3:18 AM
 
"kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo".kumbe mbowe hakusema watapigana ngumi bungeni?basi ile kauli ya 'nimeambiwa' bado inaendelea.
 
kichwa cha habari namaelezo yaliyo ndani ni tofauti. headline ingerekibishwa ingeleta maana nzuri kweli.
 
"Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa," alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mbowe alisema ni vema Rais Kikwete akaacha kuhangaika na wapinzani, badala yake awe tayari kuheshimu mawazo ya wananchi waliyotoa wakati wa kutoa maoni ya Katiba.

Mbowe alisema kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa na mtu anayejaribu kupotosha hoja, kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo.
Alisema kuwa viongozi wa CCM wamekuwa wakilazimisha ajenda ya Katiba mpya kuonekana kama sera yao, jambo ambalo CHADEMA haiwezi kuafiki.

"Katiba ni ya wananchi, si ya chama chochote cha siasa, ndiyo maana hatukubali kuona mawazo ya wananchi yakishindwa kuheshimiwa," alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba imefanya kazi nzuri ambapo Rais Kikwete na wabunge wake wanapaswa kuheshimu mchango huo.

Alisema kuwa CHADEMA itahakikisha inashindana kwa hoja katika Bunge la Katiba litakaloketi hivi karibuni na iwapo hilo litashindikana watarudi kwa wananchi ambao ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.

"Wajumbe watakaoshiriki Bunge la Katiba ni 640 ambao hao si waamuzi wa mwisho na kama tutaona kuna suala lolote linaloenda kinyume, sisi tutakachokifanya ni kurudi kwa wananchi kuwaeleza juu ya kilichotokea na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho katika kura ya maoni," alisema.

Mbowe alisema kuwa hata katika kushindana kwa hoja CCM wanapaswa wasiweke hila, maana wataweza kuchangia mchakato huo kushindwa kufanikiwa.
Alisema kuwa nia ya CHADEMA ni kuhakikisha Katiba nzuri, bora na iliyo ya wananchi inapatikana na si kusababisha vurugu kama ambavyo Rais Kikwete amejaribu kupotosha.
"Hila hiyo imeonekana wazi maana kuna hali ya kutaka kupuuza mawazo ya wananchi na CCM kulazimisha mawazo yao, hilo hatutalikubali na tutapambana…hiyo si mara ya kwanza kupambana katika suala hilo," alisema.

Mbowe alisema kuwa kuhusu serikali tatu ni muhimu Rais Kikwete akaheshimu mawazo hayo na CHADEMA itashindana kwa hoja juu ya suala hilo ili kuhakikisha mawazo hayo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba yanaheshimiwa.

Katika ziara ya mikutano ya hadhara ya CHADEMA iliyopewa jina la Operesheni M4C Pamoja Daima, Mbowe na viongozi wengine waliionya Serikali ya CCM kutochakachua mchakato wa Katiba, kwani Watanzania hawako tayari kurudi kwenye Katiba ya sasa ambayo alidai imekosa uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema CCM kwa kutumia wabunge wake wakiamua kuhujumu mchakato huo bungeni, yeye na viongozi wenzake watapita nchi nzima kuwataka wananchi wasishiriki kura za maoni na yuko tayari kufunguliwa kesi kwa kudai Katiba mpya.
Posted by Chadema Blogtz at 3:18 AM

ANA WASI WASI wa nini, waende Dodoma kitaeleweka huko huko. Ni kama anatwanga maji kwnye kinyu, huu siyo muda wa kuwahadaa watanzania mambo yote iko Dodoma, jambo la msingi wabunge wake wajipange kwa hoja na siyo madudu yale ya akina SUGU.
 
Mh Freeman Mbowe
Wednesday, February 5, 2014
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemvaa Rais Jakaya Kikwete, akimtaka kuacha kutafuta huruma ya Watanzania juu ya suala la Katiba na badala yake atumie nafasi hiyo kuwataka wabunge wake kuheshimu maoni ya wananchi.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete juzi kwamba Katiba haiwezi kupatikana kwa ngumi imejaa upotoshaji kwa wananchi.

Katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika mkoani Mbeya, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alimshangaa Mbowe kwa kauli yake kwamba mfumo wa serikali tatu ukikataliwa katika Bunge hilo nchi haitatawalika.

“Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa,” alisema.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mbowe alisema ni vema Rais Kikwete akaacha kuhangaika na wapinzani, badala yake awe tayari kuheshimu mawazo ya wananchi waliyotoa wakati wa kutoa maoni ya Katiba.

Mbowe alisema kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa na mtu anayejaribu kupotosha hoja, kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo.
Alisema kuwa viongozi wa CCM wamekuwa wakilazimisha ajenda ya Katiba mpya kuonekana kama sera yao, jambo ambalo CHADEMA haiwezi kuafiki.

“Katiba ni ya wananchi, si ya chama chochote cha siasa, ndiyo maana hatukubali kuona mawazo ya wananchi yakishindwa kuheshimiwa,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba imefanya kazi nzuri ambapo Rais Kikwete na wabunge wake wanapaswa kuheshimu mchango huo.

Alisema kuwa CHADEMA itahakikisha inashindana kwa hoja katika Bunge la Katiba litakaloketi hivi karibuni na iwapo hilo litashindikana watarudi kwa wananchi ambao ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.

“Wajumbe watakaoshiriki Bunge la Katiba ni 640 ambao hao si waamuzi wa mwisho na kama tutaona kuna suala lolote linaloenda kinyume, sisi tutakachokifanya ni kurudi kwa wananchi kuwaeleza juu ya kilichotokea na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho katika kura ya maoni,” alisema.

Mbowe alisema kuwa hata katika kushindana kwa hoja CCM wanapaswa wasiweke hila, maana wataweza kuchangia mchakato huo kushindwa kufanikiwa.
Alisema kuwa nia ya CHADEMA ni kuhakikisha Katiba nzuri, bora na iliyo ya wananchi inapatikana na si kusababisha vurugu kama ambavyo Rais Kikwete amejaribu kupotosha.
“Hila hiyo imeonekana wazi maana kuna hali ya kutaka kupuuza mawazo ya wananchi na CCM kulazimisha mawazo yao, hilo hatutalikubali na tutapambana…hiyo si mara ya kwanza kupambana katika suala hilo,” alisema.

Mbowe alisema kuwa kuhusu serikali tatu ni muhimu Rais Kikwete akaheshimu mawazo hayo na CHADEMA itashindana kwa hoja juu ya suala hilo ili kuhakikisha mawazo hayo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba yanaheshimiwa.

Katika ziara ya mikutano ya hadhara ya CHADEMA iliyopewa jina la Operesheni M4C Pamoja Daima, Mbowe na viongozi wengine waliionya Serikali ya CCM kutochakachua mchakato wa Katiba, kwani Watanzania hawako tayari kurudi kwenye Katiba ya sasa ambayo alidai imekosa uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema CCM kwa kutumia wabunge wake wakiamua kuhujumu mchakato huo bungeni, yeye na viongozi wenzake watapita nchi nzima kuwataka wananchi wasishiriki kura za maoni na yuko tayari kufunguliwa kesi kwa kudai Katiba mpya.
Posted by Chadema Blogtz at 3:18 AM
Magamba wanapita wakati mgumu sana hivyo kuto matamko mbalimbali ni jambo linalo tegemewa.Hivi sasa hata Makonda naye anatoa tamko na linajadiliwa.Kigunge naye anasema Haoni ubaya wa Lowasa kujipitisha kusaka Uraisi.Ni alimradi tu kuonyesha kutoweka kwa mshikamano wa hapo awali
 
"kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo".kumbe mbowe hakusema watapigana ngumi bungeni?basi ile kauli ya 'nimeambiwa' bado inaendelea.

Mwambieni MBOWE aache kulalamika majukwaani, wafunde Wabunge wake waende DODOMA wakiwa na hoja badala ya ujinga ujinga tena.
 
haya yana uhusiano gani na mada iliyoko jukwaani au unaota.
 
kichwa cha habari namaelezo yaliyo ndani ni tofauti. headline ingerekibishwa ingeleta maana nzuri kweli.

Mkuu hiyo mada imerudiwa rudiwa mara kibao na haina mashiko na ndiyo haina hoja za msingi.
 
Binfsi huwa nashangaa sana, unaposema katiba ni ya wananchi hivyo mawazo ya wananchi yaheshimiwe je kupinga mwazo ya wananchi wanaotaka serikali mbili kunakofanywa na Chadema je huko si kudharau mawazo ya wananchi? Au kwa wao Chadema wananchi ni wale tu wanaotaka serikali tatu?
 
Mbowe angeenda shule asingeongea huu ujinga hapo juu! Shule inasaidia sana, hata uwe na fedha vipi kama hujaenda shule huwezi kuwa na hoja iliyosimama ipasavyo!
 
Hana jipya , anatafuta huruma ya wafuasi wake wamkubali kubadili Katiba ya CHAMA ili awe mwenyekiti tena.

Wewe na mwenyekiti wako ndiyo mnatafuta huruma ya Wantanzia. Ila moto mnao, CHADEMA itawaendesha puta mpaka muisome namba. Mwigulu anazurura Kutafuta huruma ya watanzania baada ya M4C -OPD badala ya kukaa wizarani kushughuliwa swala ya serikali ya Tanzania kufirisika unnadhani anapenda? Hapa thatha, Wizarani hapakaliki. CDM hatari imeshawasha moto wa Petrol na mmeanza kutafuta njia ya kutokea. Shughuli mnayo mtajibaraguza sana.
 
Kila mmwamba ngoma kamba huvutia kwake. CHADEMA watavutia kwao na CCM watavutia kwao pia. Yule atakayeshindwa ndo kashindwa sasa ugomvi wa nini kwenye mchezo. Usitegemee mvuta kamba wa CCM avutie upande wa CHADEMA, CHADEMA hali kadhalika. Upande utakaoshindwa ujipange upya. Hakuna dhambi Raisi Kikwete kuvutia upande wa CCM na Mbowe naye akivutia CHADEMA ndiyo halali yake. Kikwete katoa hoja Mbowe naye anatoa hoja yake. Sasa Mbowe alitaka Kikwete atoe hoja Mbowe? Haiwezekani.
Hoja ya kusema tunataka Katiba ni ya nchi nzima sio ya chama haina mshiko kwa sababu nchi sio ardhi ni watu na watu ndiyo wenye maslahi iwe mmoja mmoja au kwenye vikundi vyao kama vile CCM, CHADEMA CUF NCCR Mageuzi vikundi vya dini NGOs nk. Kupata katiba itakayokuwa haiangalii maslahi ya vyama vya siasa haitawezekana. Hata wanaosema tuwe na muungano wa serikali tatu wanayaona maslahi ndani serikali tatu
"kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo".kumbe mbowe hakusema watapigana ngumi bungeni?basi ile kauli ya 'nimeambiwa' bado inaendelea.
 
Mwambieni MBOWE aache kulalamika majukwaani, wafunde Wabunge wake waende DODOMA wakiwa na hoja badala ya ujinga ujinga tena.

Na nyie muache kumtoa tundu lisu nje ya bunge kisa kachangia mara nyingi kama alivyofanya NDUGAI.
 
Binfsi huwa nashangaa sana, unaposema katiba ni ya wananchi hivyo mawazo ya wananchi yaheshimiwe je kupinga mwazo ya wananchi wanaotaka serikali mbili kunakofanywa na Chadema je huko si kudharau mawazo ya wananchi? Au kwa wao Chadema wananchi ni wale tu wanaotaka serikali tatu?
Mimi huwa nadhani huwa wanamaanisha 'wananchi wengi' badala ya kusema tu wananchi ili kuepuka maswali ya namba na jinsi zilivyopatika katika context ya wananchi.

Tatizo la wanasiasa wetu wengi pia huwa siyo makini sana katika maana ya kila neno wanalolisema na pale inapotokea watu makini wakagundua mapungufu katika kauli zao, utawasikia wanasiasa wetu wakisema 'wamenukuliwa' kimakosa.

Wanasiasa wengine wanapenda sana kujificha kwenye kauli tata kama hizi as we know, Politics, after all, is the art of persuasion and manipulation!.
 
Lakini kweli kuna mara nyingi waandishi wetu uwanukuu vibaya (au kwa makusudi)...
 
Mbowe angeenda shule asingeongea huu ujinga hapo juu! Shule inasaidia sana, hata uwe na fedha vipi kama hujaenda shule huwezi kuwa na hoja iliyosimama ipasavyo!
bora shule ya mbowe kuliko yako na baba yako ya ngumbalu
 
Back
Top Bottom