Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,202
- 138,575
Leo nimetafakari juu ya kukosekana kwa Mbowe wala kauli yake kwenye hali ngumu inayopitia Tanzania
Nikafikiria hivi kweli hawa watanzania ni watu wa kuwapigania mpaka tone la mwisho? Nikawahesabu watu kadhaa waliorisk maisha yao wakiwatetea watanzania. Nikamkumbuka Tundu Lissu na Mbowe na wengine wengi. Nikakuta nyuna yao hakuna kundi kubwa la watanzania walio nyuma yao. Nikakuta ni kakundi kadogo tu ambako ni rahisi kupuuzwa.
Nikakuta nchi haina wazee wa kuwa nyuma ya wanasiasa wazalendo, nikakuta wazee wengi wanaangalia matumbo yao, wachache wanaokerwa na hii hali ni waoga wanasema kwa mafumbo. Nikakuta viongozi wengi wa dini ni wanafiki na wanaangalia mstakabali wa taasisi zao, angalau Kanisa Katoliki linasema.
Nikaona kuna uwezekano mkubwa Mbowe aliona hapa napoteza muda hii nchi imejaa wajinga. Ameshapoteza vingi sana lakini akikutwa na majanga akigeuka nyuma anakuta hakuna mtu.
Akaona avute akae pembeni.