Wakuu,
Leo nilialikwa kwenye harambee ya KKKT dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Longuo - Moshi ambapo walikua na harambee ya ujenzi wa kanisa, na mgeni rasmi alitegemewa kuwa Mbunge wa Hai, Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Haikaeli Mbowe.
Lakini cha kushangaza, Mh. Mbowe hakuweza kuhudhuria harambee hiyo pamoja na kukubali kuwa mgeni rasmi tangu awali, na taarifa nilizopata ni kwamba Mh. Mbowe alitoa taarifa ya kutokuhudhuria siku moja kabla ya harambee bila hata ya kutuma muwakilishi.
Kwa kweli katika hili Mwenyekiti wangu ameni let down sana as I always believe that he is a man of his words!!
Akili yako na ya maiti hazitofautiani!
We si umesema kwamba alitoa uthuru! Sasa UMBEA WA NINI? Unaonekana usipomsema hulali!
Nimetafuta tusi la kukupa nikakosa.
Heshimu maamuzi yake maana pia ni mtu lakini harambee itakuwa ime endelea
Alishatoa udhuru, walikuwa wanasubiria kivuli chake au? Kama waliona hakuna mbadala walipaswa wao kumwomba atume mwakilishi anayeona angefaa kumwakilisha.
Mi si mwanasiasa lakini sijaona kosa la Mbowe hapa.
hapakuwa na haja ya kukubali kama alijua haji halafu kama alipata udhuru ghafla si angetuma muwakilishi? Kwa nini aliwaacha watu waliokua wanamtarajia njia panda?
Babu Asprini heshima kwako.
Bila shaka unajua ugumu wa kupata mgeni rasmi katika shughuli kama harambee. Hivi mtu aliyekubali awali halafu anakujulisha Jumamosi kwamba hataweza kuhudhuria hiyo harambe ya Jumapili unamchukuliaje?
Unaweza kweli ukampata mgeni rasmi mwingine ndani ya muda huo. Try to be objective babu!
Labda upeleleze ujue ni udhuru upi huo ambao ulimpata mpaka akashindwa kushiriki hiyo harambee, pia alipotoa udhuru alizungumza nini na wahusika wa harambee, pia kuhusu kuleta mwakilishi nadhani wenye harambee walimhitaji yeye kama yeye wakiamini kwamba anaweza akafanikisha hivyo akileta mwakilishi huenda akawaletea mtu ambae wanadhani atashindwa kufanikisha harambee (kwanini nasema hivi, Mbowe ameteuliwa na wana harambee wenyewe iweje nae achague harambee hasa ukizingatia hiyo haikuwa ni kazi ya kufungua au kufunga mkutano)
Ni mawazo yangu tu hayo
Nilizungumza na mmoja wa wanakamati akaniambia hadi jana ndio walipata taarifa kwamba huyu mkuu hatakuja na sababu haikutajwa ingawa mchungaji alisema labda ni kutokana na kubanwa na majukumu.
Kuhusu kutuma mwakilishi ingekua busara zaidi, mfano alialikwa baba askofu Martine Shao kushiriki kwenye harambee lakini kutokana na kubanwa na majukumu alimtuma askofu mmojawapo wa dayosisi amwakilishe.
Ila umewaza vema si kama bangii!
Jaribu kuufikirisha ubongo wako mkuu, aliyealikwa ni binadamu kama yeyote anaweza akaugua ghafla, kuuguliwa au kupata dharura yoyote na wakati wowote hata zikiwa zimebaki saa mbili tu; sasa ulitaka akamtafutie wapi huyo unayemwita mwakilishi? Kumbuka hata huyo mwakilishi atasema angehitaji muda wa kujiandaa kwa shughuli kama hiyo! Kwani harambee ile ilikuwa ya siku moja tu? siku moja? Kama siyo basi mwalikeni tena atahudhuria kwenye harambee ijayo.
We ndo ukanye ukalale, alafu utawazee! Maana huko kimimanjaro kuna baridi! BASI DOGO ACHA UNAFKI MWACHE JEMBE LA CDM LIINJOY!