Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,521
- 6,517
Napongeza sana Mbowe kufungua hii kesi, hata kama imefutwa lakini maelekezo ya wapi pa kuanzia yamejulikana. Kuishi bila kukosea ina maana hamna kitu kipya unafanya maishani mwako
Vyovyote vile utakavyopenda kutumia logic yako lakini ukweli ni kuwa Mbowe amegonga mwamba kwa sababu kesi yake ya msingi imekataliwa.Naona umeandika kimipashopasho na mbwembwe
Sasa hapo kilicholeta tatizo ni logic ya kesi au ni Jurisdiction ya mahakama?
Zisimguse vp na zimetungiwa watu! Kila mtu ana siku yake ya kufa na ukifa leo hufi tena.Hajielewi mpaka pale zitakapomgusa.
Haki mbinguni,sheria duniani.Kwa hiyo kutimiza majengo kwa Serikali ni kunyanyasa RAIA na si kutenda haki na kutotumia madaraka vibaya??
Kama ni hivyo basi ndani ya Serikali kuna matatizo makubwa sana.
Haki mbinguni,sheria duniani.
Freeman Mbowe amegonga mwamba katika kesi ya Msingi ya Kikatiba ambapo alikuwa anapinga kitendo cha polisi kumtaka afike kituoni kwa madai kuwa ni utekelezaji wa amri ya Mkuu wa Mkoa.
Mbowe katika kesi hiyo alidai kuwa sheria inayompa Mkuu wa Mkoa mamlaka ya kutoa amri ya kumkamata na kumweka ndani mtu, yako kinyume cha katiba kwa madai kuwa ilitungwa katika mazingira ambayo hapakuwa na vituo vya polisi vya kutosha.
Kutokana na madai hayo, Mbowe alidai kuwa kwa mazingira ya sasa sheria hiyo imeshapitwa na wakati na anaiomba mahakama itamke kuwa ni kinyume cha katiba.
Kadhalika alidai kuwa hata kama Mkuu wa Mkoa alikuwa anatekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa sheria hiyo, hakutimiza matakwa ya kisheria, ambayo ni pamoja na kutoa taarifa kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi na kwamba mahakama kama itaona alikuwa sawa kutoa amri hiyo, imwamuru afuate matakwa ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kulinda haki za binadamu katika kutekeleza madaraka yake hayo.
Kutupwa kwa kesi hiyo kumetokana na mahakama hiyo kukubali pingamizi la walalamikiwa kwamba mahakama hiyo haina mamkala ya kuyasikiliza.
Walalamikiwa katika maombi hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kwa sasa Paul Makonda), Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (Simon Siro) na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO) (Camillius Wambura).
Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Sekiet Kihiyo, akisaidiana na Pellagia Khaday na Dk. Lugano Mwandambo
Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya jopo, Jaji Khaday alisema upande wa walalamikiwa uliwasilisha pingamizi la awali kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu mlalamikaji alitakiwa kuwasilisha katika mamlaka husika.
Pia sheria za haki za msingi kifungu cha 8 kidogo cha (2) sura ya 3, inakataza mahakama hiyo kusikiliza maombi kama hayo na kwamba kuna mamlaka zinazoshughulikia kabla ya kufikishwa mahakamani kwa sababu si kesi ya kikatiba.
Aidha, mahakama imetoa uamuzi huo baada ya mlalamikaji kushindwa kufika mahakamani kuwasilisha majibu ya pingamizi la awali la walalamikiwa hata baada ya kupewa muda wa kufanya hivyo.
Hii kesi ilifunguliwa na mbwembwe nyingi za kisiasa huku wanasheria kama Jenerali Ulimwengu wakijitokeza na kudai waunganishwe kwenye jopo la mawakili wa kumtetea Mbowe.
Kwa wale tunafahamu vizuri mbwembwe za wanasiasa wa Tanzania tulisema mapema kuwa Mbowe hawawezi kushinda hii kesi kwa sababu sheria ziko wazi kuhusu madaraka ya Mkuu wa Mkoa na utaratibu wa kufungua kesi za kikatiba.
Siku ambayo Mbowe aliyofungua kesi niliweka thread hii,
GONGA LINK>>Mbowe ameshindwa kesi kabla hata haijaanza.
Jopo la wanasheria wa Mbowe wakiongozwa na Tundu Lissu lilifungua kesi kwa mbwembwe nyingi za kisiasa.
Kwa sasa nimesikia eti TLS wanataka kufungua kesi mahakamani kuhusu vyeti vya Paul Makonda na ‘’uvamizi wa studio za Clouds Media’’.
Hizi nazo ni mbwembwe tu za kisiasa kwa sababu kesi haiwezi kufunguliwa na kama itafunguliwa, watashindwa mapema sana.
Sheria hazina siasa pamoja na kwamba siasa wakati mwingine hazina sheria.
Kwa wasifahamu vizuri kesi hii angalia hii video:

Kwa hiyo wewe unadhani una amani ! Pole zaidi,hapa figisu nifigisue tu.Aliyekudanganya mtafute akusaidie.Bila Haki hakuna Amani.Pole.
Huko Mahakamani ndo uchochoro wa miungu watu (viongozi) wa Chadema wanakopigia hela za ruzuku ya chama,hakuna auditing yoyote inafanyika huko,hao miungu watu wanatengeneza kesi za ajabu wanaenda mahakamani huku manyumbu yao yakishangilia hlf mwisho wa siku hakuna nyumbu anahoji hizo kesi zinaisha vipi maana nyumbu hana kumbukumbu...!!!Hajui kama kisheria bado uwezekano wa Mbowe kuendelea na kesi upo na akashinda vile vile.
Kumbe Lissu,Ulimwengu,na mawakili wote waliomuwakilisha Mwenyekiti wa kudumu wa Chadema(Mbowe) walikuwa MABASHITE tu wanashindwa kujua kesi inatakiwa kufunguliwa vipi?hukumuelewa, aliposema ni tatizo dogo alimaanisha kuwa mh Mbowe hakushindwa kesi kwa sababu kesi haikuwepo.maombi hayakusikilizwa kwa sababu hayakufunguliwa katika mahakama husika.hizo ni technicalities za kisheria kwa hiyo haimzuii mh Mbowe kuifungua tena ktk mahakama yenye mamlaka ya kuisikiliza.