MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amedaiwa kuficha ubadhirifu wa fedha za miradi mbalimbali ndani ya halmashauri ya Karatu wakati akijaribu kutatua mgogoro uliopo ndani ya chama hicho mjini humo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kutoka Wilaya ya Karatu, Daniel Awakii alisema hayo jana na kuongeza kuwa kuficha ubadhirifu sio uongozi bora. "Mbowe aeleze ukweli juu ya mgogoro wa uongozi karatu na asimung'unye maneno kwani huo sio utawala bora," alisema.
Awakii alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mkutano wake wa hadhara katika Kijiji cha Barazani, Kata ya Mang'ola wilayani humo. Alihoji kwa nini Mbowe hakutoa msimamo wa chama, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi hao kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili na badala yake amefanya kazi ya kuwapatanisha jukwaani tu.
Alisema viongozi hao waliopatanishwa wakiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu mjini, Jubilate Mnyenya ambaye pia ni Mwenyekiti Bodi ya mradi wa maji vijijini wilayani humo (KAVIWASU), walikuwa wakituhumiana kwa ufisadi.
Alifafanua kuwa viongozi hao wawili wamekuwa wakituhumiana kuwa mradi huo wa maji umekuwa hauendi vizuri kama inavyotarajiwa kutokana na Mnyenya kushindwa kuisimamia vizuri bodi yake na kusababisha kukosekana kwa maji katika mabomba ya wananchi huku yeye akipata maji katika miradi na mashamba yake.
Lazaro pia anadaiwa amekuwa akimtuhumu Mnyenya kwa kutumia fedha zinazopatikana kutokana na ada zinazokusanywa kutoka kwa watumiaji wa maji huku mradi huo ukishindwa kujiendesha na kusababisha huduma kukosekana kwa wateja ambao ni wananchi.
Mnyenya naye inadaiwa amekuwa akimtuhumu Lazaro kwamba ameuza kwa matajiri maeneo ya wazi likiwemo lililokuwa likimilikiwa na magereza na kukabidhiwa kwa vijana ili waendeshe shughuli zao za ufundi gereji na kusababisha vurugu na maandamano ya vijana hao.
Pia alidai Lazaro amekuwa akituhumiwa kutoa fedha za maendeleo kwa madiwani katika kata mbalimbali kwa upendeleo hususani kwa wale wanaomuunga mkono, hali iliyosababisha baadhi ya kata kukosa fedha hizo na kudorora kimaendeleo.
"Hivi jamani wananchi wenzangu mnamuelewaje Mbowe? Anakuja hapa kuwapatanisha na kusema ni viongozi muhimu kwa chama chake na kwamba tuweke maslahi ya chama mbele badala maslahi yetu huku mali na fedha zetu zikiliwa huu si ndiyo ufisadi wenyewe," alihoji Awakii. Gazeti hili lilipomtafuta Mbowe kwa njia ya simu jana kuzungumzia kauli ya Awakii, simu yake haikupatikana.
Chanzo: HabariLeo la leo.