Mbosso, Whozu na Marioo, hawa chalii watafika mbali sana

princemikazo

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
2,197
2,054
Nikiwa nime chili knich knach maghetoni baada ya kumaliza mbanga za kuuza chai nyuma ya mic, nikawa naorodhesha baadhi ya Machalii waliofanya poa laana kunako mwaka 2018 fiade ya Bongofleva,

List angu ilipata majina shazi lakini mojawapo ya majina niliweza kuwapata Wasanii ambao kama ni wachanga kunako hii game, Washkaji hao ni Mbosso, Marioo na Whozu.

Kiukweli hawa jombaa nawaona mbali kinyama kimuziki kutokana na jitihada wanazozifanya ku-push muziki wao.

Whozu, Huyu Jamaa toka Moshi Mo Town ni mbunifu sana kwenye nyimbo na video zake, ikumbukwe uyu chalii alianzia kufanya comedy ambae still now bado anafanya iyo comedy na kuamua kuiingiza iyo comedy kwenye Muziki wake,usipocheka kwenye audio bas utacheka kwenye video, Very creative ata kwenye show zake, Mfano figidi fiesitraa ya chuga alipanda na Begi limejaa mishikaki pamoja na dancers wake, huu ni ubunifu pia.

Mbosso, Huyu Jamaa toka pale Dabiliusibii Offcourse anafanya poa sana, video zake zinapata views za ela ote, kapata collaboration za nje ingawa ni chache ila time will tell, Pia alikua kwenye nominations za tuzo za MVP Sound City2018 category ya new artist, Style yake ya uimbaji akitia ladha ya kihindi imekua ikivutia sana na kumfanya kuwa unique.

Marioo,They call him Toto bad,Chalii ambae yuko chini ya Hanscana brand na Abbah akiwa na wenzake kina Maua sama na Hanstone, Ndo kwanza akiwa na miaka21 lakini kafanya makubwa sana kaandika hit songs kama zote kama vile Banana ya Janjaro ngareroo republic, Wasikudanganye ya Nandy, Pambe ya Christian Bella, Mchakamchaka ya Shilole, Bado ya Mwasiti na Billnass na zinginezo hali iliyompelekea Msanii wa gospel toka 25flow Will paul msafi kumshauri apunguze kuandikia watu, Ngoma zake zimefanya poa pia since day uno, Dar kugumu, Subira, Yale, Ifunanya, Nyatunyatu, Manyaku pamoja na Wauwe zote ni full laana dingii, chalii anapambana ya ela ote aisee!

Kama hujaielewa list yangu dropisha nawewe yakwako apa fas ya duas alafu inakua ni echu kikosi.

Wasalaaam.
 
Whozu sio mwanamuziki wala hatakaa awe mwanamuziki na bahatisha ya uendi mbinguni haiwezi rudi tena...Mbosso ni mkali, Marioo nae mkali japo anaimba kama mbosso.
BDingii unafatilia muziki kweli??Yaan Whozu kabahatisha Huendi mbugani pekee??angalia idadi ya nyimbo zake tangia kaanza,alaf uangalie hit song ni ngapi pia,,Follow un follow,Gonga,Tunavesha,zote ni rekwe
 
Mbna Whozu kama ameishia hapo....mwambieni achukue chake mapema aanzishe mradi wa kujishikiza asije akawa mdangaji kama Ney wa mitego, kwanza hana proper management, pili style yake watu wameizoea sasa, tatu ameanza kuwa karbu na wadangaji akina tunda..ngoja tuone..ntarud mwez wa sita kuverify
 
Whozu yuko chini ya S2 Kizzy zombie,Unaposema hana management sielewi
 
BDingii unafatilia muziki kweli??Yaan Whozu kabahatisha Huendi mbugani pekee??angalia idadi ya nyimbo zake tangia kaanza,alaf uangalie hit song ni ngapi pia,,Follow un follow,Gonga,Tunavesha,zote ni rekwe
huyo msanii wa kutengeneza hana talent yoyote na alipofika ndio mafanikio yake atafute kazi nyingine ya kufanya.
 
muziki anaoimba whozu ni mzuri... lakini unachosha haraka mnooo..marioo na mbosso wako vizuri ila naona beat za laizer anazomtengenezea mbosso zinafanana hivi
 
Mbna Whozu kama ameishia hapo....mwambieni achukue chake mapema aanzishe mradi wa kujishikiza asije akawa mdangaji kama Ney wa mitego, kwanza hana proper management, pili style yake watu wameizoea sasa, tatu ameanza kuwa karbu na wadangaji akina tunda..ngoja tuone..ntarud mwez wa sita kuverify
Ya mwaka gani kaka hiyo mwezi wa sita yako
 
Mbna Whozu kama ameishia hapo....mwambieni achukue chake mapema aanzishe mradi wa kujishikiza asije akawa mdangaji kama Ney wa mitego, kwanza hana proper management, pili style yake watu wameizoea sasa, tatu ameanza kuwa karbu na wadangaji akina tunda..ngoja tuone..ntarud mwez wa sita kuverify
Hiki kijamaa kikipewa buku saba za dabliyu sibi anawehuka sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom