pambe samanini
JF-Expert Member
- Oct 27, 2015
- 368
- 169
Napenda kulipongeza jeshi la polisi kwa kazi zake za kupambana na kuzuia uharifu dhidi ya raia wake, lakini mauaji ya raia wasiokuwa na hatia yanayofanywa na majambazi bado yanakithiri hapa nchini mfano, tanga, mwanza, mara, pamoja na mauaji dhidi ya ndugu zetu wenye ualbino.
Matukio yote haya yanafanyika kwa Siri kubwa mno kiasi cha jeshi la polisi kushindwa kuhimili na kudhibiti mauaji pamoja na uharifu wa namna hiyo, kwa uelewa wangu mdogo kuna intelijensia ya polisi ambacho ni kitengo nyeti sana kwa jeshi letu; je kweli kitengo hiki lipo hai?
Na kama kipo hai kinafanya nini hadi madhara makubwa yanatokea katika jamii yetu? Watu wanauawa, watu wanapolwa Mali na majambazi na uharifu wa kila aina unatokea halafu wao baada ya madhara ndiyo wanakuwa mstari wa mbele kutoa taarifa na matamko makali bila kutuuambia intelijensia yao ilikuwa wapi kutoa taarifa kabla ya maafa?
Jeshi letu la polisi cha kushangaza limejikita kupambana na wanasiasa wanaoonekana na hapo ndipo utasikia intelijensia zao zinavyofanya kazi lakini kwa uharifu nadra intelijensia zao kupata taarifa za uharifu. Hizi ni mbio ambazo hazitufai kabisa; Mtukufu rais wetu mpendwa hawa polisi nao inabidi uwatumbue ili intelijensia zao ziwe zinafanya kazi zake kwa ufanisi kuhusiana na uharifu na siyo wanasiasa hawa ambao wanaweza lindwa kwa hali na mali.
JPM polisi wetu wachape kazi kwa kulinda raia na mali zao vingine JWTZ washike usukani kukomesha uharifu nchini kwetu.