Mbona wakenya mko kimya sana kutuletea updates za michakato ya uchaguzi kwenye vyama?

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Wanabodi salaam.

Toka wiki iliyopita michakato ya kuwapata wagombea wa nafasi mbali mbali kwenye ngazi ya vyama ilianza na zineshika kazi sana japo chama cha Jubilee ndicho kinachovuma kila ukifungulia TV kikifuatiwa na ODM kwa mbali.

Cha kushangaza wenzetu wa Kenya ambao ni members wa humu wako kimya kutuletea updates za kile kinachoendelea kwenye michakato hiyo.

Na kikubwa zaidi jana nilisikia kwenye K24 kuwa leo hii tar 27/04/2017 muungano wa NASA watatangaza mgombea wao na shughuli nzima itafanyikia Nyayo National Stadium. Sijajua kama imeshafanyika maana niko kwenye mihangaiko.

Watanzania ndipo tunapowazidia wenzetu wa Kenya kwenye mambo kama haya. Yaani ingekuwa huku kwetu majukwaa ya Sasa na Uchaguzi yangechafuka kwa updates toka kila pande za nchi.

Sasa nyie wenzetu Wakenya mbona mnakuwa wabinafsi kiasi hiki?? Sio vizuri kabisa
 
Wao wanajari sn nchi yao hata kama kuna makosa ya dhahl yanadanyika huwez sikia wakilopoka kama cc Tz. Pia, wako bze sn na shughuli za kiuchum from individual level to the national level tofaut na cc tunakalia kujadl pumba minutely. Hongeren sn Wakenya.
 
Siasa za mwaka huu ni high voltage, hazitabiriki na hakuna mwenye uhakika wa nani ataibuka mshindi wapi au wapi, yaani marafiki wa karibu wa rais Uhuru wamepigwa chini, pia hata wale wa Raila akiwemo ndugu na binamu. Wakenya mwaka huu nawapa hongera ndugu zangu, maana sikutegemea mtawapiga chini watu waliokua wanajificha kwenye migongo ya vyama au viongozi wakuu, yaani kila mtu kivyake, inabidi kuwaelewesha wapiga kura kwanini wakupe kura.

Kule kijijini ukienda na jina la rais unaambiwa huyo hatokusaidia, maana yeye rais tutampa kura lakni wewe tunakupiga chini. Japo sijaelewa mantiki ipi ilitumika kumpiga chini mbunge wa kijijini kwetu Mukrweini bwana Kabando wa Kabando, mbona niliona jamaa kama alikua anafanya kazi, hivi bibi na wazee wa kwetu mumeingiwa na kichaa? Huyo mngempa kura arudi.

Yote tisa, tuwachague viongozi kwa vigezo vinavyofaa, leo tupo kwenye hatua za mwisho za kujua nani rais wa Nairabi kati ya Sonko na Peter Kenneth. Japo Sonko anaonekana kufaulu, jamaa ni fighter sana, tena vijana wanampenda sana.

Halafu ya NASA pia tunasubiri leo, ila wengi tulishapata taarifa za ndani walivyokusudia kugawana madaraka, mgombea urais wanategemea atakua Raila Odinga, halafu mgombea mwenza Kalonzo Musyoka, wengine wameahidiwa kubnuniwa vyeo vya kuwabembeleza. Hivyo NASA kama ilivyo Jubilee hatuna chochote kipya maana wamerudia utaratibu wa mwaka wa 2013.

Anyway, wote Wakenya, atakayeshinda basi tutampa ushirikiano atuongoze hadi nch ya ahadi.
 
MK254,
Kweli kabisa kura za mchujo ni ''high voltage''.

Shughuli za kupokea matokeo ya kura za mchujo katika Jubilee kutoka vituo mbalimbali kaunti ya Nairobi zilitatizwa kiasi alasiri hii, baada ya mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Nairobi Rachel Shebesh ''kuvurumiza'' na wafuasi wake kulalamikia hatua ya ''kucheketuliwa'' kwa hesabu yake. Kulingana na Shebesh, amemlaumu sana kiongozi wa kituo hicho kwa makosa hayo.

Baada ya vurumai hizi, mgombea Rachel Shebesh alithibitishwa kuwa ameshinda kura za mchujo nyingi sana kupita wagombea wote wanawake ndani ya chama cha Jubilee na hivyo atagombea uwakilishi wa wanawake kaunti ya Nairobi kupitia tiketi ya Jubilee.

Kenya NTV
 
haya matokeo si yalifutwa?
 
Back
Top Bottom