DOKEZO Mbona ujenzi wa SGR hapa jiji la Mwanza na kwenda Isaka umekwama?

DOKEZO Mbona ujenzi wa SGR hapa jiji la Mwanza na kwenda Isaka umekwama?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,190
Tulishuhudia ujenzi wa SGR hapa Jijini Mwanza na kuelekea Isaka ukienda kwa kasi. Ghafla ujenzi umesimama na hatujui ni kwa sababu gani.

Tunaiomba Mamlaka itueleze nini kimekwamisha ujenzi huu huku tukiaminishwa kuwa Mama amemwaga fedha nyingi na anaupiga mwingi.
Kwa nini ukwame?
 
Nyie msubiri kwanza tumalize ujenzu wa barabara na stadium huku visiwani mchamba wima
 
Pesa za SGR zimepelekwa znz kujenga flyover sasahivi kila njiapanda pale unguja Inapigwa flyovers
 
Pesa za SGR zimepelekwa znz kujenga flyover sasahivi kila njiapanda pale unguja Inapigwa flyovers
zanzibar wana uchumi wao n mamlaka yao ya mapato, miundo mbinu sio suala la muungano, ila tu pale pesa za kujenga miumdombinu zikitoka nje lazima znz wapate gawiwo (kwasababu mahusiano ya kimataifa ikiwemo misaada ni suala la muungano)

usiwe na shaka hakuna pesa ya bara inayojenga flyover wala stadium hulo znz, kwa mwakanwatalii karibu milioni wanaingia znz kuliko mji wowote tz hivyo wana pesa za kutosha
 
Back
Top Bottom