Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!.Hii ni Bidhaa Muhimu au ni Starehe Tuu!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,770
121,817
Wanabodi,

Hili ni swali, Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!. Hii ni Bidhaa Muhimu kihivi au ni bidhaa ya starehe Tuu?!. Inawezekana hizi kelele zote ni kujiendekeza tuu?!.

Ninafuatilia jinsi nchi inahaha kuhusu hii bidhaa inayoitwa sukari!, watu wanahaha kuanzia rais wa nchi amekuwa mkali hadi kutishia watu maisha, kisa sukari!, TRA sasa ni kusaka tuu sukari!, Jeshi la Polisi sasa ni sukari tuu!, Takukuru nao sasa ni sukari!, vijana wa Rashid Othman ndio usiseme!, hatuchelewi kusikia hadi vijana wa Mwamunyange nao watajitosa katika hii maana sasa naona imegeuka vita! vita ya sukari, maana inatishia amani, utulivu, usalama wa nchi hadi kuhatarisha ulinzi wa taifa hivyo tutumie jeshi letu na silaha kali kabisa tumwangamize adui huyu!, hivi hii sukari ni nini haswa na ina umuhimu gani kustahilimili hizi kelele zote?!

Swali ni kuwa kwani sukari ndio nini?!, ukiondoa sukari inayotumika kuzalishia bidhaa viwandani, yaani sukari ya viwandani, hii sukari ya majumbani, tunaoitumia kuiweka kwenye chai, sio bidhaa adimu lolote, sio bidhaa adimu chochote, kwa sababu sukari sio bidhaa muhimu kivile, hivyo hizi kelele zote za kila kona sukari, sukari, Watanzani huku ni kujiendekeza tuu!.

Mimi nilikuwa Primari kipindi kile cha "miezi 18 ya kukaza mikanda baada ya vita ya Kagera" bidhaa muhimu ziliuzwa kwa ration ikiwemo sukari, tulipanga foleni hadi kupanga mawe kutushikia nafasi kwenye maduka ya kaya ili tuu kuuziwa kilo mbilimbili mbili kwa wiki kwa kila familia!.

Labda hii kelele yote ni kufuatia tuu utamu wa sukari, lakini sio umuhimu wa sukari kwa sababu kwenye miili yetu, sukari sio muhimu kivile!, virutubisho vilivyo kwenye matunda, yaani sucrose, ni lishe bora mara mia kuliko sukari!. Asali ina virutubisho mara elfu kuliko sukari!, sasa hizi kelele zote za sukari za nini?!. Na kwa msio jua, vyakula vyote vyenye wanga, vikimengevywa na vimengenyo vya pelipeptaid, peptaid na pepton, vinazalisha nguvu mara 100 ya inayozalishwa na sukari!. Ukinywa maziwa fresh ya ngombe, vimengenyo vya renin na pepsin vinazalisha lishe bora mara 100 kuliko hiyo sukari!, why kelele zote hizi za sukari?!.

Baada ya ile miezi 18 ya shida, nilijiunga sekondari ya Tambaza nikila sukari, baada ya hapo nikajiunga Ilboru kule Arusha, huko ndiko nilikojifunza kuwa sukari japo ni bidhaa adimu, lakini sio bidhaa muhimi kivile zaidi ya kujiendekeza tuu!. Shule ya Ilboru chini Mwalimu Mkuu aliyeitwa Bino, aliamua shule hainunui sukari na Ilboru ikawa haitumii sukari!. Kule sukari iliitwa "dawa ya sumu" hivyo ile tuu kujulikana umepangwa Ilboru ili ukasome kwa raha, miongoni mwa bidhaa muhimu za kufungashiwa, ilikuwa ni sukari!, kwa vile mimi nilitokea shule za Dar, wengi niliotoka nao Dar kujiunga Ilboru, walikuwa ni watoto mujini, baadhi yao laini laini na kweli walifungashiwa sukari!, mimi ni miongoni mwa wale wagumu ambao tulitinga Ilboru bila kufungashiwa sukari, ila nilikuwa na fungu, ukitokea umuhimu nitanunua!. Na hapo Ilboru nilipangwa bweni la Oldonyo, wale wa Dar wote niliopangwa nao, walihama kuhamia mabweni mengine yenye heri!, mimi nilikomaa na Oldonyo!.

Asubuhi ilikuwa ni uji wa chumvi!, ulioitwa "sumu" na sukari ndio "dawa ya sumu" saa 4 ni chai ya rangi ya majani ya chai tuu kila mtu anaweka sukari kivyake!, mwanzo nilipoanza kunywa uji wa chumvi nilishindwa, nikajilazimisha, kisha nikazoea!, baada tuu ya kuzoea, ndipo nikatambua kumbe kupenda sukari ni kujiendekeza tuu kupenda utamu!, sukari sii lolote sii chochote!, uji wa chumvi ukawa ni mtamu kuliko uji wa sukari!, nikavikia kiwango hata sukari ikiwepo, sihitaji tena hiyo sukari!.

Baada ya kufaulu zoezi la uji wa chumvi likafuatia zoezi la chai ya rangi bila sukari, hapo napo ilikuwa kazi lakini niliweza, na tena ukiweza kunywa chai ya rangi bila sukari, ndio unapata ladha halisi ya chai au kahawa, ile aroma original yenyewe, na ukiishawezakupata aroma ya chai au kahawa, hutakaa unywe tena chai ya sukari!. Hivyo matumizi ya sukari ni kijuendekeza tuu!, wenzetu Wachina, sukari hawali, chumvi hawali na chinese food hawatumii mafuta!.

Lengo la hawa waficha sukari ni kucreate demand ila wapandishe bei na kutulangua kutokana na uhaba wa sukari. Natoa wito kwa Watanzania wenzangu katika umoja wetu!, tuache kujiendekeza kwa utamu wa sukari!. Tuishii kama maisha ya Ilboru ile, maisha ya bila sukari!, tuisusie hiyo sukari ili hao walioificha iwadodee kwa sababu sukari sio bidhaa muhimu kivile!.

Namalizia na hili swali,
Hili ni swali, Mbona Tunapiga Sana Kelele Kuhusu Sukari?!. Hii ni Bidhaa Muhimu kihivi au ni bidhaa ya starehe Tuu!. Inawezekana hizi kelele zote ni kujiendekeza tuu?!.

Tuache kujiendekeza kwa maisha laini laini, tuishi kiugumu ugumu bila bidhaa ya sukari, na akiwezekana hata tumshauri Magufuli apige marufuku matumizi ya sukari ya majumbani!, au unaonaje?!.

Mgumu Pasco.
 
Hata Mimi pia ninawaza hivyo hivyo. Wakati mwingine ni sisi wananchi ndio tunasababisha hii mitafaruku. Kwani tukigoma kununua hiyo sukari hao wafanyabiashara unafikiri wataendelea kuificha? Haya mambo ni kujiendekeza tu na wala hayana umuhimu wowote ktk life. Wenzetu nchi walizoendelea wanajitahidi kupunguza/kuacha kabisa matumizi ya sukari but sisi huku ndo utafikiri tumekosa panadol. Dah
 
Vijana wa Othman Rashid wangekua makini wangemshauri mkubwa kuhusu katazo la Ku import sukari bahati mbaya wako bize Na mzee wa Bills Na EL.

ILA Pasco mi pia ni mgumu mwenzako tangia Bunge primary ila hapo Ilboru nilikua bweni Safi kuliko zote by then MAWENZI.
 
Pasco mimi hua napenda aina ya uandishi wako, utani,mzaha na kejeli kwa mbali ila unajenga hoja nzuri. Unaandika gazeti gani kiongozi?

Sio siri sukari sio bidhaa muhimu. Mimi naweza kutumia sukari hii ya nyumbani mara moja kwa wiki au nisitumie kabisa. Naweza kunununua kilo moja ikamaliza miezi 4 mwisho huimwaga.

Sukari mimi binafsi iwepo au isiwepo sina cha kupoteza.
 
Ukiondoa kwa matumizi ya hospitalini, Sukari ni ANASA.

Nilishajiondoa kutoka katika utumwa huo tangu nikiwa chuo ...

Labda nikioa nitajua tena umuhimu wa sukari sababu ya watoto. Hata hivyo, sitataka kuwazoesha sukari.

Sukari niipatayo kutoka kwenye wanga, matunda na asali is safe & more than enough for my body.
 
Sukari ni ANASA.

Nilishajiondoa kutoka katika utumwa huo tangu nikiwa chuo ...

Labda nikioa nitajua tena umuhimu wa sukari sababu ya watoto. Hata hivyo, sitataka kuwazoesha sukari.

Sukari niipatayo kutoka kwenye wanga, matunda na asali is safe & more than enough for my body.
Kukusaidia kidogo wewe na mwandishi, naomba ujue kwamba sukari na chumvi ni bidhaa muhimu sana katika uchumi wa nchi.

Hizo zinaitwa necessities maana yake ni bidhaa muhimu kwa binadamu.
 
ndivyo tulivyo wabongo,watu wanalalamika bei ya sukari wamesahau ya kwamba elimu ni bure sukari ndo na hela hii inamaanisha ya kwamba sukari ni tamu kuliko elimu..
Elimu ni bure ingawa harambee za michango ya hela kutoka kwa wadau wa elimu inaendelea kama kawaida
 
Sukari ni miongoni mwa vyakula hatari kabisa kwa afya duniani kwani huua nguvu za kiume, hushusha kinga ya mwili, ni aging agent, husababisha cancer ya kongosho, husababisha kisukari e.t.c!......Mimi huwa situmii kabisa mdudu huyu!
 
ndivyo tulivyo wabongo,watu wanalalamika bei ya sukari wamesahau ya kwamba elimu ni bure sukari ndo na hela hii inamaanisha ya kwamba sukari ni tamu kuliko elimu..
Ila diamond aliwahi kusema yeye ni sukari ya warembo....sijui kwa nini hawaendi na viroba kupanga foleni
 
Kuna namna nyingi ya kuwashughulia wanaovuruga upatikanaji wa sukari. ...mbili kati ya hizo ni hii ya Pasco kwamba tususie kutumia sukari ambayo ni ngumu kutekeleze ya pili ni kuwezesha wajasiriamali kuwa na viwanda vidogo kuzalisha sukari
 
Back
Top Bottom