5523
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 2,258
- 2,381
Ninaye broo wangu anaishi abroad miaka kadhaa, sio siri anatupiga tafu sana kwenye familia tunamtegemea kiukweli, aliwahi kuoa akiwa kule ulaya na kupata watoto 2 baadae wakaachana na yule mke wake wakagawa mbao.
Kuna kipingi tukaongea akanambia amepata mwanamke mwengine mtanashati mzuri (age yake kama 38 ivi) anataka kumuoa ili azibe pengo la yule alomuacha nikamwambia sawa ni jambo zuri, kuna kipindi alirudi kuja matembezi Africa na kuja naye huyu mama ambaye sasa anatarajia kumuoa akanitambulisha na nilimpa credit mama ametimia anamvuto wa hali ya juu nikamwambia hapa umepata na usipoteze muda huyu ndo atakuwa mke wako. Basi akafurai sana tukaondokeana atamfanyia posa na kuja kuoana naye soon na akarudi zake abroad nafkiri siku hii walilala pamoja.
Sasa huyu mama mimi baada kutambulishwa ikawa tunawasiliana on behalf of my brother, na nilizoea kumwita shem na huenda kwake ambako alikokuwa kapanga na nyumba alikuwa analipiwa kodi na broo, hushinda na kula chakula cha mchana, alikuwa ananijali na kuniheshimu sana kwa vile kaka yangu ndio anategemea kuoana naye.
Sasa kuna kipindi yule broo wangu alikatisha mawasiliano naye akawa hampigii simu na hela za matumizi ikawa hamtumii tena kikawaida huyu mdada ikawa sasa analalamika kwangu dhidi ya broo kwamba anahisi kama hamjali akinitaka mimi niongee na broo ili waweke mambo sawa.
Mimi humtwangia broo vipi mbona mdada analalamika huna mawasiliano naye kikawaida? broo anajibu ah ''kazi nyingi nikitulia nitamtafuta'' mara siku nyengine ananambia ''ah achana naye saivi mambo yang hayako sawa nitamtafuta'' muda ukawa unaenda hakuna mawasiliano naye kuna siku akanambia acha naye tu wewe mwambie nitampigia.
Yule mama akajuwa labda hatakiwi tena ni broo, sasa kwasababu mimi nilikuwa nawasiliana naye na kwenda kwake ikawa nishida na mimi kumkwepa ikawa tunapigiana simu kuulizana hali na stori za maisha ndogo ndogo.
Lakini katika maongezi yetu huwa analalamika sana kuhusu broo alivyomtenda mpaka kuna siku mimi nikamuonea huruma sana mpaka nikamtania kwa broo alivyokutenda nikwambia ''natamani kama ungekubali mimi nikakuoa ili kuziba makosa ya broo'' lakini mimi ukweli nilimwambia hivi kwa utani tu kama shemu wangu.
Dah yaani sijaamini macho yangu mama yule akaniambia mbona hakuna neno tena akafurahi sana akasema sawa niowe hata kesho nipo tayari, basi na mimi tena nikawa naona shida kwamba nimeongea utani ikabidi tukazama zaidi kwenye mazungumzo tukapendana tena kwa kasi ya ajabu.
Yaani huyu mama kwa kweli amenipagawisha sio kwa mapenzi tu lakini ana MAHABA saivi sioni wala sisikii chochote kwa yeye namuhisi kama demu wa miaka 19 ivi au 22 yaani nimeghumiwa.
Sasa huyu mama sasaivi anataka ndoa japo ya siri alimradi tu iwe imethibiti kisheria sasa bas ngoma iko kwangu Je broo kule akaja akaskia au akija huku akanikuta nimeoana naye japo yeye alimtenda? mimi ntakuwa mtu wa aina gani? Nahisi ntakuwa sina uso na broo akija Africa lazima atalala kwangu japo siku 2 au 3 mambo haya yatakuwaje?
Huyu mama yeye hana neno anasema hajali madam alimtenda lakini mimi najihisi mzito sana naogopa na ukweli hasa broo ofisi niliyonayo mradi ni wa kwake namuheshimu namuogopa ni kichwa kwenye familia.
Nimetafakari nikaona nilete hapa kwenye wataalamu wa ushauri hasa wa namna hii uhusu mambo yetu ili angalau nijuwe nianzie wapi naamini mtanishauri vyema tu, nipo hapa siondoki.
Nasubiri ushauri wenu
Kwenu wadau.