Mbona kero:tumechoka jamani...........................

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Barua ya wazi kwa wana JF wenzangu.................

Natumai ni wazima....Nimekuwa nikifatilia haya malumbano yanayoendelea katika hiki chama kilichojipa utawala yaani CCM...Kwa hakika kama ni mtanzania uliyemzalendo unaweza hata kujinyonga...kila kukicha mara


  • Shigela v/s Sumaye
  • Makamba v/s Sumaye
  • Kikwete v/s Magufuli
  • Sitta v/s vijana Tabora
  • Pinda v/s Magufuli nk
Hali hii inakera sana kama unatafakari kwa makini,

  • Hawa watu wanapata wapi muda wa kulumbana,na je muda wa kutimiza ahadi zao watapata?
  • Tutaendelea mpaka lini kushuhudia malumbano haya yasiyo na tija kwa taifa zaidi ya kunufaisha watu wachache tena mafisadi?
  • Watanzania tuchukue hatua gani iwapo hii mipasho itaendelea?
 
Waongo hawa mpwa, ni namna ya kutulia mali zetu hawana chochote wakiwa pamoja wanagongeana tano kama kawa tu
 
Inakera kwa wana ccm,ila kwa tusio itakia mema ccm ni shangwe kama sio ngazi!

Pole sana,kuliko kujiua bora uhame tu ccm
 
Back
Top Bottom