Mbona Kabendera hakuchangiwa? (maswali tata michango CHADEMA)

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
312
Reaction score
614
Wakati hukumu ya mwanahabari Eric Kabendera imetoka na kuamuriwa Alipe zaidi ya fedha za kiTanzania milioni mia mbili sikuona wanaharakati, wanahabari wala wafadhili wakichangisha fedha.

Kwa hukumu hiii iliyotoka dhidi ya viongozi waandamizi wa chama kikuu cha upinzani nchini nimeona ni ajabu kampeni za michango karibu dunia nzima ili kupata fedha za Kitanzania milioni mia tatu na hamsini, cha kustaajabisha sasa hata pamoja na Mashinji kuhama chama na kuchangiwa na chama chao kipya kiasi cha shilingi milioni thelathini, hivyo kufanya deni lililbakia kuwa milioni mia tatu na ishirini lakini wachangishaji bado wamesisitiza kuwa hela wanayotakiwa kulipa ni 350,000,000.

Nashindwa kuelewa Kabendera alikuwa na deni la zaidi ya milioni 200. Wale wote waliokuwa wanatembeza hashtag hawakujiongeza kufanya kampeni ya michango, na chama kikuu upinzani nchini kimeshindwa kulipa fedha hizo licha ya ruzuku, mishihara yao ya ubunge na wahisani.
 
Kabendera alikiri kwa kinywa chake makosa yake, which means hakuonewa na alistahili kuadhibiwa. asingekiri halafu akahukumiwa kulipa fine, definitely sisi Watanzania tungemchangia ndani ya 24 hours.

kina Mbowe hawakukiri makosa, na kibaya zaidi aliyemuua binti yetu Aquiline yuko mtaani anapumua kwa raha zake... hapa ndipo hasira ya sisi Watanzania kuwachangia kina Mbowe ilipokuja ghafla bila kujali itikadi zetu (mimi ni CCM baridi by the way!)
 
Alilipa m100 on spot watu wakajua kabisa uwezo anao,japo hata viongozi wa chadema wanao uwezo huo ila hawakujitutumua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabendera alikiri kwa kinywa chake makosa yake, which means hakuonewa na alistahili kuadhibiwa. asingekiri halafu akahukumiwa kulipa fine, definitely sisi Watanzania tungemchangia ndani ya 24 hours.

kina Mbowe hawakukiri makosa, na kibaya zaidi aliyemuua binti yetu Aquiline yuko mtaani anapumua kwa raha zake... hapa ndipo hasira ya sisi Watanzania kuwachangia kina Mbowe ilipokuja ghafla bila kujali itikadi zetu (mimi ni CCM baridi by the way!)
Katika mashtaka waliyosomewa kuna hata moja la mauaji?
 
swali la kujiuliza.... ni kwa nini shitaka la mauaji halimo?
ina maana hakuna aliyeuawa??

Kasome legality, mens rea, actus rea, causation, concurrence utajua kwa nini shtaka hilo halikuwepo
 
Wakati hukumu ya mwanahabari Eric Kabendera imetoka na kuamuriwa Alipe zaidi ya fedha za kiTanzania milioni mia mbili sikuona wanaharakati, wanahabari wala wafadhili wakichangisha fedha.

Kwa hukumu hiii iliyotoka dhidi ya viongozi waandamizi wa chama kikuu cha upinzani nchini nimeona ni ajabu kampeni za michango karibu dunia nzima ili kupata fedha za Kitanzania milioni mia tatu na hamsini, cha kustaajabisha sasa hata pamoja na Mashinji kuhama chama na kuchangiwa na chama chao kipya kiasi cha shilingi milioni thelathini, hivyo kufanya deni lililbakia kuwa milioni mia tatu na ishirini lakini wachangishaji bado wamesisitiza kuwa hela wanayotakiwa kulipa ni 350,000,000.

Nashindwa kuelewa Kabendera alikuwa na deni la zaidi ya milioni 200. Wale wote waliokuwa wanatembeza hashtag hawakujiongeza kufanya kampeni ya michango, na chama kikuu upinzani nchini kimeshindwa kulipa fedha hizo licha ya ruzuku, mishihara yao ya ubunge na wahisani.

We jitoe fahamu utaelewa tu, kwanza kesi ya uwongo na uonevu na unataka kutugombanisha na dola. Eric alitakiwa kuchangiwa pia lakini waambie hao dola waache kubumba hizi kesi hali ni ngumu mno.
 
Kabendera alikiri kwa kinywa chake makosa yake, which means hakuonewa na alistahili kuadhibiwa. asingekiri halafu akahukumiwa kulipa fine, definitely sisi Watanzania tungemchangia ndani ya 24 hours.

kina Mbowe hawakukiri makosa, na kibaya zaidi aliyemuua binti yetu Aquiline yuko mtaani anapumua kwa raha zake... hapa ndipo hasira ya sisi Watanzania kuwachangia kina Mbowe ilipokuja ghafla bila kujali itikadi zetu (mimi ni CCM baridi by the way!)
Hapa kuna maswali ya msingi, kwanini hakuchangiwa alikuwa na fedha za kutosha yeye mwenyewe ambazo chadema hawana? pili kwa nini wameendelea kukusanya milioni Mia tatu hamsini hata baada ya mashinji na Msigwa kulipiwa?
 
Hivi Eric Kabendera ni kiongozi wa Chadema, mwanachama wa Chadema au Je mashtaka yaliyokua yanamkabili yanauhusiano wowote na harakati za kisiasa???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kuna maswali ya msingi, kwanini hakuchangiwa alikuwa na fedha za kutosha yeye mwenyewe ambazo chadema hawana? pili kwa nini wameendelea kukusanya milioni Mia tatu hamsini hata baada ya mashinji na Msigwa kulipiwa?
1) hakuchangiwa kwa vile alikiri makosa ya kihalifu. uhalifu ni uhalifu tu!
2) ni sisi Watanzania wenyewe (humo tumo na kina siye wana CCM baridi) ndiyo tulioishinikiza Chadema kuchangiwa na ni sisi sisi Watanzania wenyewe ndiyo tutakaostopisha zoezi la kuchangia pale tutakapoona inafaa!

sawa sawa??
 
Back
Top Bottom