Mbona hawampi MKAPA digrii ya Heshima ya UCHUMI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona hawampi MKAPA digrii ya Heshima ya UCHUMI?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by leroy, Apr 23, 2012.

 1. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 842
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Degrii za heshima zimekuwa zikitolewa na vyuo mbalimbali duniani ili kutambua mchango wa mtunikiwa katika eneo husika.

  Hatuna shaka na utendaji wa utawala wa Benjamin mkapa katika kukuza na kuimarisha uchumi na kuleta unafuu kwa wananchi kupitia nidhamu ya matumizi, mfumuko wa bei mdogo, ukusanyaji bora wa mapato na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

  Kwa nini basi taasisi za elimu hazitambui mchango huu wa mtu huyu muhimu katika taifa letu?
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nimependa Avatar yako! Anko Ben hawezi kupewa kwa kuwa kunaushindani mkubwa sana kati yake na Jeykey. japo alituingiza katika mikataba feki na mibovu mingi, Ben amejitahidi sana. hazina aliyoiacha ndio nauli ya safari za mkweeree!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkapa sio mtu wa misifa-misifa na propaganda
   
 4. H

  HIPSON Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa maneno machache sana yenye maana nzito na sahihi juu ya Brother BEN. hizi degree za honoris caussar au za heshima wakubwa wengine huwa wanaziomba tu au kulazimisha kupewa ili apate misifa na propaganda. ****** ana sifa gani ya kuitwa Dr ? si misifa tu!
  Hakiyambongo bit mhamali ningekuwa na uwezo ningemwambia Ben Willy Mkapa awe raisi tena nadhani hata mawaziri hawa wangekimbia wenyewe. Urais siyo mchezo wa kuigiza ila ni kazi. mkapa kazi tu masifa mtampa mkitaka msipotaka leave him alon
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mbona itakuwa kama kuwatukana Watanganyika na Jinsi alivyoyagawa Machimbo ya Dhahabu kwa Ushauri wa IMF na World Bank, bila nchi kupata share yoyote na investor kupata 100%, ukiangalia Bostwana wana 40%

  Kama alifufua Uchumi kiundani aliimaliza uchumi wa nchi kwa kugawia wawekaji
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli sijawahi kusikia Ben akipewa udaktari wa heshima. Ben ni mahiri kwenye uchumi na hata lugha. Kwa hakika kabisa Ben alistahili kupata shahada ya heshima ya uzamivu kwenye uchumi.

  Mimi kuanzia sasa nitakuwa nikimuita Dr. Benjamin William Mkapa. Nimempa degree ya heshima ya uzamivu kwani lazima itolewe na akina Mkandala?
   
 7. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Yule jamaa hawezi kufanya ujinga wa kuomba digrij ya heshima kama anavyofanya JK. Ile PhD ya Muhas aliyopewa na Pallangyo ni moja ya vitu ambavyo vinadhalilisha hata hadhi ya chuo kwa sababu binafsi za Pallangyo. Digrrii ya heshima aliyonayo BWM ni uchumi imara aliotuachia.
   
 8. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwahi jk anatumia akiba aliyoizalisha mwanaume mwenzake!?
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu unataka kumaanisha enzi za ben hakukuwa na mawaziri wezi? wakati akina mramba na wengine wengi walikuwa ndo manguli wezi kipindi hicho sema hakukua na upinzani imara na walikuwa hawaruhusu wizi wao kuanikwa bungeni!
   
 11. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Aliwatukana watanzania kila walipolalamikia anavyogawa kama njugu uchumi wa nchi. Aliowagawia uchumi wetu bure wanamwona anao ufinyu wa kufikiri na anao wivu wa kijinga kuliko watu wake aliozoea kuwaambia hivyo, ambao haustahili degree ya aina hiyo. Kwa nini huulizi mzee Ruksa aliyewawezesha watanzania wengi sana kumiliki njia kuu za uchumi hata wengine wamekuwa mafisadi waliokubuhu kutokana na mtaji ule?
   
 12. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Lekanjobe usikurupuke kuchangja na ikibidi bakia msomaji tu. Nenda kwenye link ya mchangiaji anayeitwa consigliere hapo juu utaona kuwa jamaa BWM amekwishatunukiwa PhD mbili moja ya Kenyatta na nyingine ya Makerere tatizo ni kwamba yeye hajashurutisha watendaji na waandishi kumu address kama Dr Mkapa. Na kutokana na ufinyu na uvivu wenu wa kusoma nyie watanzania sampuli ya Lenkanjibe, ndiyo maana BWM anawadharau
   
Loading...