Mbona CHADEMA siku hizi hawaongelei Tume Huru?

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,258
1,541
Eti wapendwa wangu Chadema, siku izi naona mpo kimya sana juu ya swala la tume huru. Mana naona muda unazidi kwenda. Kama kweli hawana iman na tume huru waanze kushuhulika nayo sasa hivi wasisubiri mpaka uchaguzi ufanyike ndio wajitokeze hadharan na kusema tume haikuwa huru; watu tutaelewa kuwa maoni ya tume huru yalitolea kama silaha itakayotumika baada ya uchaguzi kuwa haukua huru na kuwa source ya vurugu. Nawakanya Chadema msijaribu kufanya hivyo.

Kama kweli tume mnaiona siyo huru basi hakikisheni mnagomea uchaguzi mpaka pale serekali itakapo idhinisha tume huru. Onyo kwenu pia Chadema; mwenendo wenu na Wabunge wenu wanavyowatupieni lawama na wengine mpaka kufikia hatua ya kuhama, hii inaweza ikawa mbaya kwenu pale tu mtaposusa uchaguzi halafu vyama vingine vikaingia kwenye uchaguzi.

Ila mkisubiri tume, muanze kuidai baada ya uchaguzi au kwenye kampeni nitashauri mpigwe maana mmekaa miaka zaidi ya 50 mkiwa kama wapinzani hata kama sio Chadema lakini mliridhika na tume, hivyo tume ni huru na salama mkitaka tume ibadilishwe, basi itabidi muombe na katiba ifanyiwe marekebisho kwani yenyewe ndio muhimil wa kila kitu.

Chadema kama kweli tume sio huru, anzeni kudai sasa hivi japo mmesha kaa miaka mingi na kwa baraka za tume hio mmeendelea kua wabunge msije mkaenda kwenye majukwaa ya kampeni na kuanza kuongelea tume huru mtakuwa mnawachanganya wananchi sababu wata jiuliza huu ni muda wa kampeni mwezi fulani tunaenda kupiga kura viongozi wetu wanatuambia tume sio huru. Tufanyeje, embu Chadema mtawajibu wafanyeje kwa muda huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan tume huru inamsaidia nn mtanzania wa kawaida? Au itasaidia kuingiza chadema madarakan?
Suala la Tume Huru ya Uchaguzi na pia kuurejesha mchakato wa Katiba ya Watanzania ili kuondokana na ile Katiba ya Ccm ya mwaka 1977, siyo ya Chadema pekee! Ni ya Watanzania wote Wazalendo na wapenda mabadiliko ya kweli ya Kidemokrasia nchini.

Mimi ni mmoja wao, wewe je!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan tume huru inamsaidia nn mtanzania wa kawaida? Au itasaidia kuingiza chadema madarakan?

Sent using Jamii Forums mobile app

Tume Huru ya Uchaguzi itasababisha Uchaguzi wowote ukt utakaoitishwa, kuwa Huru na wa Haki! Hata jambo hili dogo tu hilifahamu?

Yaani zile sarakasi zenu za kukimbia na maboksi ya kupigia kura, kutumia bao la mkono, DED kutorokea mlango wa nyuma wakati wapinzani wanapo rejesha fomu ya kugombea, zitapungua au kuisha kabisa!

Mwenyekiti na Mkurugenzi wa hiyo Tume atajadiliwa na kuthibitishwa na Bunge kwanza badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Mwenyekiti wa Ccm Taifa, nk. Umenielewa sasa?
 
Kuna Watanzania wanashangaza sana kwa kudhani issue ya kuwepo Uchaguzi HURU na wa HAKI chini ya tume huru haiwahusu wao bali inahusu Chadema tu. 😳😳😳

Suala la Tume Huru ya Uchaguzi na pia kuurejesha mchakato wa Katiba ya Watanzania ili kuondokana na ile Katiba ya Ccm ya mwaka 1977, siyo ya Chadema pekee! Ni ya Watanzania wote Wazalendo na wapenda mabadiliko ya kweli ya Kidemokrasia nchini.

Mimi ni mmoja wao, wewe je!!
 
Siku ukitia akili kichwani UTAELEWA TU. Kwa sasa endelea na dhana yako POTOFU kwamba HAIKUHUSU.

Kama saivi wanakula posho tu mara wakimbie bungen waseme Corona mara warudi wao wanajali matumbo yao tu Sasa Mimi tume huru inanihusu nn bwashee
 
Suala la Tume Huru ya Uchaguzi na pia kuurejesha mchakato wa Katiba ya Watanzania ili kuondokana na ile Katiba ya Ccm ya mwaka 1977, siyo ya Chadema pekee! Ni ya Watanzania wote Wazalendo na wapenda mabadiliko ya kweli ya Kidemokrasia nchini.

Mimi ni mmoja wao, wewe je!!
Bora umeniwahi kiongozi, kuna watu humu tunashindwa kuwaelewa kabisa.
 
Kwamfano sasahivi tukisema mwenyekit wa tume ajadiliwe bungen Kama mnavyosema kabla ya kupitishwa mtakubal matokeo Mana Apo ni wazi lazima CCM itashinda Tena Mana wao ndio wengi au mnataka tume huru muipange nyie chadema?

Back
Top Bottom