Mbivu, mbichi kesi ya kampeni kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbivu, mbichi kesi ya kampeni kesho

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Sep 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa chama cha Sauti ya Umma (Sau), Paul Kyara (wa tatu kushoto), akitoka nje ya jengo la Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam na wakili wake Israel Magessa (kulia) baada ya kesi yake kuahirishwa jana. Wengine ni wanachama na wapenzi wa chama hicho.  Maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau), Dk. Paul Kyara, ya kutaka kampeni za mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu zinazoendelea hivi sasa kote nchini zisimamishwe, yatasikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, kesho.
  Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, baada ya kukubali ombi lililowasilishwa na mawakili wa upande wa serikali mahakamani hapo jana.
  Mawakili hao wakiongozwa na mwenzao, Edson Mweyunge, waliliomba jopo hilo liwape muda ili wapate fursa ya kujibu na kuwasilisha mahakamani leo majibu dhidi ya maombi na kesi ya msingi iliyofunguliwa na Dk. Kyara mahakamani hapo Septemba 9, mwaka huu.
  Jopo hilo linaloongozwa na Jaji Samuel Karua, lilikubali ombi hilo na kuuamuru upande wa mlalamikaji (Dk. Kyara) kuwasilisha majibu dhidi ya majibu ya serikali kesho kama itabidi kufanya hivyo, kabla ya maombi hayo (ya Dk. Kyara) kusikilizwa keshokutwa.
  Mlalamikiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 80 ya mwaka 2010, ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wa pili, ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
  Majaji wengine wanaounda jopo hilo, ni Jaji Haruna Songoro na Jaji Fauz Twaib.
  Maombi hayo yaliwasilishwa na Dk. Kyara mahakamani hapo kwa hati ya dharura akitaka yasikilizwe haraka.
  Anataka kampeni hizo zisimamishwe hadi hapo kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa.
  Katika kesi yake ya msingi, Dk. Kyara, ambaye anawakilishwa na jopo la mawakili wanne, linaloongozwa na Wakili Israel Magesa kutoka kampuni ya Magesa & Company Advocates, anaiomba mahakama iiamuru NEC imteue kuwania urais wa Jamhuri Muungano katika uchaguzi huo.
  Dk. Kyara anadai aliteuliwa na chama chake kuwania kiti hicho katika uchaguzi huo, lakini NEC ikashindwa kumtendea haki, baada ya kumzuia kufanya hivyo kwa misingi ya ubaguzi, kinyume cha maadili ya uchaguzi.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nadhani hii ni mbinu ya kutaka JK apumzike akatibiwe!!!!!!!!!!!!!!!!! Walikuwa wapi hawa jamaa???
   
Loading...