Mbiu ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania imeishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbiu ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania imeishia wapi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ibrah, Sep 14, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mwaka 2005, Mgombea wa CCM Jakaya Kikwete alituchota sana na kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania hadi tukampa kura za ushindi wa kishindo. KIlichofuatia baada ya hapo ni kwa Watanzania wengi kukata tamaa ya hayo maisha bora kiasi cha kuwauliza Viongozi wetu mbona maisha bora hatuyaoni? Tukapewa majibu mepesi kweli kweli atri Maisha bora hayaji hivi hivi bila kufanya kazi kwa bidii! Wafanyakazi wamejitahidi kudai hata kwa kutumia nguvu za TUCTA lakini wapi.

  Umefika mwaka 2010, ile kauli mbiu ya Miasha Bora kwa Kila Mtanzania hatuisikii tena, hata yale mabango ya kumnadi Kikwete mwaka huu hayana ile kauli mbiu ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania; sijui wamesahau kuiweka au wanaogopa kuulizwa kwenye mikutano yao ya kampeni, wanajua wao wenyewe. Ajabu ni kuwa hata kwenye mikutano yao ya Kampeni Wananchi hawawaulizi au kuwakumbusha juu ya kauli mbiu ya Maisha Bora. Si ajabu ndo maana CCM wamekacha midahalo.

  Kwa wale wanaohudhuria mikutano ya CCM ya KAmpeni muwakumbushe na kuwauliza ile Kauli mbiu ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania imeishia wapi?
   
 2. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Chama cha mafisadi wanatatakiwa kurudishwa kwa nguvu kwenye midahalo ili watueleze kinagaubaga falsafa ya maisha bora imeishia wapi? Naona ilitelekezwa punde madaraka yalivyotwaliwa.
  Sasa wananchi tunahitaji majibu, maisha bora yako wapi?
  Amini nawaambieni, kukwepa midahalo asilani siyo suluhisho kwa sasa!!
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,592
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Kwani zingine ziliishia wapi? kwani hujuhi kuwa hawa jamaa ni hodari wa mipasho? Kauli mbiu zao ni kama vibwagizo vya Taaharabu baada ya msimu vina pita. wanaleta vipya!
   
Loading...