Mbio za Uraisi 2015: Kuna nini katika kuugua ghafla kwa Prof. Mwandosya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbio za Uraisi 2015: Kuna nini katika kuugua ghafla kwa Prof. Mwandosya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Sep 8, 2011.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2011
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Kuna wingu zito linalozidi kutanda juu ya suala zima la afya ya Prof. Mwandosya, ambaye aliugua ghafla wakati wa kikao cha Bunge cha hivi karibuni na kukimbizwa Muhimbili na hatimaye India kwa matibabu. Bila shaka wengi tumeona posts juu ya ziara za mkuu wa dola katika wizara, na waraka unaosemwa kutumwa kwa Nape, kuwa inaonekana huyu Prof. bado ni tishio kwa baadhi ya kambi ndani ya CCM katika suala zima la nani atashika hatamu za kugombea uraisi kwa ticket ya CCM. Katika posts nyingi kwenye JF wengi wamekiri kwamba Prof Mwandosya ana kichwa makini, na kwamba katika kipindi chote cha uwaziri wake amejidhihirisha kuwa mtu makini na mchapa kazi, anayeheshimika ndani na nje ya mipaka ya TZ. Hata kuna post iliwekwa kwamba mkuu wa dola anamuogopa Prof Mwandosya na hawezi hata kuthubutu kumbwabwajia kama anavyowafanyia mawaziri wengine. Wengine hata wameripoti kwamba ngamia alishachinjwa jangwani ili kumfanyizia na ikagonga mwamba!

  Habari zinazompamba na kumweka katika duru ya wagombea wa uraisi (kama una habari tofauti tafadhari tueleze) ni pamoja habari kwamba Mwandosya alijitoa Wizara ya Nishati wakati mkuu wa dola akiwa waziri pale kwa kuwa alimwona mkuu wa dola kuwa "mtupu" mno na akasema hawezi kufanya kazi naye. Na pia kuna taarifa rasmi kwamba Mwandosya ndiye aliyem-groom Patrick Rutabanzibwa baada ya kuona utendaji wake makini. Hii inamfanya aonekane kama siku nyingi aliona weakness za mkuu wa dola ingawa wengi hawakuona hili.

  Pia kuna taarifa zinazosema Prof alijipatia sifa kubwa katika duru ya mijadala ya "climate change" wakati wa mjadala wa Makubaliano ya Kyoto, kiasi kwamba Makamu wa Raisi wa Marekani wakati huo Al Gore alimtaja kuwa mmoja wapo wa waafrika wenye akili sana, na Bill Clinton wakati wa ziara yake Tanzania alimshauri Mkapa amtumie katika baraza lake la mawaziri. Hii ilikuwa ni baada ya Prof Mwandosya kutumikia katika mazungumzo hayo kama Spokesman wa G77 and China. Kutokana na umakini wake inasemekana Marekani walimwalika Washington kama mgeni rasmi wa "State Department" na kumwalika kutoa hotuba katika vyuo vikuu kadhaa.

  Kulikuwa na jitihada za kumhusisha na kashfa ya unununzi wa rada, na inasemekana ziligonga mwamba kwa kuwa hakuhusika, japo yeye ndiye aliyetumiwa na serikali kuwashawishi wawakilishi wa Uingereza kwamba ni kweli Tanzania ilihitaji rada hii japo unnuzi wake ulikuwa na mushkeli.

  Wengi wa mawaziri ukiwauliza juu ya Prof Mwandosya wanasema ni mtu asiye na mzaha, na ukifanya kazi chini yake lazima utamheshimu na kumwogopa kwa namna fulani kwa jinsi alivyo serious na issue za kazi.

  Sasa kuna wasiwasi kwamba suala zima la kuugua kwake ghafla linahusiana na mbio za uraisi 2015 na lilikuwa na mkono wa watu! Kama kuna taarifa juu ya hili tafadhali tuelezane zaidi.
   
 2. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Binafsi,naona nyakati hazimuungi mkono prof mwandosya tena.
  Umri na magonjwa vinamwandama sana.
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana ni mgonjwa anajiuguza nje yaa nchi, muacheni ajiuguze na mwenyezi Mungu ampe afueni! Sidhani hata kama anafikiria mambo ya sisa wakatii huu kwani afya yake ni muhimu kuliko kitu kingine chochote kwa wakati huu. Nyie wapambe wake acheni nuksi zenu.
   
 4. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kwanza nakubaliana kabisa kwamba huyu bwana kipaumbele chake sasa hivi ni afya yake na si siasa. Lakini pia ningependa kusisitiza umakini katika haya masuala ya kuamini kwamba katika mazingira kama haya kuna mkono wa mtu dhidi ya afya yake. Nadhani tujaribu kupambanua mambo kwanza kwamba anaumwa ugonjwa gani. Haya mazoea ya kuamini ushirikina huwa hayana tija kwa kweli. Tuchukulie kwa mfano ifahamike kuwa anasumbuliwa na kansa, je huo nao utakuwa ni mkono wa mtu?
  Tusisahau vilevile kuwa kwenye maisha huwapo matukio mengi ambayo ni coincidence, tusiwe wepesi kupigia mambo mstari bila kuwa na true facts.
   
 5. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama Prof. Mark bado ana ndoto za urais kwani umri umekwenda na pia ni mtu anayetambua maana ya democracy. Anajua kuwa kuwatumikia watz si lazima kuwa rais.
  Pona haraka mkuu.
   
 6. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Ina maana wanasiasa hawaugui?
   
 7. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Amekutuma? Au ndio prof mwenywe ww?
  <br />
  <br />
   
 8. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waache wafu wazike wafu wao.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  In such times, when we know for a fact that there are things we can't change, it is crucial we think outside the box.
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  What an objective counsel!
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Umri nao umemtupa mkono, sidhani kama kuna mkono wa mtu katika ugonjwa unaomsumbua!
   
 12. m

  mndeme JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  habar yenyewe imekaa kimajungu majungu sana na tetesi ni nyingi kuliko uhalisia, ingawa ktk siasa michezo ya kulogana ipo hasa wakat huu wa makundi ya magamba lakini hizo ni porojo tu coz time is not in favour of mwandosya
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Swali zuri mnoooooooo, wazee tupeni majibu.
   
 14. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Shehe Yahaya(RIP) hayupo angekupa jibu maana imani nyako iko upande wake!
   
 15. W

  We know next JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hayo mambo ya Siasa mie sijui, ila nacho jua na kuamini ni kwamba, Prof. Mwandosya ni kichwa kati ya vichwa vichache Africa vinavyotambuliwa na jumuiya za Kimataifa hasa katika mambo ya mazingira particulary issues za Climate Change. Ameshapata mialiko mingi sana ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi, lakini nadhani kutokana na uzalendo wake amekuwa akipenda zaidi kuitumikia nchi yake. Hapa nchini katika duru za Siasa, hakuna shaka wengi ktk ngazi za juu wanafahamu kuwa Prof, ni Kipanga. Pole Prof, Mwandosya
   
 16. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapna jamani hata kama huyo mwandosya ni mzuri kiasi gani kwa kizazi hiki cha com hawezi kuwa rais. Kwanza: Anatoka chama Kikongwe ( wahenga walisema ng'mbe mzee huwezi mfundisha mbinu mpya ya kulima) Pili: maarifa yake na mafanikio yake hayaonekani kwa wazi kwanini ( compare with John magufuri) Tatu: kabila analotoka lina tatizo la ukabila hwavumiliki Nne:.................( endeleza)
   
 17. m

  mtoto wa mama Senior Member

  #17
  Sep 9, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  i think mtoa mada hii anafikiri kwa kutumia didas masaburi na sio ubongo... anaunganisha vtu tofauti kabisa.. think before act au ndio kutaka kuwa premium member wa jf..
   
 18. inols

  inols JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  now comes conspiracy theorists ........... halafu haina hata mashikio. Please come up with something better than this!!!!
   
 19. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  All thoughts and prayers for a speedy recovery .. ni ugonjwa tu/ hakuna cha uraisi 2015 wala nini.
   
 20. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  yaleyale ya baba wa taifa..mi siku hizi sipuuzii mambo..
   
Loading...