Ccm ina mambo ya kuudhi na kuumiza sana. Huyu jamaa,
Kwanza alionyesha failure kubwa ya uongozi alipokuwa waziri mkuu. Akaanza kutuingiza kwenye mikataba ya wizi kwa kusingizia eti walishirikiana na swahiba wake. Huo ni utetezi? Kufanya wizi kwa kikundi hakumfutii mwizi sifa ya wizi.
Baada ya kukurupushwa na Mwakyembe, akasoma upepo, mara akaanza kujenga kundi ndani ya ccm kwa kugawa pesa. Kisha akaanza kujipendekeza kwenye makundi mbali mbali ya watanzania waliokuwa wanahitaji michango. Lengo halikuwa kufanikisha shughuli changiwa ili waboreshe maisha yao. Lengo sahihi ni kujijengea umaarufu, akilenga 2015 na akajua, mbwa mwenye njaa, mtupie tonge tu anasahau lindo. Angelikuwa najali watanzania asingewaibia.
Muda umewadia, jamaa kaanza kuwafunga mikono na miguu wale wanaompinga kwenye jimbo lake, kwa kutumia cheo cha ubunge. Hapa anaonyesha mwendelezo aliouasisi ccm na mwenzie wa matumizi mabaya ya madarka kibabe.
Baadaye anatangaza kwamba hagombei ubunge lakini lazima mbunge awe yule anayemtaka yeye. Yeye anagombea uraisi!!!!!!!!1
Kwa kutumia mtindo ule ule wa mbwa mwenye njaa mtupie tonge asahau lindo, jamaa anatupa tonge kwa watanzania maskini na wajinga ili wacheze sinema ya kujifanya kwenda kumshawishi. Wakati alishatanganza nia na kuanza kampeni mapema, sasa anakuja na kauli eti kutokana na makundi mengi ya watu kwenda kumshawishi angombee uraisi, ameshawishika muda ukifika atachukua form.
Kaona ccm wamemshitukia na upinzani mkali ndani ya chama chake, sasa anatumia tonge, kusambaratisha CC iliyopo ili atengeneze inayomuunga mkono yeye. Kama kule kule wilayani kwake, kuhakikisha wanaompinga wanafutika.
Halafu baada ya cc yake kumpitisha, hatujajua atakuja na lipi tena. Lakini hadi hapo, tayari huyu mtu ameshaonekana ni mtu wa namna gani.
Kwanza hana sifa wala uwezo wa kuongoza ndiyo maana hana jambo la kujivunia badala yake anatumia fedha alizowaibia watanzania ili kuwazubaisha. Akishakuwa ikulu, na uwezo hana, na gharama alizotoa, nini kitafuata?
Pili anajua hakubaliki ndiyo maana sarakasi za maigizo na mbinu haramu nyingi. Yote haya analazimisha ni kwa maslah i ya nani?
Tatu jamaa ni dictator tena hater asiyekuwa na utu wala kujali demokrasia. Anatumia nguvu na zana yoyote kuhakikisha wanaompinga siyo wanamkubali, bali wanapotea na wasisikike tena. Kaanzia kwenye jimbo lake, sasa amefika kwenye ccm, akipata uongozi hii nchi itakuwaje? Atawafanya nini wenye mawazo tofauti na yake ndani na nje ya chama chake? Mwenye macho haambiwi tazama.
LAKINI CCM KWELI ANAKWENDA KUISAMBARATISHA KWA KUANZIA KUIUA CC ILIYOPO ATENGENEZE YA KWAKE ITAKAYOFUATA ANACHOTAKA YEYE!. Ndiyo ccm mnataka mtu mbinafsi na dictator lakini bahati mbaya asiyekuwa na ufahamu wala moral principles kama huyo?
YES, BILA SHAKA CCM IMERIDHIA. NA KWA MTAJI HUO, WATANZANIA HATUTAKI KUMWONA AKIPIGIWA DEBE LA KURA KWENYE KAMPENI. CCM MSISIMAMISHE MGOMBEA HATA KAMA MTAKOSA RUZUKU KWA SERIKALI YA UKAWA LAKINI SI MATUSI KWA WATANZANIA YA KUWAWEKEA MTU WA NAMNA HII.
MISINGI YA NCH YETU HAIJAFIKA HUKO JAPO MMEIDHOOFISHA KWA KIASI KIKUBWA.