Ndibalema
JF-Expert Member
- Apr 26, 2008
- 10,956
- 4,647
Jamani hii ni kweli kabisa, yamenikuta.
Ilikuwa hivi,
Ilikuwa mida ya alfajiri mi na waifu tumejihimu tunaelekea kituo cha dala dala ili tuwahi daladala tukamwone ndugu yangu mgonjwa aliyelazwa ktk Hospitali ya Muhimbili.
Kama unavyojua mida ya mapema kama hiyo dala dala huwa ndo kwanza zinaamka.
Wakati tunakaribia kituo cha daladala tukasikia sauti ya mpiga debe..."Mtonganiii.....Temekee....Kariakoo...
..Muhimbiliiii wahi bado wawiliiiii"
Nikamhimiza waifu akaze mwendo kwani tusije tukaikosa hiyo daladala
huku nikimpigia mkwara kuwa nitamwacha 'kwenye mataa' mi niwahi kama hatokaza mwendo.
Sasa tukawa tunaikaribia ile daladala ambayo tulikuwa tukiona imewasha taa za mbele kutokana na kigiza kile cha alfajiri.
Ingawa nilijiuliza mbona taa za nyuma haziwaki lakini sikutilia maanani.
Kuikaribia karibu zaidi ndo hapo tulipobaki hoi.
Kumbe pale tulipofikiri imepaki gari, palikuwa wamesimama jamaa wawili wamewasha tochi ambazo kwa mbali tulifikiri ni taa za gari,
pembeni palikuwa na jamaa mwingine anapiga yale mayowe ya kuita abiria.
Wakati mi na waifu tumetahamaki, ndidpo walipotokea jamaa wengine wapatao nane au zaidi mikononi wakiwa na mapanga makalii.
Nikawa mpole huku waifu akinisihi nisilwaletee ubishi vile vipande vya watu (unazani ningethubutu!!)
wakatupora kila kitu (kasoro mavazi) ikiwemo chupa ya uji wa mgonjwa na vitafunwa.
Bahati nzuri hawaku tujeruhi.
Na safari ikafia hapo.
Ingawa mi na waifu tumekubaliana tusimsimulie yeyote, ila mi nimeona kwa tahadhari niwahabarishe wana JF.