Mbinu za uizi wa kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbinu za uizi wa kura

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Fredrick Sanga, Mar 28, 2012.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimeona kwamba ni vizuri tukiziweka wazi mbinu zinazitumika kuiba kura ili wanauhusika waweze kuudhibiti uizi huu ambao unawaza kutuvunjia amani yetu tuliyonayo:

  1 Kupiga kura zidi ya mara moja: Bandika wino usiotoka (Ukitoka je)
  2 Gawa shahada kwa wasio husika: Mawakala kuwagundua kwa sura
  3 Kugawa karatasi zaidi ya moja kwa mpiga kura: Wakala kuwa makini
  4 Kutumbukiza kura katika box kabla ya kufunga
  Kufunga kituo: Wakala akihongwa anakubali. (Sijui hapa watafanya nini)
  5 Mpiga kura anaweza kuingia na karatasi nyingi za kura alizopigia nyumbani. Hii hutumika sana kama masanduku ya kura yakiwekwa kwenye vizimba. (Tunazibiti vipi)
  5 Tuwe makini na hizi Ambulance zinazokpita pita kila mara haswa wakati huu wa Uchaguzi (Tafanyeje sasa)

  6 Kutumia nguvu kuwatisha mawakala, kuchakachua (Nini kifanyike), hii inaweza ikawa katika vituo vya kupigia kura, wakati wa kusafirisha masanduku na wakati wa majumuisho. (Hapa naona ipo kazi, labda mawakala wa nguvu wasioogopa MG)
  7 Kuwahi sana kupiga kura na kuwaacha mawakala peke yao katika vituo (hapa inakuwaje?)
  8 Segerea style, kukimbia na masanduku ya kura. Hapa panahitajika escot ya nguvu sana, bila hivyo sijui. Bodaboda wanaweza hii kazi.
  9 Je Magari ya Jeshi yanaweza kutumika, Basi tume ipate ma MP ili kushirikiana na wananchi wenye wasiwasi.
  10
  kuanzisha vurugu kituo cha kupigia kura hasa mida ya jioni. (Kuabakia katia vituo m 103 hadi kura zinapoondoka)
  11 Karatasi ya kupigia kura huchanwa kwenye kitabu: Kwa maana hiyo idadi ya kura zinazopigwa ni lazima iwiane kwa idadi na serial namba za karatasi, itakayokosekana kwenye kishina cha kitabu si kura halali. mawakala wahesabu idadi ya karatasi zilizotumika, wawianishe kwenye vishina wakati wa kuhesabu.
  12 kutumia chupa za chai na hotpot za vyakula.
  (Zinapoletwa kwa mawakala zisachiwe)
  13 Kuwapotosha wapiga kura kwa taarifa za uongo siku ya kupiga kura. (Tumienin mawakala kupata taarifa sahihi)


  Hebu changia nyingine, na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kubana mianya hiyo.
   
 2. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Vile vile mpiga kura anaweza kuingia na karatasi nyingi za kura alizopigia nyumbani. Hii hutumika sana kama masanduku ya kura yakiwekwa kwenye vizimba.
   
 3. s

  sawabho JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  katika matumizi ya pesa na akili, hakuna lisilowezekana chini ya juu.
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Money is the source of all evil.
   
 5. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,268
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Tuwe makini na hizi Ambulance zinazokpita pita kila mara haswa wakati huu wa Uchaguzi.

  Jiulize wagonjwa wameongezeka sana kipindi hii?
  Ni mzigo unapitishwa huo kupelekwa vijijini
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hiyo mizigo inashushiwa wapi? Tutoe taarifa wapi?
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  1. Kila mpiga Kura ahakikishe anawahi mapema na Kupiga kura.
  2. Kila moja wetu ahakikishe anakaa nje ya mita 100 kutoka kituo cha kupigia Kura.
  3. Hakuna kumwogopa mtu yeyote awe Askari etc.
  4. Kukesha kwenye kituo hadi matokeo yatangazwe...
  5. Hakuana Mtu au Gari yeyote kwenda kwenye eneo la kuhesabia kura mpaka likaguliwe ikiwa nje ya mita 100.
  6. Kusindikiza masanduku ya kura hadi kituo kikuu cha kuhesabia kura.. Ofisi za halimashauri.
  7. Kukesha kwenye kituo cha kutangazia matokeo hadi matokeo yatakapotangazwa kituo kwa kituo na Jumla kuu.
  Hii inatosha?
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivyo vyakula vya kulaza usingizi je.
   
 9. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  umesahau mbinu hii iliyompatia mahanga ubunge.
  9.KUKIMBIA NA MASANDUKU YA KURA!
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Hiyo ipo No 8 Inaitwa Segerea syle, Kukimbia na Masanduku ya Kura (Hapa panahitajika escot ya nguvu ya masanduku.)
   
 11. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mmesahau magari ya wanajeshi kupitapita nayo yakaguliwe mnalisimamisha na kuwashusha wote na kuwasachi ni haki yenu!
   
 12. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hapa inabidi tume iombwe kutoa ma MP ili hili zoezi lifanikiwe. Maana hawa wanapolice wao sijui itakuwaje hapa. Labda Dr atalijua hili.
   
 13. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kuanzisha vurugu kituo cha kupigia kura hasa mida ya jioni.
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii huwa inatokea, hasa askari ambao hawakupangiwa kusimamia vituo, na huwa hawajapata mafunzo ya tume.
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  karatasi ya kupigia kura huchanwa kwenye kitabu kwa maana hiyo idadi ya kura zinazopigwa ni lazima iwiane kwa idadi na serial namba za karatasi, itakayokosekana kwenye kishina cha kitabu si kura halali. mawakala wahesabu idadi ya karatasi zilizotumika, wawianishe kwenye vishina wakati wa kuhesabu.
   
 16. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Oo Mama hii inaonekana kuwa super trick, sikuwa naijua kabisa hii. Big up
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa tunakaribia sana ule muda wa kupiga kura huku Arumeru, Tupeni mbinu zingine zinazotumika, nia yetu ni kuziweka wazi ili zidhibitiwe.
   
 18. Maruku Vanilla

  Maruku Vanilla Member

  #18
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Ukistaajabu ya Wade, utaoona ya Sioi na ccm......... Nabashiri barriers kuwekwa njia kuu za kuingia Arumeru East kuanzia kesho, abiria waliofunga safari rasmi kwenda kutumia haki yao kupiga kura, watakaguliwa, watabughudhiwa, wataibiwa IDs, watacheleweshwa na wataruhusiwa ktk muda ambao hawataweza kuwahi kufika vituoni kabla zoezi halijafungwa. Utoto mwingine; wako watu ccm wanaona kutega miiba na misumari njiani nao ni ujanja na mbinu itakayowapa ushindi kwa kupunguza kura za wanaotoka mbali. Hamtoamini, kuanzia Jmosi Arumeru itakuwa na matrafiki wengi kuliko wa Dar. Magari yanayoondoka mikoa ya karibu (Arusha, Kili, Mantra, etc) kuja Arumeru yatakamatwa hovyo hovyo na askari katikati ya safari kwa kisingizio cha Ukaguzi wa Kawaida.
   
 19. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kigoma na Pemba pekee ndo wameweza kuwadhibiti CCM,kule watu wamepigika mifukoni sio kichwani kama watu wengi wa maeneo mengine wakioneshwamwekundu wanakodisha shahada zao mpaka uchaguz uishe!
   
 20. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hapa hili nalo neno, Je wameru wakoje, hebu tusaidie kwa hili.
   
Loading...