Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,363
- 1,135
Inachekesha lakini inasikitisha at the same time kwasababu ndio ukweli.Ndio maana nimekuwa nikiwaambia marafiki zangu kuwa CCC haiwezi kukubali kuwaelimisha watu.Wanajua wakifanya hivyo ulaji utapotea kwani watu watajua haki zao.CCM wanataka classes.Watawaliwa na watawala.Angalia budget ya serikali..chunguza uone kama elimu imepewa namba moja kama inavyostahili.!Rais mpenda watu na maendeleo anashindwa kuifanya budget ya elimu kuwa ndiyo itakayopewa pesa nyingi kuliko kuliko ya mashangingi,marupurupu,na mishahara?Kama wananchi wakijua kuwa pesa zote hizo wanazozitumia kuishi kama wako peponi zi za kwao kutakalika kweli?Tuitumie nafasi hiyo na kwenda kufanya mambo huko vijijini uone kama hawataiondoa CCM madarakani!Mugo"The Great";130369 said:Ukweli ni kuwa "Watanzania" ni kama watu waliorogwa lakini ukichunguza kwa undani si kurogwa bali ni upeo wa elimu ya kuchanganua mambo na sera. Huwezi kuamini katika vijiji vya Tz, wanaamini bila CCM hakuna AMANI. Hiki ndicho kinachowafanya "MAFISADI" waendelee kula kuku kwa mrija. Nashauri vyama vya "SIASA" vifungue "VITUO au MAKTABA" za habari ambapo yatapatikana magazeti ya kila siku na Viperurushi kutoka Vyanzo mbalimbali vya habari" ili hata wale wasio na uwezo kupata magazeti waweze kupata habari. Wachache watakaoweza kusoma at grass root level watasaidia kusambaza habari ambazo ni sensitive. Huwezi kuamini nimetembelea Nguruka, Uyumbu-Ussoke, Sitalike-Mpanda na Misigiri' nikakuta wananchiwengi hwajui kuwa BoT ndiyo injini ya nchi, wanafikiri ni kama benki nyingine nchini.
sawa tu almradi tubaki kwenye pointi na kuwa serious!jmushi1:
Mjadala huu juu ya "Serikali Ishinikizwe......" unazungumzia mambo yale yale yanayozungumziwa kwenye mjadala mwingine uliopo hapa ulioanzishwa na Mr. EWA wenye kichwa cha habari: "Mbinu za Kutokomeza Ufisadi...."
Lingekuwa jambo zuri kama MODS wangeiunganisha mijadala hii miwili ili wanaJF waweze kutoa mawazo yao mahala pamoja kuhusu njia zinazoweza kutumiwa kuondosha ufisadi, tena wa nguvu, usiokuwa na aibu wala haya unaofanywa na watawala wetu.
WAKATI watu wengi wakijitosa kuzungumzia kashfa ya ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu (BoT), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ameonekana kusita kuungana nao.
Mwinyi aliweka bayana msimamo wake huo, nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi, muda mfupi tu baada ya kukamilika kwa hafla ya ufunguaji wa akaunti katika Benki ya NMB, kwa ajili ya michuano ya soka ya Kombe la Ali Hassan Mwinyi Orphans.
Rais huyo mstaafu ambaye alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa gazeti hili, alisema ni mapema mno kwa sasa kueleza msimamo wake kuhusu jambo hilo na akaahidi kufanya hivyo wakati muafaka utakapowadia. "Suala la BoT aahaaa , siwezi kuzungumzia, ni mapema mno (kicheko), wakati ukifika nitalizungumzia," alisema rais huyo mstaafu huku akiingia nyumbani kwake.
Mwinyi anaweka bayana uamuzi wake huo ikiwa ni takriban wiki mbili sasa tangu Rais Jakaya Kikwete alipochukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, siku chache tu baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za taasisi hiyo nyeti, kazi iliyofanywa na Kampuni ya kimataifa ya Ernst & Young.
Ballali aliyeko nchini Marekani anakoaminika kuwa alikwenda kutibiwa tangu katikati ya mwaka jana, ndiye ofisa pekee wa juu wa serikali ambaye tayari amehusishwa kwa namna moja au nyingine na ufujaji wa shilingi bilioni 133, fedha za umma kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Mbali ya Ballali, viongozi wengine kadhaa wakiwamo Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati fedha hizo zikichotwa mwaka 2005 na Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina wakati huo, ni miongoni mwa viongozi ambao majina yao yanatajwatajwa kuwa miongoni mwa watu wanaostahili kuwajibika au kuwajibishwa kutokana na ubadhirifu huo.
Tangu Kikwete atoe uamuzi huo, kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa watu kadhaa binafsi na taasisi za kijamii na kidini zilizoeleza kushtushwa na kugundulika kwa ubadhirifu huo mkubwa wa kwanza kuwekwa hadharani hapa nchini. Katika hatua ya hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama cha siasa cha PPT-Maendeleo, Peter Mziray, ameitaka kamati iliyoteuliwa na Rais Kikwete, kuacha kufanya uchunguzi zaidi, na badala yake iwakamate viongozi wa taasisi za serikali, makampuni binafsi na wafanyabiashara ambao wametajwa katika ripoti ya Kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya Ernst & Young kuhusika katika uchotaji wa fedha katika akaunti ya madeni ya nje (EPA).
Mziray aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa kitendo cha wanasheria kuomba wapewe taarifa kutoka kwa wananchi ni kupoteza muda, kwani masuala mengi ya msingi ambayo yanaweza kutumika kama ushahidi mahakamani, yalishabainishwa na kampuni hiyo.
Alisema kilichotakiwa kwa timu hiyo ni kutafuta vielelezo zaidi kutokana na maelezo yaliyotolewa na Ernst & Young kama vile kutafuta kumbukumbu za makampuni hayo katika ofisi za wakala wa usajili wa makampuni - BRELA. Kwa upande mwingine, Mziray alisisitiza kuwa, anauona uhusiano wa kisayansi kati ya uchotaji wa fedha kutoka BoT na ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.
"Mwaka 2004 magazeti humu nchini yaliandika kwamba NEC ya CCM ilimwomba mwenyekiti wake wa wakati huo kuziongezea uwezo wa kifedha, magari na vitendea kazi ofisi za chama hicho nchini pote. Na baada ya muda mfupi, CCM ilimwaga magari ya kuzinufaisha ofisi za wilaya zote pamoja na kugawa kanga, fulana na kofia nchi nzima. Tunahoji walipata wapi pesa kwa muda huo mfupi?
"Mimi sioni lolote la kumpongeza Rais Kikwete eti kwa kutengua ajira ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu kwani ni sehemu ya utendaji wake," alisema. Alisema yeye ataridhika iwapo waliotajwa kuhusika na upoteaji wa fedha hizo wakichukuliwa hatua stahili kama vile kukamatwa na kuhojiwa, kwani ukiacha Dk. Ballali ambaye yupo nje ya nchi, wengi wa waliotajwa wamo humuhumu nchini.
Alisema kuwa bila ya jambo hili kuchukuliwa hatua kwa umakini, uamuzi wa kuzirejesha fedha hizo unaweza usitekelezeke. Aidha, Mziray alimtaka aliyekuwa waziri wa fedha wakati wizi huo ulipotokea, Basil Mramba, na Waziri wa Fedha wa sasa, Zakia Meghji, kujiuzulu, si kwa kuwa wanahusika na wizi huo, bali ili kulinda heshima zao.
Habari Mpya | Kitaifa | Dar | Mikoani | Tahariri | Makala | Michezo | Matangazo | Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd. Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233 faksi +255-22-2126234 Selula 0713 296570
WATU WA MIJINI KUNA NAMNA NYINGINE YA KUONGEA NAO..KUMBUKA WENGI WAO NI CORRUPT!NDIO MAANA JIJI LINAITWA "BONGO"CORRUPTION NI KAMA FASHION NA JINA LENYEWE LINATUONYESHA HIVYO!NA UKUMBUKE KUWA WENGI WA HAO WAKAZI WA VIJIJINI WANAMIMINIKA KILA SIKU MIJINI NA JIJINI KUSAKA MAISHA BORA!WALISHACHOSHWA NA MAISHA YA VIJIJINI!HAWAWEZI KUAMINI KUWA SERIKALI ITAWASAIDIA ETI KWASABABU WAMEKUJA JIJINI!WATAJIULIZA KWANINI HAWAKUPATA HIYO MISAADA WALIPOKUWA UKO VIJIJINI?"Mwisho; ninaamini mabadiko yanawezekana..ila ni baada ya uwajibikaji.Ni kweli kwamba sisi wenyewe ndio wakujibadili.Lakini MADILU usisahau kuwa asilimia zaidi ya 80 ya watanzania wako vijijini ambako bado wanahitaji msaada wa hali ya juu;moja kuwahelimisha,kuwasaidia ili waweze kwanza kabisa haki zao,uraia wao, umuhimu wao,pia ni kuwaelimisha na kuwaonyesha ni kwajinsi gani umasikini wao, maradhi yao,magonjwa yao,ukame wao,uduni wao wa elimu,ukosefu wao wa maji na matibabu,kuwaonyesha direct link kati ya matatizo yao yote na maamuzi yao wanapokwenda kupiga kura!Wajue kwamba upigaji wao kura ndio hatua ya kwanza na hatua ya pili ni kufanya mabadilko na kutegemea mabadilko.Kwamba wanaweza kuwachagua viongozi wengine wanaoweza kufanya kazi ya kuwaondoa kwenye matatizo yao."
Tatizo haliko vijijini tatizo liko kila kona ya nchi.
Watu waishio Dar wameshindwa kufanya mageuzi ya kumchagua hata mbunge mmoja mwanamageuzi toka vyama vya upinzani.
Kama Dar nzima haina mbunge hata mmoja kutoka chama chochote cha upinzani, ni vipi uelewa mdogo wapewe wananchi wa vijijini tu?
Wananchi wote wa Dar, pia wana uelewa mdogo sawa na ule wa 80% ya walio vijijini hawajatuonyesha tofauti yeyote.
Elimu ya utambuzi wa haki za uraia itolewe nchi nzima iwe Dar au kijiji cha Kyabakari kule Musoma vijijini ili kuleta utambuzi wa nguvu ya wananchi ilojituliza kwa kila mmoja ikisubiri kutumiwa vyema.
Rushwa pengine inaonekana halali zaidi mbele ya wananchi wa Dar kuliko hata wale wa vijijini, kwa sbabu watu wa mijini wamezoea kuishi maisha ya ubabaishaji na pengine maisha nusu.
Kura zinaibiwa vizuri Dar kuliko kule vijijini.
Watu wa Dar ndo wepesi kutatua matatizo yao kwa kile wakiatacho Quick Fix kuliko wale wa vijijini.
Watu wa mijini wakilinganishwa na wale wa vijijini, hawana subira.
Wananchi wa vijini wanajua vema kufanya jambo sahihi wakati sahihi katika shughuli nzima za shamba. Wanaelewa wazi na kwa upeo mkubwa kwamba inachukua msimu mzima kusuburi mazao yakomae shambani.Natural Principle
Wanajua kusoma majira vema na nini cha kufanya katika majira hayo kwa usahihi mkubwa.
Kwa kuzingatia hilo yawezekana ni rahisi kumweleza mwananchi wa kijijini akaelewa vizuri kuhusu haki yake ya uraia kwa kutumia mifano ya mazingira aishiyo na majira mbali mbali ya mwaka na miongo na karne kuliko kumwelimisha mtu wa mjini,aliye zoea Quick Fix,juu ya somo hilo hilo.
Kwahiyo kama tunatambua kwamba Uwezo wa kuleta mageuzi u mabegani mwetu, ni vema kupiga hatua moja mbele na kutambua pia kwamba watu wa mijini vile vile wana matatizo makubwa ya utambuzi wa haki zao sawa na wale wa vijijini.
Ujanja wao wa usoni pengine ndo ufichao udhaifu wao.