Mbinu za kutokomeza UFISADI

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
25,372
23,303
Tunataka Serikali ya CCM ielewe kwamba kama ikiendelea na viini macho dhidi ya watanzania then watanzania wote tulioko nje tutazishinikiza serikali za magharibi kujaribu kuhakikisha kwamba this time haki inatendekana hakuna mazingaombwe!
Uwajibikaji ni lazima uwepo this time!
Inashangaza kuona Serikali inasema wananchi wanahojiwa ili kujua ukweli wa tuhuma za ufisadi kabla ya kumhoji Balali?
Rais alimfukuza kazi kwasababu gani?Anawahoji wananchi na kula meza moja na mafisadi?
Kama Kikwete anajua madhara yatakuwa makubwa ukweli ukianikwa hadharani then hayo ni matatizo yake..Tunataka ukweli na uwajibikaji!
Afute baraza lote la mawaziri ikiwezekana..ama yeye mwenyewe ajiuzulu ikibidi!Huo ndio uwajibikaji!Nchi si ya watu wachache!Ni ya raia zaidi ya milioni 30!
 
Huko Tanzania kama mambo hayaendi sawa then "MAANDAMANO" Ni muhimu!Kwa watanzania walioko USA KUNA UTARATIBU UNAANDALIWA WA KUISHINIKIZA SERIKALI YA MAREKANI IFUATILIE KWA KARIBU UJAMBAZI NA UFISADI HUU KWANI SERIKALI INAWASIKILIZA WAO KULIKO SISI WENZETU NA SIE!
 
Tatizo kubwa ni kutokuelewa haki ambayo wananchi wanayo kumuondoa madarakani rais ambaye anashirikiana na majambazi kuiba pesa ya walipa kodi.

Angalia Italy Prodi ameisha chemsha wakati sisi tunamwachia tu na kufanya anavyotaka, hata wabunge ambao ndio wangekuwa mstari wa mbele wanafyata mkia, kazi ni kubwa.
 
Tatizo kubwa ni kutokuelewa haki ambayo wananchi wanayo kumuondoa madarakani rais ambaye anashirikiana na majambazi kuiba pesa ya walipa kodi.

Angalia Italy Prodi ameisha chemsha wakati sisi tunamwachia tu na kufanya anavyotaka, hata wabunge ambao ndio wangekuwa mstari wa mbele wanafyata mkia, kazi ni kubwa.
Ni kweli kazi ni kubwa lakini this time haitakiwi yaishe hivi hivi tu..Wenye kuelewa wawa"organize wananchi popote pale walipo Duniani ili kuhakikisha this time haki inatendeka!Watanzania wote popote walipo hapa duniani ni lazima washirikiane kuhakikisha kwamba serikali inawajibishwa!Kama Kikwete asipochukua hatua..then tutachukua hatua!
 
Ni kweli, this time mpaka kieleweke TZ tumezidi kuwa "kichwa cha mwendawazimu," tumeonewa kiasi cha kutosha, tumeibiwa kiasi cha kutosha na kudanganywa kuliko pitiliza na ahadi zisizotimizwa, haya yote ni upole wetu, unyamavu wetu, amani yetu na ujinga wetu(i can say that too) ila wakati ni huu wa kuamka usingizini... something has to happen NOW.This is a lot of money to go into 'few selfish individual's pockets'....we can't afford to keep quiet this time NO NO NO its just too much to handle and extremelly shameful...Let's wake up and act together kuukomesha huu udhalimu!
 
Ni kweli, this time mpaka kieleweke TZ tumezidi kuwa "kichwa cha mwendawazimu," tumeonewa kiasi cha kutosha, tumeibiwa kiasi cha kutosha na kudanganywa kuliko pitiliza na ahadi zisizotimizwa, haya yote ni upole wetu, unyamavu wetu, amani yetu na ujinga wetu(i can say that too) ila wakati ni huu wa kuamka usingizini... something has to happen NOW.This is a lot of money to go into 'few selfish individual's pockets'....we can't afford to keep quiet this time NO NO NO its just too much to handle and extremelly shameful...Let's wake up and act together kuukomesha huu udhalimu!
MANENO YAKO YANAONYESHA UZALENDO HALISI!SASA NI WAKATI WA KUSHIRIKIANA BEGA KWA BEGA KUIKOMBOA NCHI YETU KUTOKA MIKONONI MWA MAFISADI!BABU ZETU WALIWAONDOA WAKOLONI NA SASA NI SISI KUWAONDOA MAFISADI!
 
jmushi1:
Machungu yaliyo moyoni mwako, na yanayojionyesha hapa katika maandishi yako tunayo pia wengi wetu hapa JF. Ukifuatilia karibu kila mjadala unaoletwa hapa kwenye jamvi hili la siasa na wachangiaji mbalimbali kuhusu manung'uniko juu ya watawala wetu wa chama na serikali ya ccm.

Na ukichunguza vizuri pia myenendo ya hawa watawala wetu, utaona kuwa kelele zinazopigwa hapa JF na kwingineko ni kama hawazisikii na wala haziwastuwi hata chembe. Mfano mzuri ni hilo sakata la Ballali na BOT, na jinsi Mkuu wa nchi na wenzake wanavyolichukulia. Hatua zote zinazotendeka ni bayana kwamba ni harakati tu za kufifisha mambo; hakuna wahusika wakubwa wa hili jambo watakaoguswa. Mwelekeo huu unatulazimisha wengi tuamini kwamba wakubwa wengi,tokea Mkapa hadi Kikwete mwenyewe ni wahusika katika uhujumu huu waliofanyiwa waTanzania. Kwa hiyo njia zinazofanywa sasa ni kutafuta njia ya kuwapata akina 'yakhe' wachache kama akina Ballali watakaokidhi lawama za wananchi; na hapo hapo wananchi hao wakichochewa washangilie uhodari huo mkubwa uliofanywa na mwenye nchi. Na waTanzania wako tayari, tunasubiri tu kuambiwa, ili tuanze kushangilia ushindi huo.

Sasa basi, tukirudi kwenye hoja yako ya msingi - ya baadhi ya waTanzania waliochoshwa, wengi wetu tukiwemo humu humu JF - kutafuta njia za kuwafanya wakubwa watambue kuwa hawawezi kuendelea kutupuuza wananchi kwa ujumla wetu.

Kelele tunazopiga humu kila siku kusema kweli hazina nguvu yoyote ile bila ya kuwa na utaratibu wa kutenda; ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi.
Jambo la kuwalalamikia wahisani linawezekana sana, lakini siamini kuwa linaweza kutokana na kusimamiwa na wanachama wa JF. Wengi wetu hapa tupo tukiumia na kuwa na uchungu mkubwa, lakini inapofikia katika hatua ya kushirikiana lifanyike jambo, hapo panakuwa na uzito mkubwa mno. Binafsi sioni watu wa JF wakishirikiana na kushinikiza serikali au fisadi hata mmoja tu alazimike kufanya jambo. Kuna wachache, katika makundi ya wawili au kadhaa, wanaweza kwa mfano wakashirikiana kwa pembeni wakaandika barua au ujumbe kuwafikia, tuseme 'wahisani'. Hilo nadhani inawezekana.

Nisilolifahamu mimi ni kuhusu vyama au asasi zisizo za kiserikali zilivyo hapa kwetu Tanzania. Hivi hapa hatuna 'Civil Societies' na NGOs ambazo kazi yake ni kuwapigia serikali kelele kila mara serikali inaposhindwa kufanya kazi? Hivi hawa watu wapo wapi? Hawa ndio wangeweza kuwa na sauti barabara, hasa hiyo ya kuwashitaki mafisadi hawa kwa hayo mashirika ya kimataifa na hao wahisani wanaotoa misaada kila mwaka. Ni hawa hawa ndio wangekuwa wakufunzi wakuu kuwataarifu wananchi kila mara mambo mazito kama haya ya BOT yanavyotokea na usanii unaofanyika katika kupoteza lengo ili wahusika hasa wasifahamike. Hawa watu wapo wapi?
HakiElimu ilijitahidi kidogo na mambo ya elimu huko miaka iliyopita; lakini nadhani na wao sijui walitishwa, siku hizi hawasikiki kabisa.

Kwa hiyo ndugu zangu jmushi1, mashoo, Dua na wengine; mimi ninaamini kuwa bila kuwepo na njia zitakazokuwa zinawaelimisha na kuwafahamisha wananchi kuhusu mambo haya ya ufisadi na uhujumu wa nchi yetu hii, hatutaweza kamwe kujinasua. Vyama vya siasa vya upinzani inaelekea uwezo huo hawanao kabisa. Akina Slaa, Zitto na akina Hamad peke yao hawawezi.
 
katika hali iliyojitokeza Bot na sehemu nyingine ndani ya nchi yetu,mimi niko na maombi mawili kwa ndugu zangu wanaJF.

1. Je ni kweli kwamba tumeridhika kweli mabilioni kuliwa na sisi tubaki tunalia na kupiga kelele tu? nafikiri tujaribu kuchangia mawazo ni njia ipi ambayo itatuwezesha hawa waliokula fedha zetu wazirudishe na pia sheria yetu akate kama ilivyokusudiwa na isiogope kigogo yeyote kwani tunaamini hakuna mtu yuko juu ya sheria na kama tunayemtegemea awawajibishe kashindwa basi tumwambie na tuangalie ni jia ipi tunaweza kuwawajibisha hao waliochota hadhina ya taifa letu.2.Kwa mtizamo wangu naona kama tunaweza piga kelele bila njia madhubuti ya kuhakikisha hili linakuwa fundisho kwa viongozi wetu tuliowapa uongozi wasitumie nafasi zao kufuja mali ya nchi,Je nini kifanyike kuhakikisha hali hii haitokei tena kwani hali hii inawezajitokeza baadaye tena tusipoziba ufa kabisa na hali hii ikitokea mara kwa mara inahatarisha taifa kurudi nyuma kiuchumi na kufanya ndoto ya maisha bora kutokomea kabisa.

Hitimisho, Karibuni kwa michango yenu kwani mawazo yanaweza kutusaidia kufanya nini ilituepukane na ufisadi huu unaotetewa na viongozi wetu tuliowapa uongozi.
 
Mh Kalamu;
Kwanza nashukuru sana kwa ushauri na mawazo pamoja na uchangiaji wako kwenye hii thread.
Yote uliyoyasema ni kweli tupu! Na mimi sio mshirikina lakini this time naamini there's something!
Kwani nilishtushwa sana na uamuzi wa watanzania kumpongeza Rais Kikwete! Watanzania ni wazi sasa tuko kama misukule ambao hatujui ni nini kinandelea.Haya...Kabla hata sijakaa sawa nasikia eti kamati ama bodi iimeundwa kuchunguza mafisadi! wapi accountabilty? Wananchi wanahojiwa badala ya Balali na wenzake?

Kama watu wanaelewa kwamba uchunguzi ni wazi ulishafanyika.OK Balali kapigwa chini..Vipi kuhusu hao wengine waliopiga masignature ya kuapprove huo uozo?WAMEWAJIBISHWA?
Rais mwenyewe something kama kashfa ikitokea ananzisha ziara za kuwafumba wananchi macho na kuandaliwa dhifa mbali mbali za ufunguzi wa miradi! Hii yote ni kuwahadaa wananchi kwamba serkali inawatumikia vyema.
Na sisi tumezoe kuridhika na shida. Na mawaziri wake!Si unakumbuka baada ya kashfa ya migodi i.e Buzwagi aliwaambia mawaziri wake waende mikoani? Kikwete akiwa underpressure ni wazi anajulikana!

Sio na watu wote,bali ni wachache!
Hivi kweli tutafika?
Huu ndio wakati pekee wa kujaribu kuwawajibisha viongozi wetu ambao badala ya kuwatumikia wananchi na nchi yetu,ni kinyume wananchi na nchi yetu ndio wanawatumikia viongozi?
Bush anakuja bongo..so balozi wao nae pia anatakiwa ambrief kuhusu mambo haya!
La mwisho ni kubadili katiba ili mambo yasije kuwa kama ya kenya ambapo sasa hivi itabidi waibadili katiba ila baada ya damu kumwagika!
KATIBA NI KILIO CHA KWANZA CHA WAPENDA DEMOKRSIA NCHINI MWETU KAMA KWELI TUNATAKA MABADILKOA KWELI!
 
WAKATI watu wengi wakijitosa kuzungumzia kashfa ya ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu (BoT), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ameonekana kusita kuungana nao.

Mwinyi aliweka bayana msimamo wake huo, nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi, muda mfupi tu baada ya kukamilika kwa hafla ya ufunguaji wa akaunti katika Benki ya NMB, kwa ajili ya michuano ya soka ya Kombe la Ali Hassan Mwinyi Orphans.

Rais huyo mstaafu ambaye alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa gazeti hili, alisema ni mapema mno kwa sasa kueleza msimamo wake kuhusu jambo hilo na akaahidi kufanya hivyo wakati muafaka utakapowadia. "Suala la BoT… aahaaa…, siwezi kuzungumzia, ni mapema mno ………(kicheko), wakati ukifika nitalizungumzia," alisema rais huyo mstaafu huku akiingia nyumbani kwake.

Mwinyi anaweka bayana uamuzi wake huo ikiwa ni takriban wiki mbili sasa tangu Rais Jakaya Kikwete alipochukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, siku chache tu baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za taasisi hiyo nyeti, kazi iliyofanywa na Kampuni ya kimataifa ya Ernst & Young.
Ballali aliyeko nchini Marekani anakoaminika kuwa alikwenda kutibiwa tangu katikati ya mwaka jana, ndiye ofisa pekee wa juu wa serikali ambaye tayari amehusishwa kwa namna moja au nyingine na ufujaji wa shilingi bilioni 133, fedha za umma kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Mbali ya Ballali, viongozi wengine kadhaa wakiwamo Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati fedha hizo zikichotwa mwaka 2005 na Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina wakati huo, ni miongoni mwa viongozi ambao majina yao yanatajwatajwa kuwa miongoni mwa watu wanaostahili kuwajibika au kuwajibishwa kutokana na ubadhirifu huo.

Tangu Kikwete atoe uamuzi huo, kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa watu kadhaa binafsi na taasisi za kijamii na kidini zilizoeleza kushtushwa na kugundulika kwa ubadhirifu huo mkubwa wa kwanza kuwekwa hadharani hapa nchini. Katika hatua ya hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama cha siasa cha PPT-Maendeleo, Peter Mziray, ameitaka kamati iliyoteuliwa na Rais Kikwete, kuacha kufanya uchunguzi zaidi, na badala yake iwakamate viongozi wa taasisi za serikali, makampuni binafsi na wafanyabiashara ambao wametajwa katika ripoti ya Kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya Ernst & Young kuhusika katika uchotaji wa fedha katika akaunti ya madeni ya nje (EPA).

Mziray aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa kitendo cha wanasheria kuomba wapewe taarifa kutoka kwa wananchi ni kupoteza muda, kwani masuala mengi ya msingi ambayo yanaweza kutumika kama ushahidi mahakamani, yalishabainishwa na kampuni hiyo.

Alisema kilichotakiwa kwa timu hiyo ni kutafuta vielelezo zaidi kutokana na maelezo yaliyotolewa na Ernst & Young kama vile kutafuta kumbukumbu za makampuni hayo katika ofisi za wakala wa usajili wa makampuni - BRELA.

Kwa upande mwingine, Mziray alisisitiza kuwa, anauona uhusiano wa kisayansi kati ya uchotaji wa fedha kutoka BoT na ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. "Mwaka 2004 magazeti humu nchini yaliandika kwamba NEC ya CCM ilimwomba mwenyekiti wake wa wakati huo kuziongezea uwezo wa kifedha, magari na vitendea kazi ofisi za chama hicho nchini pote.

Na baada ya muda mfupi, CCM ilimwaga magari ya kuzinufaisha ofisi za wilaya zote pamoja na kugawa kanga, fulana na kofia nchi nzima. Tunahoji walipata wapi pesa kwa muda huo mfupi? "Mimi sioni lolote la kumpongeza Rais Kikwete eti kwa kutengua ajira ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu kwani ni sehemu ya utendaji wake," alisema.
Alisema yeye ataridhika iwapo waliotajwa kuhusika na upoteaji wa fedha hizo wakichukuliwa hatua stahili kama vile kukamatwa na kuhojiwa, kwani ukiacha Dk. Ballali ambaye yupo nje ya nchi, wengi wa waliotajwa wamo humuhumu nchini.

Alisema kuwa bila ya jambo hili kuchukuliwa hatua kwa umakini, uamuzi wa kuzirejesha fedha hizo unaweza usitekelezeke. Aidha, Mziray alimtaka aliyekuwa waziri wa fedha wakati wizi huo ulipotokea, Basil Mramba, na Waziri wa Fedha wa sasa, Zakia Meghji, kujiuzulu, si kwa kuwa wanahusika na wizi huo, bali ili kulinda heshima zao.


h.sep3.gif

juu
blank.gif
blank.gif
amka2.gif
blank.gif
blank.gif
Habari Mpya | Kitaifa | Dar | Mikoani | Tahariri | Makala | Michezo | Matangazo | Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd. Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233 • faksi +255-22-2126234 • Selula 0713 296570
 
Tunataka Serikali ya CCM ielewe kwamba kama ikiendelea na viini macho dhidi ya watanzania then watanzania wote tulioko nje tutazishinikiza serikali za magharibi kujaribu kuhakikisha kwamba this time haki inatendekana hakuna mazingaombwe!Uwajibikaji ni lazima uwepo this time!Inashangaza kuona Serikali inasema wananchi wanahojiwa ili kujua ukweli wa tuhuma za ufisadi kabla ya kumhoji Balali?Rais alimfukuza kazi kwasababu gani?Kama Kikwete anajua madhara yatakuwa makubwa ukweli ukianikwa hadharani then hayo ni matatizo yake..Tunataka ukweli na uwajibikaji!Afute baraza lote la mawaziri ikiwezekana..ama yeye mwenyewe ajiuzulu ikibidi!Huo ndio uwajibikaji!Nchi si ya watu wachache!Ni ya raia zaidi ya milioni 30!
Kuna jamaa mmoja kaniambia kaacha kabisa kufatilia mamabo ya tanzania.kachoka anasema kila akiiifikiria tanzania machozi yanamtoka.KIla akinywa Heineken yake akaikumbuka tanzania pombe zinamuisha.

Huu ni mfano wa mtu mmoja kati ya watanzania waliochoka na usanii wa serikali yetu.Ipo siku tu watakiona cha mtema kuni
 
"true" Ni Kweli Iko Siku!lakini Siku Yenyewe Ndo Hii!tusisahau Mrema Alijivua Ubunge Na Uwaziri Kipindi Kile Cha Kashfa Ya Kina Mbilinyi!next Time Itakuwa Ni Watoto Wa Vigogo Ndo Wanakula..then Sijui Siku Hiyo Ni Ipi Tena Zaidi Ya Hii?
 
Wako wapi wakina mkjj?Hawaoni umuhimu wa kuchangia?ama anaogopa kukosa interviews?Uzalendo wa kweli unahitaji moyo nakujitolea!
 
Haya tena..Kikwete ndo aliyepongezwa baada ya kuunda kamati ya madini na sio Zitto aliyepoteza maslahi yake bungeni kwa ajili ya kutaka kamati ya bunge iundwe ili kuwe na uwajibikaji wa kweli utakaoshinikizwa na sheria!

Uwajibikaji ambao ni serious kwani unasimamiwa na sheria pindi bunge litakapounda hiyo kamati..
Then hivi sasa anapongezwa tena wakati Dk Slaa kutoka upinzani ndo ametoa hizo siri!?
Anapongezwa lakini hakuna uwajibikaji!?
Wa Tz tunamacho kweli?
 
Rais Bush kutua Bongo mwezi ujao

2008-01-25 18:41:34
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Rais wa Marekani, Bwana Goerge Walker Bush anatarajiwa kuitembelea Tanzania mwezi ujao, taarifa zilizotolewa na kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Marekani, Jijini Dar es Salaam, zimethibitisha.

Hata hivyo haikuelezwa ni tarehe gani kiongozi huyo wa taifa lenye nguvu kubwa duniani atatua Bongo.

Imeelezwa kuwa hiyo inatokana na sababu za kiusalama.
Bw. Bush atatembelea Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo kati ya nchi chache za Afrika anazotarajiwa kuzitembelea.

Marekani na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa karibu katika masuala mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
  • SOURCE: Alasiri
 
Rais Bush kutua Bongo mwezi ujao

2008-01-25 18:41:34
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Rais wa Marekani, Bwana Goerge Walker Bush anatarajiwa kuitembelea Tanzania mwezi ujao, taarifa zilizotolewa na kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Marekani, Jijini Dar es Salaam, zimethibitisha.

Hata hivyo haikuelezwa ni tarehe gani kiongozi huyo wa taifa lenye nguvu kubwa duniani atatua Bongo.

Imeelezwa kuwa hiyo inatokana na sababu za kiusalama.
Bw. Bush atatembelea Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo kati ya nchi chache za Afrika anazotarajiwa kuzitembelea.

Marekani na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa karibu katika masuala mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
  • SOURCE: Alasiri
Haya sasa Bush anakuja bongo!Je atakuwa na ujumbe gani kwa Kikwete?Na je atapata fursa a kukutana na vingozi wa vyama vya upinzani?kumbuka kuwa wao ndo waliojitoa muhanga kuanika uozo wote wa mafisadi!Hapo ndio umuhimu wa demokrasia ya vyama vingi unapojiweka wazi!
 
Kwanza serekali imhakikishie Balali ulinzi na apelekwe mahakamani kueleza namna fedha ilivyochotwa na wote waliohusika kushughulikiwa kisheri.

vyama vya ushindai na wadau wote walioguswa na sakata hili kuandamana nchi nzima kuishinikiza serekali kuacha mzaha na kulishughulikia swala hili kikamilifu na haraka sana.

Asasi zote za kisheria zisizo za serikali zijaribu kuangalia ni sheria ipi itumike kuwapeleka wote waliohusika katika vyombo vya sheria iwapo serikali itaendelea kusuasua.

Iangaliwe namna ya kuwapunguzia nguvu kisheria watendaji wote wenyekutoa maamuzi makubwa yanayoweza kupelekea taifa kupata hasara kubwa.
 
Mr. Ewa,

Unachoshindwa kuelewa hapa ni je Ballali akisema Mkapa alichota pesa ili kumsaidia JK ashinde uchaguzi, kuna kitu kitafanyika?

JK anajua kila kitu kilichofanyika pamoja na watu walioiba, kwahiyo usanii tunaouona ni kwasababu hana ubavu, hawezi kuwashughulikia rafiki zake wakubwa akiwemo Rostam.

Ballali alikuwa na uwezo wa kuzuia huo wizi toka mwanzoni kwa kukataa, kisha kusema ukweli na kuachia nafasi hiyo na kurudi kwake USA, kukaa na familia yake na kupata kazi ya maana zaidi.

Lakini yeye akaona bora ashirikiane nao, matokeo yake wote tunayaona.

Sasa mnataka kumpa ulinzi mtu kama huyo ili iwaje?
 
HISTORIA YA UFISADI TANZANIA
Nimeona nichangie mada hii kutokana na mlolongo wa matukio mbalimbali ya ufisadi na mijadala hapa JF ili tuweze kupanua mjadala huu
Hoja yangu inaanzia takribani miaka zaidi ya 20 iliyopita.

KUFA KWA MASHIRIKA YA UMMA.

Wote tunakumbuka kuwa baada ya Azimio la Arusha mashirika mengi yaliyokuwa ya binafsi yalifanywa ya umma na mengine yalianzishwa na serikali. Sitazungumzia malengo ya kuanzishwa kwa mashirika haya ila nitaangalia kufa kwake.
Pamoja na sababu nyinginezo baadhi ya sababu hizo ni
1. Kuendeshwa kwa hasara (matumizi makubwa kuliko mapato)
2. Kutokuwa na wataalamu wa kutosha kipindi hicho
3. Elimu duni , na kutokuwa na uchungu na mali ya umma
4. WIZI NA UFISADI
5. Namba 1,3 na 4 kwa pamoja
Katika kipindi (1967-1990) nafasi zote za juu za uongozi na usimamizi wa mashirika zilitolewa kwa uteuzi na serikali chini ya chama pekee kilichoshika hatamu wakati huo yaani CCM.
Viongozi waliofuja mali ama kuiba katika mashirika haya hawakufungwa wala kufunguliwa mashtaka bali walihamishwa toka shirika moja kwenda jingine au kupewa nafasi nyingine ya uongozi.

KUFA KWA MADUKA YA USHIRIKA

Mwanzoni mwa miaka ya 80, pale kijijini kwangu kulikuwa na duka la ushirika,wengine waliita duka la kaya.Duka hili pekee kijijini liliweka utaratibu kuwa mwanakijiji atakayepata bidhaa toka duka hili sharti awe mwanachama .
Ili kupata bidhaa ilikuwa kwanza unajiandikisha na kama bidhaa ilikuwa kidogo basi iligawiwa kulingana na ukubwa wa familia na wakati mwingine kwa kuangalia WEWE NI NANI nafikiri mmenielewa hapa.Nakumbuka familia yetu ya watu 7 ilikuwa ikipata nusu kilo ya sukari na robo mche wa sabuni ya ILULA

Bidhaa ziliwekwa kwa madaraja yaani bidhaa adimu na bidhaa za kawaida.Kutokana na bidhaa kutotosheleza mahitaji basi wale wasimamizi wa maduka haya walikula njama na wauzaji wa maduka pekee ya jumla yaani RTC na kuuza kiasi cha mgawo wa kijiji husika kwa wafanya biashara binafsi ambao waliitwa walanguzi na maduka haya ya kijiji kuleta robo ya mgawo wa bidhaa pale kijini.Bidhaa tulizostahili kuzipata duka la kijiji tukawa tunauziwa kutoka majumbani kwa siri (black market) kwa bei ya juu maarufu kwa MWENDO WA KURUKA au Kulanguliwa n.k
Kibaya zaidi haikuishia hapo hata hayo mapato yaliibwa na maduka kufa kabisa.Nafikiri hii ilikuwa nchi nzima si kwa maduka ya kijiji tu bali hata ya kitaifa kama RTC,Mashirika kama SUKITA na viwanda.

RUSHWA MAHAKAMANI, BARABARANI, BANDARINI, TRA N.K

Kuna rafiki yangu mmoja tuliwahi kusoma shule moja sasa yeye ni askari polisi.Huyu rafiki yangu aliniambia kwamba anatamani kuwa kitengo cha trafiki au cha upelelezi nilipomuuliza sababu aliniambia huko ndio kwenye madili.Sasa niliwahi kudokezwa pia hali ipo hata katika baraza la mawaziri.Kuna baadhi ya wizara ambazo zinachukuliwa kuwa ndio zenye madili na nyingine hazina madili.Hizi zenye madili hupewa wale walio karibu na mkuu wa nchi.Mfano wa wizara hizo ni Fedha, Maliasili,Viwanda na biashara , Ujenzi pamoja na Wizara ya Nishati na Madini. Nini maana ya madili?

RUSHWA /UFISADI KWENYE MIKATABA NA WIZI Sasa tukija kwenye hii ishu ya ufisadi benki kuu, buzwagi,Richmond n.k ambayo imegeuka kama swala tano kwa watanzania,tuangalie historia wakati tunaweka matumaini kwa serikali yetu kuchukua hatua.

Pili tujiulize pia maswali sisi wenyewe tumechukua hatua gani.

1. Pamoja na kujua ufisadi wote tangu uhuru tumeendelea tumeendelea kuwachagua walewale waliotufisadi

2. Pamoja na kuwajua wezi tumeendelea kuwachagua waliotuibia shilingi elfu moja wakatununulia peremende ya shilingi moja na ahadi za sherehe mwezini wakati wa kampeni

3. Pamoja na kujua tumedanganywa hatuulizi na kuhoji ahadi bali tunawasifu na kuwapigia makofi wakituongezea ahadi

4. Badala ya kuchukua hatua za kisheria imeundwa tume,badala ya kuwakata wahusika sisi tunashangilia na kusifu kwa gavana anayelipa kutenguliwa uteuzi ,wakati walioidhinisha malipo wapo ofisini wakitucheka na sisi tunashangilia

5. Tunajua mafisadi wa rada wamefanya nini,leo mhusika mmoja amefunguliwa shitaka la kudanganya, si la uhujumu uchumi, amefika mahakamani hata hivyo?
Kwa ufupi tukirejea historia tunaweza kujiuliza yafuatayo.
Ni kiongozi gani mtiifu wa CCM na serikali amewahi kuhukumiwa kwa ufisadi na kwenda jela

Kama hakuna leo tunashangaa nini iwapo ufisadi umedhihirika na hakuna aliyefunguliwa mashtaka

NAHITIMISHA KWA KUULIZA SWALI:

Pamoja na juhudi za akina Slaa kuweka mambo hadharani sisi wananchi tumewaunga mkono vya kutosha?.Viongozi wa vyama mbalimbali za kiraia wanapiga kelele kuhusu mabadiliko ya katiba ikiwa ni pamoja na vipengele vinavyolinda uhalifu kama kutomshitaki rais aliye madarakani au aliyetoka madarakani,kupunguza nguvu za rais n.k sisi wananchi tumewaunga mkono vya kutosha.

JE WATANZANIA TUNALEA UFISADI?
 
MR EWA.

Heshma kwa kuanzisha hii thread nzuri.

Mkononi kwangu nina magazeti mawili yana makala ambayo kama zingekuwa na WEBSITE ningewapa moja kwa moja. Kuna Watanzania wawili shupavu kabisa. Wametoa mawazo yao Loud and Clear! related na topic ... MBINU ZA KUTOKOMEZA UFISADI NCHINI MWETU. Ni gazeti la Mwanahalisi(jumatano.january 23-29,2008) na Gazeti la Rai.rai.(Alhamisi, januari 24-30,2008) Gazeti la Rai wana web www.newhabari.com/rai lakini hiii makala sioni humo.

Mwananchi wa kwanza:

Jasper Mirenyi: Anasema yuko Arusha Tz: simu: 0773 463 332

Ameandika:Makala ya WAZO MBADALA: Kichwa cha habari:

ANDAMANENI KUPINGA UFISADI

Anawaandikia Vijana wa vyuo vikuu Tz.

Paragraph moja anasema:
... Maandamano ya amani yaliyofanyika kulaani yanayotokezea Kenya hayakuwa na umuhimu sana kwa Watanzania wanaoadhirika na kuangamia...kwa ufisadi wa BoT ...Ufisadi huu unafanyika huku wananchi wakiona... Hebu vijana vyuo vikuu shikamaneni barabara na mlilie hali za mamilioni ya masikini walioko vijijini mlikotoka baadhi yenu...Huu ndio wakati muafaka kuwa hamasisha wananchi bila ya kujali itikadi washinikize serekali ikamate wote waliohusishwa na ufisidi...Ni kufanya maandamano ya amani kushinikiza kukamatwa kwa kampuni zilizotajwa. Mshinikize pia kujiuzulu kwa mawaziri walioshindwa kusimamia utendaji wa taasisi hiyo...

Mwananchi wa Pili:

Abel pangamawe <brazaabel@yahoo.com>: 0755479082. Ameandikia Rai.
anasema hivi:

WANAFUNZI ELIMU YA JUU NA UFISADI TANZNANIA.​

Wasomi waliandamana 'kupinga machafuko yaliyopo kenya' kuanzia ubungo na kumalizia viwanja vya jagangani. Abel Anasema kwa hilo nawapongeza...Nawauliza; Ni mangapi yametokea nchini mwetu, tena yanawaumiza Wa tanzania wakati wamo wao wenyewe? Bila shaka ni mengi lakini wamefunika Midomo yao na kusema chini chini katika vyumba vyao vya kupumzikia... Anaendelea: Sasa wakati umefika kwa wanafunzi wetu kutumia nafasi yao tulyowapa..ili kuibua uchafu uliopo kwenye jamii na hata serekali yanayofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wasio safi...

Makala ni ndefu laniki nimevutiwa na paragrafu hiy.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom